Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Mengi ni historia,wengi wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?

Jamani fanta ya kidonge ilikuaje?
 
Nakumbuka foleni kupata unga, mchele, sukari n.k. Ugawaji, RTC na NMC. LAKINI HaKUNA MGONJWA HOSPITALINI ALIEKOSA SABUNI -ACHILIA MBALI CHAKULA (MILO MINNE KWA SIKU)!
RTC Magodown naona kachukua Mohamed Enterprise!!
 
Jamani fanta ya kidonge ilikuaje?

Fanta ilikuwepo ya kidonge unakiweka kwenye glass ya maji ya kunywa yanabadilika rangi na ladha inakuwa ya Fanta

Vidonge vilikuwa vingi kama Cafenol...ASPRO...na ungaunga wa Andrews kwa tumbo la gesi na kiungulia
 
Kwa kumbukumbu hizo zote sijaona comments za waliyokasirika au kujuta kwa hali ilivyokuwa, ila bado huwa sielewi kwa nini awamu ya kwanza inavyotukanwa na kubezwa? Hivi katika awamu zilizofuata tunazikumbuka/ tutazikumbuka kwa lipi?
 
Kwa kumbukumbu hizo zote sijaona comments za waliyokasirika au kujuta kwa hali ilivyokuwa, ila bado huwa sielewi kwa nini awamu ya kwanza inavyotukanwa na kubezwa? Hivi katika awamu zilizofuata tunazikumbuka/ tutazikumbuka kwa lipi?
Labda kwa Mv Bukoba...Train ya Gulwe..EPA...Richmond..na mabomu mbagala na Gongo la mboto
 
Labda kwa Mv Bukoba...Train ya Gulwe..EPA...Richmond..na mabomu mbagala na Gongo la mboto
Zamani kulikuwa na maneno yenye kutia hamasa na yaliyoaminika kwa viongozi na wananchi na yaliyoleta matokea chanya, mfano:- Uhuru na umoja, Uhuru ni kazi, kilimo cha kufa na kupona,usiwe manamba,usiwe kupe,kilimo cha kufa na kupona,siasa ni kilimo,kisomo cha watu wazim,etc, linganisha na maneno ya sass, mfano:- mpango mkakati, wadau,wafadhali, wapiga kura wangu,si mwenzetu,kilimo kwanza,MKUKUTA,MKURABITA,MKUZA,mwadilifu,etc
 
tancut almasi kinyekinye kisonzo fimbo kugoda au mabush star? kasaloo akamtungia wimbo jean butinini dada yake na mshambuliaji wa reli moro duncun butinini. duh the good old days.
 
Ushakunywa 'double cola'? Nakumbuka hata shule sijaanza ila niliweza kuisoma jinsi ilivyoandikwa.
Ulishaishika senti hamsini, na sh 10 ya note?
 
Ushakunywa 'double cola'? Nakumbuka hata shule sijaanza ila niliweza kuisoma jinsi ilivyoandikwa.
Ulishaishika senti hamsini, na sh 10 ya note?

Kaunga we bei ya chini kabisa kununua soda ni shs ngapi?? Mi nakumbuka vizuri ni shs 60/ tena hapo nipo mkubwa!!

Nakumbuka nikiwa mdogo sana niliokota shs 38/ ile hela ilikuwa sawa na kuokota laki leo au zaidi. Misuko suko yake sijaisahau mara kwa balozi na balozi ndo anaogopeka enzi hizo!! Tukaenda ofisi za mtaa zikatangazwa hakutokea mmiliki nikarudishiwa, zilikuwa ni nyingi sana coz matumizi yalikuwa senti tano na juu sana shilingi! Mwendo wa thumni hahahaaa unaijua hiyo??
 
