Walichomfanyia jamaa yangu. Anatokwa na machozi kila anapokumbuka

Kama huna pesa,achana na chemchemu za maji! Kule Kunduchi mtongani, karibu na kanisa la KKKT Mtongani,kwa juu upande wa kulia,ukiwa unaangalia kusini! Waliojenga maeneo yale,hua wanapata shida sana,unaweza kua umekaa sebuleni,unashangaa maji yanatiririka!
Duuh Kisa wanataka kukaa ushuani?
 
Jamaa yangu tupo naye kazini kitambo sana. Si haba vijicent vipo. Shida kubwa ya jamaa ni ubabe na unyanyasaji sababu ya vijicent.

HuWa namwambia asiwe na lugha za kibabe, dharau na unyanyasaji kwa watu wa kipato cha chini. Haelewi.

Anajenga nyumba. Ashafukuza sana mafundi bila kuwalipa na matusi mengi akitishia kuwaweka ndani n.k ni jambo la kawaida kumsikia akiwaambia umaskini wenu na kukosa akili ndo kumewafanya mchague hii kazi.

Basi amejenga nyumba yake akiwalalia sana mafundi ...sana yaani kumbe nao wanajua pa kumlalia.

Leo tumeenda akakague mifumo ya maji baada ya kuunganishwa mabomba...aiseee.... Alikuwa kila akifungua bomba maji yanatokea ukutani...kumbe katika hali ya kumkomoa mafundi walikuwa wanaweka mabomba hawafikishi mwisho.

Kwa hiyo ameenda kufungua maji kwenye koki kuu...kuingia ndani anakuta kuta zinatiririsha maji tu...

Hivyo anapaswa abomoe afunge mabomba upya...Kuta zinatiririsha maji ile mbaya. Mimi kwenda gusa zaidi zile kuta aisee ....hazifai.

Yaani ukipata muda ukaanza ukuna au tekenya ukuta mchanga unamiminika chini hadi ukuta unatoboka....

Ile nyumba ina maeneo ukikaa tu kama upo idle kwa kidole tu anza kufanya kama unaukuna ukuta au fanya kama una utekenya...ukuta unacheka kinyama....

Mafundi haijulikani wanakaa wapi ila nao wameshalipiza wameondoka zao.ukijua ya mbele wenzio wanajua ya nyuma.
Anatokwa na machozi atakua anaigiza
 
Jamaa yangu tupo naye kazini kitambo sana. Si haba vijicent vipo. Shida kubwa ya jamaa ni ubabe na unyanyasaji sababu ya vijicent.

HuWa namwambia asiwe na lugha za kibabe, dharau na unyanyasaji kwa watu wa kipato cha chini. Haelewi.



Mafundi haijulikani wanakaa wapi ila nao wameshalipiza wameondoka zao.ukijua ya mbele wenzio wanajua ya nyuma.

Safi sana...
 
Kitaalam plamber ni mtu mwingine na fundi kujenga ni mwingine sasa hapo ilikuaje fundi huyo huyo mmoja afanye yote hayo huyo jamaa pia hajasoma km ni hvyo
Hivi hawa mafundi wenyewe huwa hawafanyi kile ambacho huwa kinachitwa na vijana wa kisasa "kolabo"
 
Mnawadharau sana mafundi ujenzi, mnasahau kuwa ukiacha madaktari mafundi ujenzi ndio watu mhimu sana ktk future zenu.
Kweli kabisa.

Sisi tunaitwa Madrassatul Abraar, ni wadau wa ujenzi wa kisasa, tuna kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ujenzi za kisasa na tunahitaji mafundi ujenzi, kuanzia wa kiwandani kwenye uzalishaji mpaka kwenye ufundi wenyewe. Tunahitaji mafundi wa viwango tofauti, kuanzia wanaotaka kujifundisha ujenzi mpaka wale wazoefu wa kusimamia kazi. Tupo very strict kwa ubora. Kama unapenda kufanya kazi na watu wenye kujali ubora wa kazi za ufundi, nidhamu za kazi za ufundi na mwenye kujali miiko ya kazi za ufundi na sio uwingi wa kazi basi wasiliana nasi.

Pia tupo tayari kuongea na vikundi au makampuni na madalali wa mafundi ujenzi namna ya kushirikiana.

Kwa maelezo zaidi fika tuonane ana kwa ana au tuma whatsapp 0625249605. Tupo, Mtaa wa Vitendo, Kata ya Misugusugu, Kibaha, Pwani. Tanzania.
 
Hivi hawa mafundi wenyewe huwa hawafanyi kile ambacho huwa kinachitwa na vijana wa kisasa "kolabo"
Kama unamnyanyasa fundi mwashi utashindwaje kumpelekesha plumber? Wote wanakuona Foo tu na wakiform alliance wanakuangamiza na hela yako wanaila.

Siku zote fanya kazi na watu ukiwa unawathamini. We all got families to feed! Sasa ukijifanya mjuaji sana ndio balaa litakapoanzia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom