Walimu, nipeni comments zenu hapa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Walimu, nipeni comments zenu hapa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by moseskwaslema, Jul 5, 2012.

 1. m

  moseskwaslema Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania wenzangu hasa walimu wa kada zote pamoja na wakufunzi wa vyuo,serikali imetangaza kuongeza mishahara ya watumishi kwa asilimia 15-20 lakini gharama ya maisha imepanda zaidi ukilinganisha na kiwango kilichoongezeka.Lakini ukijaribu kuangalia wabunge pamoja na maofisa wa serikali ambao hawana hata taaluma yoyote wanalipwa fedha nyingi na kwa wanataaluma serikali mara nyingi hujaribu kusema kazi zetu ni wito,hivi uongozi hauwezi ukawa wito?

  Mi nafikiri ni muda mwafaka sasa serikali itueleze kazo ambazo siyo wito,kwa jinsi ninavyojua mimi ni kwamba kila kazi ni wito na ndo maana kili majawetu ana interest yake,interest ndo wito wenyewe.

  Viongozi wa chama cha waalimu hivi karibuni wametangaza kwamba kutakuwa na mgomo endapo serikali itashindwa kutekeleza yafuatayo;

  1.kupandisha mishahara kwa asilimia 100
  2.kima chini kiwe 350,000
  3.walimu walipwe madeni yao yote.
  4.kuwe na posho ya mazingira magumu[hardship nallowance].
  5.kuwa na malipo ya over time.
  6.malipo yanayofanyika katikati ya mwezi kama ilivyo kwa polisi na wahasibu.

  Walimu wa kada zote tuungane katika kutekeleza mgomo huu endapo serikali itakuwa kimya mpaka tarehe 07 mwezi huu.Watanzania nao watuelewe na kutuunga mkono ili maisha yetu yawe bora na hatimaye tuweze kufanya kazi yetu kwa ufanisi zaidi.
   
 2. g

  gforum Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo nyie wenyewe hamjaungana katika kudai haki zenu . Sisi tutawasaidiaje? Kazeni buti, kiukweli nyie ndio mnadharauliwa zaidi ya mfanyakazi mwingine yeyote na ndio mana hata mkisema mnagoma serikali inaona kama mgonjwa hataki dawa na anajua bila dawa hawezi pona. Tafadhali acheni woga gomeni daini haki zenu, msipogoma na iwe mwisho kuimba ule wimbo wa solidarity forever. La sivyo mtadharauliwa zaidi.
   
 3. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Lazima tupachimbe,afu ole wake Abduel ampigie simu Mukoba,!
   
 4. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tatizo la walimu ni kukesekana kwa umoja na sababu ni asilimia kubwa ya waalimu wametumia vyeti feki kupata taaluma hiyo na ajira hasa walimu wa kipindi cha miaka ya nyuma. Waalimu wa shule za msingi na wa sekondari si kitu kimoja ktk mambo km haya mambo ya kudai maslai ktk kazi na wale wa vyuo vya ualimu wao ndio wanajiona wako juu. Tofauti za kimaslai na elimu za kuunga na feki ndio ugonjwa ktk kada hii inavunja umoja. CWT wengi ni walimu wa shule za msingi na wengi ni waoga ndio maana mgomo kwao ni ndoto.
   
 5. Butho Mtenzi

  Butho Mtenzi JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 326
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Bila mabadiliko ya kuing'oa CWT akuna jipya chini ya jua mana hawa ndio kikwazo kikubwa kwa mafanikio kwa Waalimu.Tuanze na hao may be mafanikio yataja patikana
   
 6. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,815
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  he mugomo tena! nasikia chadema walimwendea Mukoba akaogopa ya Ulimboka
   
 7. j

  jaje Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  walitenga mil200 kuwalipa madaktari wa nje...watenge zingine za kuwalipa waalimu wa nje..GOMENI mnadharauliwa sana
   
 8. N

  Njangula Senior Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi napenda walimu tugome lkn tatizo kuna baadhi ya walimu mgomo kwao mwiko kisa kapewa kanafasi fulani. Pia walimu wa primary ni janga kubwa ndani ya CWT kazi kujikombeleza tu kwa kuwapelekea kuku na mahindi wakubwa wilayani. Migomo yetu pia itakosa dira kwa vile fani imevamiwa na yoso toka UDOM who strike emotionally only. I dream no success at all.
   
