Walimu wa Ajira mpya 2014: List ya waliokubaliwa kubadilishiwa vituo!

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,202
5,012
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA

SERIKALI ZA MITAA

WALIMU WA AJIRA MPYA 2014 WALIOKUBALIWA KUBADILISHIWA VITUO

Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imefanya mabadiliko ya vituo vya kazi kwa walimu Ajira mpya mwaka 2014 baada ya kupokea na kuchambua maombi mbalimbali kutoka kwa walimu walioomba kubadilishiwa vituo.

Hivyo walimu wote walioomba kubadilishiwa vituo lakini majina yao hayapo katika orodha hii kwa ngazi zote watambue kuwa maombi yao hayakukubaliwa na hivyo wanatakiwa kwenda kuripoti katika vituo walivyopangiwa kwa mujibu wa tangazo la tarehe 15/03/2014.

Inasisitizwa kuwa tarehe ya mwisho ya kuripoti ni 10/04/2014 na ambaye

hataripoti mpaka tarehe hiyo atakuwa amepoteza nafasi ya ajira.

Hakutakuwa na mabadiliko mengine tena.
Tunawatakia kila la kheri.


Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) Kwa Ajili Ya Shule Za Msingi(Bofya hapa)

Walimu wa Stashahada Kwa Ajili Ya Shule za Sekondari(Bofya hapa)

Walimu wa Shahada Kwa Ajili Ya Shule Za Sekondari(Bofya hapa)
 
nashukuru kwa taarifa mkuu tupo pamoja kwen ye ujenzi wa taifa
 
Back
Top Bottom