Wale wanaoamini uchawi, nawaombeni mje mthibitishe

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,196
Reaction score
1,846
Habari zenu Wana-jamiiforum?

Moja kwa moja kwenye mada, kuna minong'ono mbalimbali kuwa kuna nguvu fulani fulani zinazoweza kubadilisha hali ya kitu, kuleta maafa, kuleta bahati, au kuamua muafaka wa maisha ya wanadamu.

Binafsi mpaka nafikia huu sijawahi kushuhudia nguvu hizo.

Sasa naomba wale wanaoamini nguvu hizi wanithibitishie .

NB: Nipo tayari kutoa ushirikiano kwa atakayekuwa tayari kuthibitisha stori hizi.
 
Usitusumbue. Kama upo Dar mtafute huyu mdau hapa chini mthibitishiane huko halafu urudi hapa utupe mrejesho.

We acha tu, jana wakati wa usiku nikiwa nimebanwa na haja ndogo si nitoke niende toi, nakuapia sikufika niliambulia kukutana na matraco ya mama mkwe live bila chenga nikaludi zangu kulala kwa amani.
 
Kama uchawi upo, mimi nakupa picha ya SAMIA, MULIRO, MAFWELWE na KIKWETE uchague wawili uwaue ndani ya siku 3.
 
Uchawi unafanyika gizani kwa vificho kwasababu nia au lengo la uchawi ni uovu.

Uchawi sio maonesho au burudani, uchawi haufanywi hadhalani eti kwasababu tu ya kumdhiirishia mtu kama upo, ukiona mtu ana promote uchawi mchana kweupe basi jua hayo ni mazingaombwe sio uchawi.
 
Habari zenu Wana-jamiiforum?

Moja kwa moja kwenye mada, kuna minong'ono mbalimbali kuwa kuna nguvu fulani fulani zinazoweza kubadilisha hali ya kitu, kuleta maafa, kuleta bahati, au kuamua muafaka wa maisha ya wanadamu.

Binafsi mpaka nafikia huu sijawahi kushuhudia nguvu hizo.

Sasa naomba wale wanaoamini nguvu hizi wanithibitishie .

NB: Nipo tayari kutoa ushirikiano kwa atakayekuwa tayari kuthibitisha stori hizi.
Hakuna hata mbuzi mmoja atajitokeza kukuthibitishia. ....kila mtu anaujua uchawi kwa kusimuliwa tu.
 
Hapi ndipo matapeli wa uganga na uchawi wanajificha kwenye hoja kama zako
 
Hakuna hata mbuzi mmoja atajitokeza kukuthibitishia. ....kila mtu anaujua uchawi kwa kusimuliwa tu.
Moja ya kazi kubwa ya waganga wa kienyeji ni shughulika na matatizo yenye kuhusu uchawi, na sasa hivi kumekuwa na idadi kubwa sana waganga, sasa najiuliza inakuaje kila mtu aujue uchawi kwa kusimuliwa tu halafu kwenye jamii kumejaa waganga wa kienyeji?

Hauoni kwamba wingi wa waganga maana yake watu hujihusisha sana na hayo mambo na si simulizi tu ambazo wanazisikia bali ni mambo ambayo wanajihusisha nayo?
 
Kama uchawi upo, mimi nakupa picha ya SAMIA, MULIRO, MAFWELWE na KIKWETE uchague wawili uwaue ndani ya siku 3.
Hata hivyo ikitokea bado litabaki zoezi la kuthibitisha kuwa hivyo vifo ni vya uchawi, atatakiwa aelezee vp uchawi unavyofanya kazi na aleze na jinsi ulivyoweza kusababisha hivyo vifo.
 
Mimi nipo tayari kukufanya wewe mwenyewe uthibitishe kwa macho na mwili wako.
Jibu haya maswali yangu mawili then nitakupa mwongozo.

1 Katika hali ya kawaida, unaweza ukatafuna wembe ukaumeza na usidhurike??

2 Uko tayari kusafiri ili ukajiridhishe kuwa uchawi upo??

Karibu
 
Shida ya watu wenye kupinga uchawi hawajui kutofautisha kati ya kutokuamini kwao na kukosekana uthibitisho kwenye uchawi, kwa sababu unaweza usiamini kitu kwa sababu haujawahi kushuhudia au haujaona sababu za kukushawishi uamini au unajua hicho kitu sio kweli.

Sasa wapingaji wetu humu wa uchawi hawaeleweki kwamba hawajawahi tu kushuhudia huo uchawi, hawajashawishika tu kuamini uchawi au wanajua kiuhakika hakuna huo uchawi.
 
Usiseme Waganga sema Matapeli wameongezeka
Moja ya kazi kubwa ya waganga wa kienyeji ni shughulika na matatizo yenye kuhusu uchawi, na sasa hivi kumekuwa na idadi kubwa sana waganga, sasa najiuliza inakuaje kila mtu aujue uchawi kwa kusimuliwa tu halafu kwenye jamii kumejaa waganga wa kienyeji?

Hauoni kwamba wingi wa waganga maana yake watu hujihusisha sana na hayo mambo na si simulizi tu ambazo wanazisikia bali ni mambo ambayo wanajihusisha nayo?
 
Habari zenu Wana-jamiiforum?

Moja kwa moja kwenye mada, kuna minong'ono mbalimbali kuwa kuna nguvu fulani fulani zinazoweza kubadilisha hali ya kitu, kuleta maafa, kuleta bahati, au kuamua muafaka wa maisha ya wanadamu.

Binafsi mpaka nafikia huu sijawahi kushuhudia nguvu hizo.

Sasa naomba wale wanaoamini nguvu hizi wanithibitishie .

NB: Nipo tayari kutoa ushirikiano kwa atakayekuwa tayari kuthibitisha stori hizi.
Ndugu yangu, kuwa uyaone.
 
Usiseme Waganga sema Matapeli wameongezeka
Matapeli wapo karibu kila sehemu kwenye biashara na huduma mbalimbali hivyo waganga matapeli pia hawawezi kukosekana. Na waganga wote wangekuwa matapeli basi nadhani hadi sasa kusingekuwa na watu wenye kwenda kwa waganga.
 
Back
Top Bottom