Walichofanya Ethiopia kutengeneza Megawatt 5,000 za umeme; Je, Watanzania tunathubutu?

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,320
Siku si nyingi Ethiopia ilikamilisha ujenzi wa bwawa la maji linalozalisha megawatt 5,000 za umeme. Wakiunganisha na mabwawa mwngine waliyokuwa nayo sasa wanakaribia megawatt 1,000 za umeme...

Ujenzi wa bwawa hilo uliogarimu zaidi ya $ 3bn, ulichangiwa kwa karibia asilimia 30 na wafanyakazi wa serikali, na wa binafsi ambapo kila mwananchi mwenye mshahara nchini humo alitakiwa kuchangia mshahara wake wa mwezi mmoja. Kwa hiyo walichukua mshahara wa mfanyakazi, wakagawa kwa 12, then kiasi hicho kikawa kinakatwa katika mshahara kwa mwaka mmoja.

Fedha nyingine walipata kutoka mikopo ya mabenk ya nje...

Kwa sasa wanapata mapato makubwa kwa kuuza umeme nje ya nchi wakianza na Djibout, lakini zipo nchi nyingi zimshaaply kuuziwa umeme ikiwemo Spain!

Je, leo Kikwete akisema anachukua mshahara wa mwezi mmoja wa kila mfanyakazi ajenge stiegler's gorge, tutakuwa tayari?
 
Mkuu hii ndio naita planning and forward thinking mambo ambayo viongozi na wataalamu wetu wanakosa..

Sio hao tu hata Gadaffi alimanage kutengeneza the Biggest Man Made River ambayo iliwasaidia wananchi wake katika ukulima na mahitaji mengine.., sisi hata kutumia kile kilichopo hatuwezi ni kugawa tu kila kitu na kuuza (eti uwekezaje) yaani kila mtu mpaka wana siasa wamekuwa wafanyabiashara wanashindana kuuza nchi ili tu wapate 10%
 
Hao jamaa si umeme tu hata miundo mbinu ya barabara zao usipime, wanazo hadi fly over sisi tunaadhimisha miaka hamsini ya uhuru bado tunazungumzia umeme wa magumashi ovyo kabisa.
 
Siku si nyingi Ethiopia ilikamilisha ujenzi wa bwawa la maji linalozalisha megawatt 5,000 za umeme. Wakiunganisha na mabwawa mwngine waliyokuwa nayo sasa wanakaribia megawatt 1,000 za umeme...

Ujenzi wa bwawa hilo uliogarimu zaidi ya $ 3bn, ulichangiwa kwa karibia asilimia 30 na wafanyakazi wa serikali, na wa binafsi ambapo kila mwananchi mwenye mshahara nchini humo alitakiwa kuchangia mshahara wake wa mwezi mmoja. Kwa hiyo walichukua mshahara wa mfanyakazi, wakagawa kwa 12, then kiasi hicho kikawa kinakatwa katika mshahara kwa mwaka mmoja.

Fedha nyingine walipata kutoka mikopo ya mabenk ya nje...

Kwa sasa wanapata mapato makubwa kwa kuuza umeme nje ya nchi wakianza na Djibout, lakini zipo nchi nyingi zimshaaply kuuziwa umeme ikiwemo Spain!

Je, leo Kikwete akisema anachukua mshahara wa mwezi mmoja wa kila mfanyakazi ajenge stiegler's gorge, tutakuwa tayari?

ethiopia hawajazoea kupiga porojo ni watu wa vitendo halafu ni wazalendo wa nchi yao tofauti na tanzania kinachokwamisha maendeleo ni uongo umekuwa mwingi kuliko ukweli halafu hakuna uzalendo nchi ya wadanganyika
 
Wewe unayeshauri Tanzania wafanye hivi hata kama una nia nzuri, umewasahau wezi wetu wanaoitwa waheshimiwa wasiostahili hata heshima. Bahati mbaya kwa nchi yetu, kila kinachofanyika, watawala hawaangalii mbele zaidi ya 10%. Wenzetu wa Ethiopia walitumia vichwa badala ya masaburi. Kwa madini na raslimali nyingine tulizo nazo, hatuhitaji hata kukata watu mishahara. Ukitaka kujua nimaanishacho angalia wahindi wanavyokuja wakiwa maskini na kuondoka wakiwa mabilionea huku wakiacha maelfu ya maponjoro wengine nyuma. Tatizo letu si wapi tupate pesa bali nani mwenye akili timamu na udhu kuzismamia. Kwa sasa nchi yetu haina tofauti na taifa la mapanya kwani kila mtu anaguguna atiacho jicho. Hata wananchi maskini pamoja na umaskini wao hawauchukii ufisadi. Wanachotamani ni kupata nafasi nao waibe. Huo ndiyo ugonjwa wa taifa letu lenye kutegemea matapeli kama jambazi shehe yahaya au jambazi la Loliondo.
 
Sisi megawat zetu ziko kwenye makablasha ya Ngereja,akitaka kutufariji anayatoa na kutusomea halafu anayarudisha tena.
 
