Kama uchawi upo, mimi nakupa picha ya SAMIA, MULIRO, MAFWELWE na KIKWETE uchague wawili uwaue ndani ya siku 3.
Uchawi Upo lakini haufanyi kazi kama tunavyoaminishana mitaani/mitandaoni, na hauna nguvu kama tuliyoaminishwa kihivyo, una taratibu zake, haufanyi kazi kienyeji hivyo.
Kutoamini uwepo wa uchawi haiondoi ukweli kuwa uchawi upo na wenyewe haupungukiwi kitu kutoaminika uwepo wake na huenda unafaidika kutoaminika uwepo wake maana unaleta adhari kubwa ambazo visingizio hupewa vitu vingine, yaani si shida zake.
Jinsi zilivyotumika propaganda za kutuaminisha kipindi kile kuhusu stories za uongo kuhusu uchawi kutumika kuangusha magari, na ajali za kutisha, kupeleka watu kuzimu, sijui na maajabu gani ule haukuwa uchawi bali uzushi ambao hauhusiani na uchawi.
Uchawi wa kwanza kabisa unaanza ndani ya mtu kwa kukubali kwa utashi wake mwenyewe kumfanyia jambo baya mtu mwingine mfano chuku, wivu mbaya, husda, unafiki, mauwaji.
Uchawi wa pili ndio huo wa mtu kumilikiwa na nguvu hasi ndani yake ambazo huzitumia kufanya madhara ya kiroho yanayopelekea adhari mwilini.
Uchawi unafanyika kwa taratibu si hivyo mnavyotaka ninyi, kama huamini haya mambo usiyatafute kwa lazima yaache maana hayamkumbi kila mtu, mpaka utakapokuwa target.
Na kuna wale husema kama uchawi upo kwanini wachawi wasifanye maendeleo au kuwauwa baadhi ya wanasiasa, jamani haya mambo yanataratibu zake, zile movies za ki-nigeria si uhalisia wa uchawi na hazihusiani kabisa na uchawi wenyewe.
Mchawi hawezi kuroga kila mtu, mchawi hawezi kufanya uchawi bila yeye kumilikiwa na Demon, mchawi hawezi kukuua ukiwa mbali, mchawi hawezi kukudhuru bilia ya mtu wa karibu,
Huwezi kumdhuru mtu wa nyadhifa kubwa kiserikali kupitia uchawi maana nao unafanya kazi kiutaratibu kama vile mifumo yetu ya kisiasa inavyofanya kazi, yaani huwezi kuonana na mkuu wa mkoa bila Kupitia kwa viongozi wa chini kama watendaji kata, wakurugenzi na wakuu wa wilaya the same thing kwa uchawi.
Ili umfikie kiongozi wa nyadhifa kubwa ni either na wewe uwe wa nyadhifa kubwa au upitie kwa hawa Viongozi wadogo, ata uchawi ndivyo ulivyo, 50% ya hawa wanasiasa wetu hutumia hizi nguvu za uchawi ili kujilinda kiroho, hivyo hawawezi kudhurika kivyovyote vile Mpaka taratibu zifuatwe.
Nguvu anazotumia mkuu wa mkoa kujilinda ni tofauti na anazotumia balozi wa mtaa, the same thing nguvu anazotumia rais kujilinda ni tofauti na anazotumia mkuu wa wilaya au wizara fulani, hivyo basi iili umdhuru mwanasiasa fulani fuata utaratibu kama huu wa siasa za kidunia, Demon anayotumia kiongozi mkuu wa nchi ina nguvu kuliko anayotumia mkuu wa mkoa ndiomaana hawa maraisi huwa na utisho mkubwa na mamlaka makubwa si kwasababu ya nguvu za kicheo bali spiritual power behind zinazowalinda.
Ukitaka upambane ni wewe umiliki Nguvu kubwa zaidi yao jambo ambalo si jepesi, na mnachotakiwa kujua kuwa huwezi kumdhuru kiongozi wa kisiasa kupitia uchawi kama analindwa na uchawi hutofainikiwa maana haiwezekani na haitowai kuwezekana.
Kwamaana yeye mchawi na wewe mchawi ili kupambana mtatumia Demons kuzipambanisha ili mmoja adhurike kitu ambacho hakiwezeni, demon zinafuata utaratibu ule ule hazihombani wala kumdhuru mtu anayemilikiwa na demo mwenzao au kumdhuru mtu anayelindwa na demon(uchawi) maana yake kahalalishwa kichawi kuwa puppet wao iweje wewe mtu wa kawaida utumie uchawi kuondoa uhalali wa uchawi?.
Ni sawa na kusema umtumie mwanaCCM damu damu kuuangusha Uongozi damu damu wa CCM ambao uongozi huo ndio umempa majukumu hayo ya kuulinda huo mfumo.
Kiufupi, huwezi kumroga mwanasiasa wa level za uraisi Kupitia uchawi hilo sahau, labda kama mwanasiasa huyo hatumii nguvu hizo.