Walimu ni kundi la watu Weledi Sana

fullcup

JF-Expert Member
Jun 21, 2016
806
2,182
Kaka mwalimu mwenzangu ndugu Mpwayungu Village nakuheshimu Sana na naheshimu mawazo yako.

Ndugu zanguni kati ya kundi la watu wenye heshima kubwa nchi hii ni walimu. Walimu tunaheshimika Sana najamii inayotuzunguka na ukikuta mwalimu hapati hiyo heshima basi ujue ameipoteza mwenyewe kwakujiingiza kwenye majanga.

Licha ya heshima hiyo Kuna Mambo tunatakiwa kuyaweka sawa. Baadhi ya mambo hayo ni kama vile;

1: Kutoshobokea makombo ya viongozi au wananchi
Walimu tumekua tukitia aibu yaani kama watoto. Akija kiongozi au wageni shuleni na kuandaliwa chakula walimu wote huwa tunakaa standby yaani kiongozi akiingia tu kwenye gari tunavamia venue na kumalizia vyakula na vinywaji na sometimes kuweka kwenye makopo na kupelekea watoto.

2: Kuondoa uchawa Kwa viongozi na watu wenye uwezo

Walimu tunajipendekeza Sana Kwa wakuu wa shule. Yaani baadhi ya shule mwalimu mkuu ni kama Rais yaani hakosei na hashauriki na anaamua anachotaka na ukizungumza jambo kumhusu linafika. Pia Kama Kuna mwalimu anakipato kidogo au mtu mtaani anakipato kidogo walimu wote watamnyenyekea na hakuna wa kumgusa hata akikosea sometimes hata mwalimu mkuu akiwa na Hali duni lazima atajipendekeza.

3: Kushoboka na matukio ya kiserikali na chama
Walimu ifike mahala tuachane na sijui sherehe za mwenge, ziara ya kiongozi gani, kusimamia sijui uchaguzi, sijui sensa tuwaachie vijana waliokosa ajira wajinafasi nazo. Walimu tunatia aibu unakuta tunarundikana kwenye saili na wanafunzi wetu wa miaka kadhaa au miaka ya nyuma tu kwenye saili. Hii inatupunguzia credit mtaani na heshima inapungua na kuongeza kudharaulika.

4: Adhabu na mahusiano na watoto
Walimu tuunganishe nguvu na kupaza sauti kwenye vikao vyetu Inapotikea mtu anamahusiano na mwanafunzi . Kesi hizi zinatuharibia uaminifu uliojengwa na waasisi wa fani hii tangu miaka na miaka. Adhabu za fimbo auangumi na kupelekea vifo au matatizo Kwa watoto tuachane nazo na tutafika mbali. Mtoto ambae hataki aondolewe Bora nibaki na watoto wawili wanaonisikiliza.

5: Matumizi ya Pombe yaliyopitiliza

Kuna walimu wanalewa Tena sometimes Pombe za kienyeji na wengine mpaka wanabebwa na wanakijiji. Yaani Hali Kama hizo tuziepuke na tule Pombe kiasi hii itatusaidia Sana kutunza jina letu.

6: Mikopo isiyo ya lazima
Jamani walimu tunakopa Sana. Sometimes Mambo mengine tuachane nayo. Tukope kununua vyakula na kuuguzia lakini mwalimu unakopa ujenge, ununue suti, ununue sim Kali, ununue redio sijui flat au umkoge sijui nani tuache. Kama ikishindikana basi tupunguze mikopo yaani Kuna wengine hata Raha ya mshahara hatuioni maana unaambulia ujumbe tu wa 'umepokea. Umelipa.

Mambo hayo tu yanafanya tuonekane wa hovyo tofauti na kada nyingine hasa Afya yenye wafanyakazi wengi Kama sisi.
 
Namba 2 imenikuta majuzi tu alikuja wazlri x katika shughuli maalum na wananchi na kuzindua mpango huo maalum,
ila nilitulia ofisini kiasi kwamba hakuna kiongozi wa kijani ametembelea around us.

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Hivi hizi threads za kipumbavu za kuwajadili Walimu zitaisha lini? Hivi kati ya Mwl. na Polisi (kwa mfano) au Mwalimu na TISS Agent nani anashobokea '3.Matukio ya Kiserikali na Chama'?

Mlishawang'ang'ania Walimu hata issue za wizi wa kura. Hivi mnajua hao niliowataja (bila kuwasahau wajeda wavaa mboga mboga) wanavyohusika na ufisadi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko hata huyo Mwalimu? Hii nchi pumbavu zenu...maana hamumjui adui yenu hasa.
 
Hivi hizi threads za kipumbavu za kuwajadili Walimu zitaisha lini? Hivi kati ya Mwl. na Polisi (kwa mfano) au Mwalimu na TISS Agent nani anashobokea '3.Matukio ya Kiserikali na Chama'?

Mlishawang'ang'ania Walimu hata issue za wizi wa kura. Hivi mnajua hao niliowataja (bila kuwasahau wajeda wavaa mboga mboga) wanavyohusika na ufisadi wa kura kwenye Uchaguzi Mkuu kuliko hata huyo Mwalimu? Hii nchi pumbavu zenu...maana hamumjui adui yenu hasa.
Walimu ni wapumbavu hilo lipo wazi
 
Back
Top Bottom