Wali kupika kwa gesi, unaweza kukausha?

Kaka kama una jirani mwambie akusaidie kwa leo but kwa ufupi ufundi wa kupikia jiko la gesi hasa yale yenge mtungi ni utaalamu wa kucheza na kiwango cha moto.

Huwa ninapikia gesi na njia ninayoitumia ni kufunikia kwa mfuko ili ule mvuke usitoke uivishe wali taratiib.
 
Wana jamii naomba maujuzi ya kupika wali kwa gesi hadi kuukausha kwake.

1. Chemsha maji.
2. Weka kwenye thermos.
3. Andaa mchele, uoshe.
4. Weka kwa hayo maji.
5. Maji yazidi nchi moja juu ya mchele.
6. Uache uchemka.
7. Ugeuze taratibu.
8. Kama ulipima maji vizuri utakuwa unakaribia kuiva, kama bado ongeza ya moto ila kidogo, yapita mpaka chini.
9. PUNGUZA jiko sana.

Kama wewe ni mtu wa nazi weka kabla ya namba 7.
 
Wana jamii naomba maujuzi ya kupika wali kwa gesi hadi kuukausha kwake.

Unapoanza kupika wali wako(Ukishaweka maji) weka moto wa kawaida tuu utakaoufanya wali wako utokote vizuri, Ukiona maji yamepungua punguza uweke moto mdogo sana ili kuukausha wali wako.

Sometimes ninapokuwa napika nipo makini wali haung’ang’anii kabisaa
 
Hapana. nimeanza kutumia gesi kupikia wali toka Nipo chuo , just usimtumie Moto mwingi au tafuta dem akupikie .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom