Walimu karibu wote uwezo mdogo

Mkuu kada gani inachukua ufaulu mkubwa kuliko zote tuanzie ngazi ya cheti kwanza
 
walimu ka kaizirege wote wana one?

je wote wamesoma udsm?

wote wametoka familia bora?
 
Reactions: cpt
ndugu mwalimu nakushukuru rasmi kwa kuthibitisha hoja ya mtoa mada!
 
Hawawezi kukiri na watatukana sana, lakini upo sahihi sana. Asilimia kubwa ya walimu wa zama hizi ni VILAZA na hawana wito. Hatuotei, tunao mitaani huku ni ndugu, jamaa na marafiki zetu.
Sometime ukikaa unasikia "fulani" naye kawa mwalimu hadi unashtuka. Inasikitisha. Wengi wanabebwa na hizi ajira za mafungu zisizo na interview.
 
bora tuliopiga education na tuna hella zetu za kutosha...ajira full..full
 
Reactions: cpt
Mkuu tuanzie ngazi ya cheti..ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko zote
Mkuu swali lako naweza kulijibu lakini nikawa siko realistic sana.
Mathalani katika kuhitimu kwangu kidato cha iv tuliofaulu kuanzia daraja laI-III wengi tuliendelea na kidato cha V na baadhi technical colleges km DIT,ATC,MTC etc kwa kipindi hicho.
Kwahiyo watu wote waliofaulu chini ya hapo wengi wao walienda ualimu(mpaka IV ya 28) kipindi hicho na wengine pengine walisomea kada mbalimbali kulingana na vigezo vya udahili kwa mujibu wa NACTE.
Sasa kwa muktadha huo, itoshe tu kusema kwamba wenye ufaulu hafifu ndo hao walienda kusomea ualimu na hatmae kuwa walimu.
Vivyo hivyo hata kwa wahitimu wa kidato cha VI.
Bila shaka umenielewa mkuu.
 
Bonge la logic
 
Nakubaliana na wewe 100%.Nisiloelewa ni kwa nini mambo yafanywe hivi,huku tukijua kwamba mwalimu wa hivyo ataleta kihiyo.Nadhani kuna conspiracy hapo.Kwa nini tusiwalipe vizuri vijana intelligent wakapenda ualimu ili hatimaye watuletee product nzuri.Again an obvious conspiracy.
 
Kada gani hapa nchini ambayo mtu aliyepata 3 hawezi kusomea...nitajie yoyote
Inategemea na chuo pia ushindani wa nafasi hiyo katika chuo hicho.
Chuo kama st joseph candidate aliyeopt kuchukua electronics qualifications zake zipo chini sana ukilinganisha na yule aliyepata admission UDSM.
 
Ndo maana umesema walimu wengi ni vilaza upstairs
 
Mkuu umetoa maelezo pasipo kunijibu swali..nimeuliza katika ngazi ya cheti ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko nyingine
 
hii ndio tanzania bana, afu tunatokwa povu escrow, epa, sijui nini!
 
Inategemea na chuo pia ushindani wa nafasi hiyo katika chuo hicho.
Chuo kama st joseph candidate aliyeopt kuchukua electronics qualifications zake zipo chini sana ukilinganisha na yule aliyepata admission UDSM.
Owk kwa maelezo yako kumbe kuna mtu aliyesoma pcb anaweza kwenda kusoma udaktari kampala university or hubert kairuki wakati ufaulu wake ni mdogo kuliko mtu aliyesoma pcb na akaenda science education university of dar es salaam...sasa hapo kati ya huyo daktari na mwalimu nani mwenye ufaulu na uwezo mdogo????
 
Mkuu umetoa maelezo pasipo kunijibu swali..nimeuliza katika ngazi ya cheti ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko nyingine
Unaongelea failure kwa failure mkuu...hata kama wanachukua point 27 ualimu still ni four...halafu upande wangu mwanafunzi yeyote ambaye kamaliza four akapiga four akakimbilia chuo huwa namuita Kilaza...ninaowaongelea ni wale wamemaliza form six wakaingia chuo wanaoenda ualimu upstairs ni wabovu...so tambua hao unaowaongelea wote uwezo mdogo...ni sawa na aliyemaliza form six akafeli na kupata principal moja akakimbilia diploma, so tambua point asilimia kubwa waalimu ni wabovu upstairs
 
Kumbe kada zote kwa ngazi ya cheti ni failure sasa kwanini umemuongelea mwalimu tu hujaongelea watu wakada nyingine huoni hapo unaonyesha tu kuwa unachuki zako binafsi na kada ya ualimu
 
wewe ni mwongo mimi ni mwl wa BIO/CHEM nilisoma PCB na nikapata div ii, nikasoma chuo Bsc Edu. nikiwa na teaching subjects 2, na nikasoma Msc Env sc. na napeta kwa kufundisha watoto
 
Kumbe kada zote kwa ngazi ya cheti ni failure sasa kwanini umemuongelea mwalimu tu hujaongelea watu wakada nyingine huoni hapo unaonyesha tu kuwa unachuki zako binafsi na kada ya ualimu
Kama ulinifuatilia vyema nilitoa sababu kadhaa za wengi kukimbilia ualimu...halafu pili wengi wanaomaliza kidato cha nne na kufeli wengi wabovu kichwani, tukubaliane hakuna kufeli kwa bahati mbaya au kufaulu kwa kubahatisha...hivyo basi hao wakishafeli ndio linakuja swala la familia kama lina uwezo wa kusimamia show mpaka amalize chuo kama hawawezi vilaza hawa hukimbilia udhamini wa wizara ya elimu na kupangiwa vyuo na hatimaye vilaza hawa humaliza na kusubiri kupangiwa shule kama wanavyosubiria kupangiwa wa sasa....
Hebu nijuze swala moja hivi iwapo mpo wawili mnasoma HKL halafu matokeo kutoka umefaulu na kupiga one ya tano na mwenzako akapiga three suppose ni 14 unadhani wewe utaenda kusoma education chuo?? Kama ni ndio basi linakuja swala la familia kwamba ukitaka kusoma law hutapata mkopo hivyo itakulazimu kusoma ualimu ila yule wa three hana option kwakuwa amefeli...kwahiyo tukubaliane waalimu wengi wabovu upstairs
 
Hivi kwa nini walimu wengi wana jishtukia sana ikisemwa fani yao kuliko fani nyingine,na wanalalamika sana mfano jeshi wengi wanaenda ambao hawakufaulu sana kuliko hata hao walimu lakini huwezi kukuta wanalalamika eti isingekua sisi kuilinda nchi na kuwa na amani wewe usingesoma na kuwa na kazi flani unakuta mtu anapiga education bachelor ukimuuliza unasoma nini anakwambia nazuga zuga na education si unajua ualimu ni daraja tu ya kupitia!!!!!huwa inanishangaza sana sijui nini kimewafanya wasijiamini hivi
 
Mkuu umetoa maelezo pasipo kunijibu swali..nimeuliza katika ngazi ya cheti ni kada gani inayochukua ufaulu mkubwa kuliko nyingine
Zipo nyingi tu mkuu. Mathalani kada ya sheria na teknologia ngazi ya cheti min. entry qualifications ni kubwa ukilinganisha na ualimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…