Wale wapenzi wa movie pitia hapa.

povour3

Member
Dec 11, 2019
5
3
Kama umewahi kuona movie hii taja jina la mtu huyu na kueleza kidgo kwann unamkubali au kutomkubali
Jack_Sparrow_In_Pirates_of_the_Caribbean-_At_World's_End.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Not Jack Sparrow, its Captain Jack Sparrow.
Unforgetable
Hahaa! CAPTAIN Jack Sparrow kwenye filamu ya Pirates of The Carribean. Nakumbuka kwenye filamu ya kwanza watu walivochoka na janja janja zake kisha wakaamua kumuacha afe kwenye kisiwa, ndani kabisa baharini. Kisiwa ambacho hakikuwa na watu wengine. Kumbe kwenye kisiwa hicho alikuwa na maficho yake ambapo alikuwa amefukia mvinyo kwa wingi. Sparrow akaanza kulewa kupindukia, party kila siku, akijiburudisha na kujiongelesha kama chizi. Akiwa pekee yake kwenye kisiwa na wala hakuwa na stress za atakavojiokoa. Kwa bahati nzuri meli nyingine ikapita kwa umbali na ikamuokoa. Kilichofurahisha ni walipopigwa na butwaa baada ya kumuona amerudi kitaa. Wakawa wanamuuliza alifanikiwa vipi kutoka kwenye kisiwa kile. Akawatisha kwa kuwadanganya kwamba alikata nywele zake ndefu kisha akazitumia kutengeneza boti kwa kufunganisha magamba ya kasa ambao aliwawinda baharini. :D
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom