TANESCO yataja miradi itakayowezesha Tanzania kufikisha Megawatt 5,000 za Umeme waka 2025

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,433
49,102
Maharage Chande Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco ameitaja miradi itakayowezesha Tanesco kufikisha Megawatt 5,000 za Umeme Mwaka 2025.

Alikuwa akizungumza na Kamati ya Bunge.

---

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Maharage Chande ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa miradi ya kimkakati inayoendelea kutekelezwa italisaidia Shirika la Umeme wa Tanzania (TANESCO) kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 5,000 za umeme ifikapo Juni 2025.

Ameyasema hayo wakati akiwasilisha mipango mkakati ya Shirika hilo wakati wa semina iliyotolewa kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dunstan Kitandula (Mbunge) siku ya Jumamosi, tarehe 25 Machi, 2023 jijini Dodoma.

"Uzalishaji una miradi ya muda mfupi yaani kutoka leo hadi 2025 na miradi ya muda mrefu ya kutoka 2025 mpaka 2035. Kama tunavyoona Julai 2022 tumeweza kuingiza mradi wa Kikagati Murongo wenye megawati 3.7. Tunategemea kwamba mradi wa Kinyerezi I Extension utaisha tarehe 20 Aprili 2023. Halafu tunategemea mwezi wa nne mradi wa Rusumo wa megawati 26.67 nao utakamilika; kwa hiyo kwa mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 tunategemea kuwa na jumla ya megawati 1,913 kutoka jumla ya megawati 1,822. Na kwa mwakani, tunategemea mnamo mwezi Januari mradi wa project mawe utakaozalisha megawati 150 za umeme kwa kutumia gesi utaingia. Pia mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) tunategemea utaanza kutupatia megawati 470 za umeme ifikapo Juni 2024 na ndani ya miaka mitatu hadi minne tutakuwa na umeme wa kutosha, kwa hiyo tunategemea mwakani tutamaliza megawati 2,538. Na hapa bado hatujaweka zile megawati 200 za umeme kutoka Ethiopia kupitia Kenya" alisema Bw. Chande.

Bw. Chande aliendelea kufafanua kwa kusema, "Tutamaliza na megawati 5,013 na miradi ndiyo hii Solar Kishapu megawati 50, Masdar megawati 210, Total Energy wa jua megawati 100, Ubungo Combined Circle megawati 70, halafu Mwalimu Nyerere megawati 470 mara mbili mwezi Oktoba 2024 na Machi 2025, Project Mwamba (Gas to Power) megawati 300. Halafu Kishapu tutaitanua na kuongeza megawati 100 halafu tunategemea Juni 2025 tutafika megawati 5,000, alihitimisha Bw. Chande.


 
Katika lengo la kufikia uzalishaji wa umeme wa megawatt 5,000 by 2025,Tanzania itanunua Umeme wa megawatt 200 kutoka Ethiopia.

MyTake

Kuna haja gani ya kununua Umeme Kutoka Tanesco badala ya kuendeleza Vyanzo Vyetu lukuki?

 
Tunangojea matunda yake uenda nchi ikawa na uhakika wa umeme kwa maendeleo yake, sema Maharage anazingua Jambo la kuthamini wasomi waliomaliza masomo tangu 2021 hajawapatia haki Yao ya kupandishwa licha ya kupewa ruhusa ya kwenda masomoni.
Akitoka hapo ahamie kwenye Mifumo ya usambazaji kwani nayo haiko katika hali nzuri Kwa sasa.
 
Katika lengo la kufikia uzalishaji wa umeme wa megawatt 5,000 by 2025,Tanzania itanunua Umeme wa megawatt 200 kutoka Ethiopia.

MyTake

Kuna haja gani ya kununua Umeme Kutoka Tanesco badala ya kuendeleza Vyanzo Vyetu lukuki?


Hawa watu hawaeleweki mara tutawauzia south africa umeme, halafu then sisi tunaenda kununua ethiopia. Hivi hii nchi watu wamechanganyikiwa au vipi
 
Back
Top Bottom