 9. k

  kasahunga Senior Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  tatizo la walimu ni kutokujielewa wenyewe kwa sababu wanashidwa kujua haki zao. kwani mazingira ya kufanyia kazi ni magumu sana lakini wenyewe hawajui. kingine ni viongozi waliopo wapo kwa manufaa ya kisiasa .kwani kuna wenyekiti wa cwt wilaya bunda ni mjumbe wa nec ya ccm je anaweza kusaidia walimu ili waweze kudai mambo ambayo umeyaweka hapo.
   
 10. dedam

  dedam JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 846
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  walimu hawewizi kugoma sabacu walimu wengi wanatumia vyeti si vyao. pili walimu wa kike ndio waliopangwa shule zenye mazingira mazuri so akigoma anaogopa kupelekwa shule zenye mazingira magumu. walimu wa kiume wengi wapo shule za chaka ambao wao walishagoma siku nyiingi!
   
 11. k

  kasahunga Senior Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 170
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko na kuwa na chama kingine cha walimu badala ya kuwa na cwt ambayo haiwezi kumtetea mwalimu. tuungane na walioanzisha UMET ili tuweze kuingoa cwt kwani ni mshirika wa ccm
   
 12. N

  Njangula Senior Member

  #12
  Jul 6, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu hiyo CWT inavyonikera we acha tu. Nadhani iwepo ile ya sekondari na primari.
   
 13. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #13
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,985
  Likes Received: 1,909
  Trophy Points: 280
  jamani naona hili la vyeti feki hapa sasa linapambwa san, labda kwa akili za darasa la kwanza tu je tz kuna idadi gani ya waalimu ngazi ya cheti? na fanya hivyo kwa diploma degree na hata masters. je katika hao wangapi wamegushi vyeti hivyo? Jamani ikumbukwe tu kwamba haya ya waalim kuwa na vyeti bandia inapata publicity kubwa kwasababu ndio field yenye watumish wengi na ambao siku zote wapo kulia shida tu. sidhani hata kama hawa wa vyeti feki wana weza kumzuia mwl wa degree ama dip asigome ama yeyote yule. pia ujue hata kama ancheti feki basi kosa ni la aliyemwajiri wala siyo la kwake kwani aliyemuajiri alipaswa athibitishe kama kweli vteti ni halali ama la.

  nia ya waalim kugoma iko wazi kabisa na hapa tunachoangalia ni maslah na mazingira mabaya ya kufanyia kazi, tuache habari ambazo hatuna evidence nazo. kweli waalim wmefoji vteti ukilinganisha na polisi au uuguzi? ama kwakua nyie mmezoea kwaonea na kuwaona kama mapoyoyo ilihali they made you to be who you are today?
   
 14. Msenyele

  Msenyele JF-Expert Member

  #14
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 332
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Serikari haijagundua bado kwamba walimu ndo kiungo pekee na ni chachu ya maendeleo kwani kila mmoja wetu lazima atakuwa amefundishwa na walimu mpaka hapo alipofikia. Kumekuwepo na hali fulani ya kudharauliwa walimu tangu enzi za mwalimu nyerere. Kinachotakiwa kufanyika ni walimu kuungana pamoja ili suala hili la kuongezwa mshahara lifanyike. Haiwezekani hata siku moja mwalimu wa degree walingane na certificate wa nursing hata katika hali ya kawaida ni ukichaa uliokomaa. Mimi naunga mkono hoja ya kugoma pasipo na kikomo mpaka kieleweke. LIWALO NA LIWE.
   
Loading...