Walichotuachia Wakoloni Tumekitunzaje?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Nikiwa najiandaa kwenda kula Pasaka nje ya mji nimeona niache swali hapa ili hata nikiwa nje ya kamji kangu kaitwacho Cyber Village ntapata nafasi ya kuona kwamba huku tukiila Pasaka tunaweza kuwepo hapa jamvini JF kubadilishana mawazo.

Sasa leo nina swali kuhusu shirika la reli ya kati Tanzania.

Sote twajua kwamba njia za reli hii zilijengwa na watanzania wakisimamiwa na wakoloni na ilikuwa ni katika kuhakikisha malighafi, na mazao vinasafirishwa katika muda muwafaka bila kusahau watu.

Lakini pia ujenzi wa reli yoyote ile unaweza kuleta manufaa makubwa kwa chi husika.

Baadhi ya manufaa hayo ni pamoja na urahisishaji wa usafiri kwa watu ambao huweza kusafiri kutoka kona moja ya nchi hadi ingine.

Kisiasa, watu huweza kupata mwanga wa nini kinaendelea nchini mwake na pia kuwa na uhakika wa kupata habari kupitia magazeti ambayo huweza kusafirishwa na kufika kila mahala.

Kiuchumi ndio kabisa watu wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa ufanisi kupitia miji mbalimbali na shughuli za kibenki kuweza kusamba kila kona ya nchi kutoka mijini hadi vijijini.

Pia katika hili la uchumi ndio unaweza kuona kwamba sehemu kama Dodoma au Singida inaweza kufanzwa kama ndio kituo kikubwa (trading centre) ya Tanzania ambapo watu kutoka mikoa yote nchini huweza kukutana na kufanza mikakati mbalimbali ya biashara.

Kwa hio reli tu ni moja ya njia kuu za kukuza uchumi wa Tanzania.

Sasa baada ya miaka 47 sijui, ya uhuru bado watanzania tumeshindwa kusimamia shughuli za reli nchi mwetu ambapo tumefikia kuwa na mizozo ya watumishi wake na pia kufikia kuuza moja ya njia kuu za uchumi wa nchi.

Mimi katika maisha yangu hapa Cyber Village huwa natumia sana usafiri wa reli na huwa najiuliza kila siku kwamba sisi tumeshindwa nini kusimamia njia hii.

Kwa mfano nchi ya Uingereza bado serikali inamiliki shirika la reli nchini humo. Walichofanza ni kutoa leseni kwa makampuni mbalimbali kama Virgin,North Great Western na zingine, hutumia njia za reli na kulipa kodi tu na kampuni ingine itwayo Network Rail ndio yenye jukumu la kuhakikisha njia za reli ziko imara na salama kila kukicha.

Kwa hio hapa hizi kampuni hupata mapato yake kupitia mtaji wa kwanza ambao hupewa na serikali kuanzisha biashara hio na nauli mbalimbali kutoka kwa watumiaji wa huduma hio.

Hapa moja kwa moja serikali inakuwa imetoa mwanya kwa wananchi kupata ajira, bidhaa kusafirishwa kwa ufanisi kama barua na kadhalika kwa hio sula la ajira linakuwa limetatuliwa kwani watu watakuwa wanajenga, wanaendesha na kusimamia huduma za reli.

Faida zingine ni pamoja na wabunge kuweza kusafiri kwa kutumia njia ya reli na kuokoa fwedha kibao ambazo zinapotezwa kwa kununua magari yenye gharama kubwa.

Sasa je tumeitumia vipi njia hii muhimu kwa uchumi wa Tanzania?

Kwa wale ambao wangependa kujiendeleza kwa kusoma zaidi masuala ya uhandisi wa reli mnaweza kubarizi link hio hapo chini.

http://www.railway.bham.ac.uk/index.htm

Kheri ya Pasaka.
 
Hii habari ya shirika la Reli inaumiza sana mioyo ya kila anyejali maendeleo ya Taifa letu.Ikumbukwe kuna mahali huwezi kufika bila kupanda Treni au ndege,hilo la Ndege siwezi hata kulizungumzia maana labda ni chini ya asilimia 5 ya watanzania wenye uwezo wa kuzipanda.Jamani haya ndiyo maisha bora kwa watanzania? au hawa watanzania hatuwafahamu nini? ni kina nani hasa? wapanda Treni ni watanzania kweli? Ah jamani Serikali yetu sijui inataka nini,Reli angalau ingebinafsishwa kwa wananchi kwa kuchanga kidogo kidogo tungeelewa kuliko kuwapa 'strangers' waliokuja kuchuma.Ni aibu ukitoka nje ya nchi kujiita mtanzania maana yatendekayo nchini mwetu ni zaidi ya aibu.

Miaka ya 47 reli ilikua inafanya kazi vizuri badala ya kuboresha miaka inavyokwenda mbele ndo tunarudi nyuma.Hakuna adui mwingine ila ni UFISADI tu. Mpaka hapo viongozi wetu watakapo weka pembeni maslahi yao na wapambe wao na ndugu zao ndipo nchi hii itaendelea.Kwani Reli ni mfano tu angalia viwanda vilivyokufa na kubinafsishwa kwa watu wa nje kwa bei chee.Maisha bora yatapatikana kweli?
 
Umewahi kuiona bajeti ya shirika la reli? tena siyo reli tu, bali mashirika karibu yote ya Serikali. Hakuna O&M (operation and maintanance), hakuna fidia au bima ya uchakavu wa mali (depreciation). Hata wewe baba yako akikupatia nyumba kubwa let say Hoteli & guest house kama huta kuwa na vitu nilivyovitaja hapo juu kwenye bajeti lazima utabinafsisha baada ya miaka kadhaa.

Dhana yenyewe iko hivi: leo kinavunyika kisehemu kimoja unaacha, kesho kingine nk. utakapotaka kutengeza sasa, gharama yake inakuwa kubwa kuliko uwezo.

Tuipe nafasi kampuni iliyowekeza labda hawafanani na city water, netgroup solution at el..
 
Back
Top Bottom