Walemavu kupanda mlima kilimanjaro

Steven Sambali

JF-Expert Member
Jul 31, 2008
352
170
WanaJamii,
Kuna watalii wasio wa kawaida na kwa sasa niandikavyo ni kuwa wapo tayari Tanzania. Wapanda mlima hao walifikia Kenya na huko wakapokelewa na makamu wa rais wa Kenya. Leo jioni kutokana na News ni kuwa tayari wameshafika Tanzania na wamefikia Arusha. Wameshangazwa na baridi ya pale kwani wao wanafikiri Africa ni Sahara tu. Safari yao imeandaliwa na Mama mmoja ambaye ni Actor aitwaye Anna Dymna. Lengo la safari ni kuja Tanzania na kupanda mlima Kilimanjaro.
Nisingeandika hii habari kama si kwamba, wapandaji wote ni vilema. Wengine hawana macho (Vipofu), wengine hawana mikono na wengine miguu. Katika hawa kuna bwana mdogo mmoja aitwaye Jan Mela ambaye na yeye ni kivutio kikubwa. Alikatwa mkono mmoja baada ya kuwa amenaswa na umeme. Pamoja na ulemavu huo, alijitahidi na kwenda na mwisho kufika kwenye POLE zote yaani North Pole na South Pole. Baridi la huko kwa kweli latisha.
Naandika ili kama kuna wahusika basi wachangamkie hili tukio kwani ni tangazo kubwa sana la utalii kwa Tanzania. Waandishi wa habari na wizara husika fuatilieni na muone twaweza watumiaje hawa vilema wapandao Kilimanjaro yetu. Mungu Ibariki Tanzania.

Kwa watao taka maelezo zaidi basi angalieni kurasa hizi. Ila zimeandikwa Kipolishi na itabidi mjaribu kutafasiri kwa kutumia Google.

FOTO

Wahusika wote wanaonekana hapa pamoja na maelezo yao kwa ufupi.

Kilimandżaro 2008 – Mimo Wszystko - Uczestnicy
 
Its amazing what people can do regardless their dissabilities, we should always thank God for everything; including a nice day.
 
Its amazing what people can do regardless their dissabilities, we should always thank God for everything; including a nice day.

Tonga,
Ukiangalia katika hao, huyu bwana mdogo Jan Mela (John), hizi safari za kwenda North na South Pole zilimfanya awe maarufu sana na kumpa kujiamini katika maisha. Ulemavu wake sasa anaona ni kama faida. Ni sawa na wale wanaooenda kwenye michezo ya Olympic, wakirudi huwa wamebadilika sana ki-akili. Katika hao, yule kipofu watu walimuuliza kabla hajaondoka kuwa sasa na wewe kipofu kwa nini wataka kwenda kupanda mlima Kilimanjaro wakati huoni? Akasema kuwa tatizo siyo kuona ila kusikia sauti za huko, hali ya hela ya huko, kuvuta pumzi kwenye paa la Africa na kuisikia mwilini baridi ya huko. Naona ile kufika tu Africa kwake ilikuwa ni furaha kubwa sana. Huyo mama Anna Dymna anasema watakwenda wote na kurudi wote. Mmoja wao akikwama kwenda juu zaidi basi ndiyo utakuwa mwisho wa kupanda mlima.
Katika maisha nimejifunza kitu kimoja. Huwa najitahidi nisilaani kwa nini tukio fulani limenikuta. Maana siku zinavyokwenda huwa ninaanza kumshuru Mungu kwa kunisababishia tukio hilo kwani aliniokoa kwa janga fulani. Yep, tumshukuru Mungu kwa kila jambo, liwe baya au zuri, Amen.
 
Back
Top Bottom