Mjamaa1
JF-Expert Member
- Apr 9, 2013
- 7,312
- 5,484
You can't be serious, yani unashimda njaa wakati una watu wa kukusaidia? Mkuu wako wa shule umemwambia hali yako? Mkurugenzi , HRO ??Serikali kwanini inapenda kututesa hivi?
Yaani tangu tupangiwe vituoni, hatujapewa pesa yoyote ya kujikimu wala kurudishiwa nauli na kuna tetesi mshahara wa mwezi huu nao hatupewi, yaani shule zenyewe hazina nyumba za walimu, walimu wageni imetulazimu kupanga na kujitegemea kununua mahitaji yote kwa gharama zetu.
Shule zenyewe hazijatupa support yoyote watu tupo mbali na nyumbani mfano kama mimi nimepangiwa Kagera na nyumbani ni Songea, kurudi nyumbani siwezi na huku huduma sipati so nalala njaa muda mwingine na hapa nilipo nanuka madeni maana watu wa kuwakopa hela nao wameisha karibia wote nimewakopa.
Naishi maisha magumu sana, tena sana hadi najuta kupata hii ajira kama mtu anaweza nikopesa 20000 inisaidie hili wiki ninavyoendelea kusubiri hela ya kujikimu utakuwa umeniokoa maana hapa nimelala tu Toka Jana asubuhi sijala chochote.
Na sasa hivi shule zimefunga ni shida tupu yani