"The way you treat your EMPLOYEE is the way they treat your CUSTOMERS, there is no big result now without big salary now"
huo ni ujumbe unaosomeka katika sms zinazo sambaa kwa walimu.
Mimi kama mwalimu naunga mkono hoja kwa 100% kwan hamna Taifa imara bila walimu madhubuti na wanao thaminiwa, kueshimiwa.
Teaching is the mother of all profesionals in the world.
Teachers can either build a strong or weak country.
Wanaoafiki waseme ndiyoooo,....Wasioafiki waseme Hapanaa....!!!! Nadhani wanaoafiki Wameshinda.....
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?
Idiotic question on red. Unauliza majibu?
At least unajua kuwa si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake: hakuna mbadala wa MORALE ya ufundishaji mashuleni kwa kubadili badili majina na slogans huku unawanyonya watendaji na kujinufaisha kwa posho.
Ndugu yangu uliyegoma kutumia akili zako, ni hatua gani serikali imepiga kwa kuleta msamiati wa KILIMO KWANZA mashambani kwa pembejeo na urasimu ule ule?
Mtabadili majina hadi maneno yaishe, lkn kama hamkujifunza kuwajali wanaotumika, basi kina Kagame wataendelea kutupuuza huku tunalalama kama wauza matap-tap waliodhulumiwa na askari wa jiji.
Matokeo makubwa sasa bila mikakati ya muda mrefu ni upumbavu mkubwa,hiyo pesa ya semina wangenunulia madawati huko vijijini ambako magogo yanavunwa lakini bado wanakaa chini,
1)Shule ziwe na mazingira ya kusoma kweli
2)Mitaala ya masomo irekebishwe
3)Walimu wapewe wanachokidai
4)Wazazi watimize wajibu wao
5)Vijijini kupewe nguvu ya ziada kubadili hali ya elimu
Tofauti na hapo tusubiri hili janga lifike elimu ya juu muda siyo mrefu
Walimu hamna lolote tuendelee na woga tu
Mkuu, si kila mtu anaweza kujibu swali hilo. maana wengi wanaoiba iwe serikalini, kwenye makampuni binafsi au mashirika ni wale wenye mishahara mikubwa.
Wanaoiba serikalini ilhli wana mishahara mikubwa sio justification ya serikali kuwapunja walimu mishahara, hizo ni sababu nyepesi tena za kisiasa. Hainiingii akilini kuniambia ukiongeza mishahara haitaleta mabadiliko. Nikukumbushe kuwa, uwepo wa wizi serikalini na kwenye mashirika ya umma ni uzembe mwingine wa serikali na sio jambo linalohusiana na haki wanazodai walimu.
Unaweza kuongea maneno yako ya kuungaunga kadiri upendavyo, lkn nikuulize swali: mbali na mishahara, walimu pia wanadai malimbikizo ya stahili zao za uhamisho na likizo, je nahizo nazo hawapewi sababu wataiba?
Mimi sio mwanasiasa bwana, usinijie na hoja za kuungaunga, hapa tunazungumzia mtu kujikimu ili aweze kutumikia ajira yake kwa ufanisi
Si kila kitu unaweza kukitafutia mbadala wake. hivi maana ya Big Salary ni nini?