Rtc, tanganyika tanaries, kncu, maziwa halisi, notco, nafco, shell, mobil, agip, bedford,juwata, ottu, tanu youth league,mwatex, tanalec, azimio la arusha,sabasaba,uhuru na jamhuri,madaraka mikoani vijiji vya ujamaa, gezaulole, kabaila, bwenyenye, sabuni kanga, ujamaa na kujitgemea, elimu ya kujitegemea, upe, dartex,mpango wa maendeleo wa miaka mitano, scopo,npf,radio sauti ya injili ikitangaza toka addis ababa ethiopia, kenna(kahawa), safari boot, kiatu cha ngozi 99, stileto, raba mtoni, saa ya seiko 5, bonamade(dawa ya meno),nuta,barabara ya stilingi(sterling), nguo za oksheni(auction), bafta, robin wood, jinja, khaki,kalamu ya kinsing,miezi kumi na nane ya shida, motel agip,drive inn cinema, cameo, avalon, starlight, hotel continental, sea view, etienes, nyumba ya sanaa, ymca, bushtrekker, air tanzania corporation, matshishuta, mawenzi hotel, co cabs, longman press,kiuta print, sido, nico, alaf,jet club, national milling corporation, scania kibaha,tanzania tours corporation(ttc),benki ya nyumba tanzania(thb), gazeti la baraza toka kenya,mafuta ya karanga, mafuta ya pamba, supper ghee, kcc, shimawimo, msamaria mwema, shirika la posta na simu tanzania
 
kunavitu menifurahisha kunikumbusha kama huyo TT wa TRC labda nami nikukumbushe jamaa mmoja wa TRC alikua anaitwa Kiluma huyu nae ni TT,Sijafurah mdudu mmoja umemtaja anaitwa Cda.
 
Shirika la Nyanza,mafuta ya mamis,bright light,chupi za Tyson ndala za umoja

tiper? tulikuwa tunapata lami hapa hapa na mafuta bei poa. kiwanda cha ngozi na magunia moshi wacha tz itajengwa na wenye moyo na kuliwa na wenye meno.....!!!!
 
Kaunga we bei ya chini kabisa kununua soda ni shs ngapi?? Mi nakumbuka vizuri ni shs 60/ tena hapo nipo mkubwa!!

Nakumbuka nikiwa mdogo sana niliokota shs 38/ ile hela ilikuwa sawa na kuokota laki leo au zaidi. Misuko suko yake sijaisahau mara kwa balozi na balozi ndo anaogopeka enzi hizo!! Tukaenda ofisi za mtaa zikatangazwa hakutokea mmiliki nikarudishiwa, zilikuwa ni nyingi sana coz matumizi yalikuwa senti tano na juu sana shilingi! Mwendo wa thumni hahahaaa unaijua hiyo??

Kama si sh 6 basi itakuwa sh 12. Thumni tulikuwa tunanunua kitumbua ambacho leo utanunua sh 200. So pesa imeshuka thamani mara 400.
 
SHIMAWIMO, hili lilikuwa kama UDA, ila lilikuwa pale moshi. Tanzania bag, au magunia pale pale moshi, GAPEX, TANARIER, MACHINE TOOLS, TES, nk.

Life bouy, Rexona, sabuni maarufu enzi hizi, mafuta ya kupaka yakijanja lazima upake Yolanda au YOU! Yananukiaaah.

Mitindo ni nywele, afro, mashati ya juliana, sketi zenye mpasuo zikiitwa "sina habari" kumbi za sinema Plaza cinema, na ABC cinema.

Movie za kiindi, Dostana, amne samne, bombay 405 miles, ashanti, andhaar khanoon, the burning train, Naseeb, the great gambler,disco dance...masteling Amitab batchan, mithun chakraborty, Rish kapoor, Rajesh khana, Shash kapoor, dharmendar, Vinod khan...majambazi, Amjed khan, Ranjeet, Amrish poor, mademu waliotamba enzi hiza, Jaya Prada, Hema Malini, dah, long tym kweli.
 
Mimi nakumbuka tu suruali za Bayokti na Viatu vya Ndulla...

Then ndiyo vikaja viatu vya Dockers, landrover n.k
 
Back
Top Bottom