Siku si nyingi Ethiopia ilikamilisha ujenzi wa bwawa la maji linalozalisha megawatt 5,000 za umeme. Wakiunganisha na mabwawa mwngine waliyokuwa nayo sasa wanakaribia megawatt 1,000 za umeme... mkuu hapa unamaananisha nini. Pls weka takwimu zako vizuri ili tukuelewe.
 
hao jamaa si umeme tu hata miundo mbinu ya barabara zao usipime, wanazo hadi fly over sisi tunaadhimisha miaka hamsini ya uhuru bado tunazungumzia umeme wa magumashi ovyo kabisa.

nilikuwa hapo ethiopia zenawi kile kichwa bwana zile fly over zilikuwa zinapita kwenye makazi haswa slams yeye akawajengea magolofa halafu akawahamisha jamaa hawana mpango na wapinzani wa nini jamaa ana deliver, yani sishangai vile mod anavyo sema jamaa anavile anajalibu kufanya vitu tofauti na hawa wa kwetu ni mtu wa ku -take risk vilevile huwa ha-commit sucide
 
Watz hatujafikia hatua ya kukatana mishahara. Waethiopia wana resources chache sana kulinganisha na TZ. Sisi hapa tz pesa ipo ila mchwa imezidi
 
Hao jamaa si umeme tu hata miundo mbinu ya barabara zao usipime, wanazo hadi fly over sisi tunaadhimisha miaka hamsini ya uhuru bado tunazungumzia umeme wa magumashi ovyo kabisa.

Nyie hile sio nchi! Amshangai kila siku tunawakamata Mbeya, songea na Mtwara wakijaribu kukimbilia SAUZI? JIULIZENI
 
Nyie hile sio nchi! Amshangai kila siku tunawakamata Mbeya, songea na Mtwara wakijaribu kukimbilia SAUZI? JIULIZENI
Hao ni wale wanaotafuta maisha bora haraka,je kuna mtu aliyerizika na maisha yake popote pale.
 
Nimeipenda sana hii mkuu. Tatizo letu sisi kushindwa inabidi uende Dodoma na uongee na maofisa wa Bunge wakupatie hansard moja ambapo mbunge mmoja (pia sikumbuki ni wa wapi) aliwahi kusema kuwa "vichwa vyetu vina matatizo na itabidi huko mbeleni wafukue mafuvu yetu kuangalia tulikuwa binadamu wa aina gani"! Hilo tatizo naona ndio limezidi kwa sasa.
Lakini hapo (kwenye red), hivi hizo US $3bn si ni karibia na Trilion 3!!???
Basi kama ni hivo hata nasi tunaweza kujaribu kujenga kwa kuwa funded na mtu mmoja tu au waili ....anyway, ni mtamo tu!
Siku si nyingi Ethiopia ilikamilisha ujenzi wa bwawa la maji linalozalisha megawatt 5,000 za umeme. Wakiunganisha na mabwawa mwngine waliyokuwa nayo sasa wanakaribia megawatt 1,000 za umeme...

Ujenzi wa bwawa hilo uliogarimu zaidi ya $ 3bn, ulichangiwa kwa karibia asilimia 30 na wafanyakazi wa serikali, na wa binafsi ambapo kila mwananchi mwenye mshahara nchini humo alitakiwa kuchangia mshahara wake wa mwezi mmoja. Kwa hiyo walichukua mshahara wa mfanyakazi, wakagawa kwa 12, then kiasi hicho kikawa kinakatwa katika mshahara kwa mwaka mmoja.

Fedha nyingine walipata kutoka mikopo ya mabenk ya nje...

Kwa sasa wanapata mapato makubwa kwa kuuza umeme nje ya nchi wakianza na Djibout, lakini zipo nchi nyingi zimshaaply kuuziwa umeme ikiwemo Spain!

Je, leo Kikwete akisema anachukua mshahara wa mwezi mmoja wa kila mfanyakazi ajenge stiegler's gorge, tutakuwa tayari?
 
[njaa kali sana ethiopia, wanaoneana na wana matabaka pia huyo zenawi ni mshenzi wa kutupwa good point jamaa wana kubalika na mataifa ya nje wanasaidiwa sana na wachina etc ]Hao ni wale wanaotafuta maisha bora haraka,je kuna mtu aliyerizika na maisha yake popote pale.[/QUOTE]
 
Nyie hile sio nchi! Amshangai kila siku tunawakamata Mbeya, songea na Mtwara wakijaribu kukimbilia SAUZI? JIULIZENI

Pamoja na kujitahidi lakini ile nchi iko nyuma sana ukifananisha na Tz. Wana population ya 91m, mshahara wa profesor kwa mfano ni dola 300, ikilinganishwa na dola 3000 Tz, gharama za maisha ziko juu, kwa mfano kilo moja ya mchele ni 2 dolars ukilinganisha na 0.8 hapa kwetu, nyama ni 5 dollars ukilinganisha na 3 dollars hapa kwetu. Hawana demokrasia (hakuna vyama vya upinzani), na ukichalenji serikali unathibitiwa saa hiyo hiyo ikiwamo kupoteza kazi kama ni mwajiriwa. Nchi inatawaliwa kikabila na sasa wanaotawala wanatokea katika kabila ndogo sana lakini kwa kuwa zaidi ya 70% ya mapato inakwenda kwenye ulinzi, sio rahisi kumwondoa Zenawi. Ndio maaana wanatoroka kwao...
 
Viongozi wetu hawathubutu kama hakuna 10% kwani wako kimasilahi zaidi kuliko jututumikia
 
tatizo la TZ ni utekelezaji wa maazimio wafanyakazi wanakatwa
  • 18% - income tax
  • 2% - CWT
  • 2% - Bima ya afya
  • etc
  • Mikopo ( overdraft)
 
Kuchangia si tatizo nafikiri kila Mtanzania anaweza kuchangia mbona kipindi cha vita ya Kagera watu walichangia vitu mbalimbali?! Hapa mimi ninacho kiona ni kuwa hatuwaamini tena viongozi wetu. Kwasababu tunaweza tukachangia afu watu ndio wakapata mtaji wa kutokea..Ikawa deal tena na tatizo la Umeme likabaki palepale.
 
Back
Top Bottom