Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Mengi ni historia,wengi wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?

Mkuu haya mambo mbona tumeshayaongelea sana hapa JF!
Ebu pitia hapa:
[post=3678402]Kama hujawahi tumia hii kimbo, basi wewe ni kizazi cha Lulu[/post]
 
Hao pamoja na MANG`ULA Machines na NYUMBU JWTZ KIBAHA
Bora hata zingegeuzwa kuwa Polytechnic Colleges

Unakifahamu kiwanda cha radio cha Philips Arusha?? Inauma sana aiseee....!!

General Tyres nako vipi?? Nchi imelaaniwa hii kaka!!

Tunaojua historia ndogo tu ya hii nchi!! Tuna machungu na ni bora kizazi chetu kipite tu mana nahisi kuna siku tutakuja kuchafua hali ya hewa ya hii nchi!! Serious, sijui kama uchungu ninaoupata mimi na vijana wengine wa age yetu wanao na bado wanashabikia siasa uchwara!! Siasa inayodidimiza badala ya kuinua nchi

Kili Tex ilikuwa ina export nguo ulaya mamamaaaaeeeee....!!

Tanzania Bag (Magunia) unaikumbuka??
 
Hii nchi ni tajiri toka zamani aisee
 
Bongo unatega antenna TVZ ya Zanzibar nawale wa Moshi wanatega antena za miba kushika KBC ya kenya
 
Mkulu, kuna kiwanda kilikuwa kinaitwa TanCut Almasi! Historia yake inauma sana, kifo chake kinasikitisha sana!
Iringa ilikuwa Moto kwa Tancut Almasi..Cocacola..Dabaga..Mgololo...Bendi ya Kimulimuli JKT nk
 
Hii nchi ni tajiri toka zamani aisee

Kaka mi nalia na utalii tu! Tanzania ni nchi ya pili kwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii duniani! Cha kushangaza ni ya 105 kwa kuvutia watalii duniani! Hivi kuna nchi kweli hapa?? Tungeweza kusamamia vivutio vyetu tu na kutangaza duniani kote, tusingekuwa nchi ya kukopa hata kidogo

Nchi ni tajiri sana hii
 
Radio toka kiwanda cha MATSUSHITA; unapata DUDU PROOF haina matatizo na mende wala wapi unaiweka!!! Muziki kwa kwenda mbele toka kipindi cha Shambani Mkulima (jioni baada ya taarifa ya habari ya saa kumi)
 
Gonga hapa:
[post=6545833]Nani wanakumbuka haya-RTC, KAUDO, KAUMA, KAURU?[/post]
 
Hiki ni kile kiwanda cha karatasi?? Nasikia kulikuwa kuna kiwanda cha kutengeneza spares za machine huko Mufindi hatari kabisaa na wamekiua??

SPM kiwanda kikubwa zaidi A. mashariki na kati. Kikiwa kikiwa cha tatu kwa ukubwa miongoni mwa viwanda vya karatasi ulimwenguni kikitanguliwa na kile cha Norway na kile cha south
walikigawa kwa masingasinga kwa bei ya kutupa! Hawakuridhika wakawatenda unyama wafanyakazi wake! Inachukizaaaa
 
Tuncut almas,Imucu,Imac n.k Pale Ir town EInkoskaz;10718681]SPM was a giant in Paper Industry
Wapi KIUTA Na PRINTPAK?[/QUOTE]
 
duh! bora shoes hiyo khabari nyingene! kuna kiatu nilinunuliwa miaka miwili bado kizimaa, nikakichoka ikawa nikitoka shule kila jiwe halali yangu lakini wapi kikakaa kama mwaka ndio kikaisha.

unanikumbusha mbali sana nilikua napita juu ya reli na kusugua ili kiishe tu ninununliwe kingine!!!
 
Loo,hahaha leo mmenirudisha mbali sana zama za utoto wangu nakumbuka shule nilikuwa navaa mashati ya shikibo na viatu vyeusi vikiitwa prefect sikumbuki vilikuwa vinatoka wapi,nakumbuka usafiri wa Trcenzi hizo wakuaminika sana nikisafiri toka Dar kuelekea nyumbani Ujiji nilikuwa nina enjoy sana ile trip kupitia Tabora ile ilikuwa ni safari moja ya kiuhakika kulikuwa hakuna kufikiria labda mtatekwa na majambazi porini wala kuibiwa au kunyang"anywa mali au mizigo yako na pia tusiisahau network iliyokuwepo Afrika ya mashariki,pia ilikuwa ni ya hali ya juu sana,nakumbuka safari yangu ya kwanza kutoka nje ya nchi kupitia Mwanza pale nilikuwa naunganisha through Mv Victoria inanipaleka Kisumu na nikifika pale naunganisha Train inanitupa Nairobi kwa usiku mmoja asubuhi namkuta brother wangu Nairobi Railway station ananisubiri kunichukuwa nyumbani kwake,ile network iliyokuwepo ilikuwa ni universaly sana yaani unalipia ticket yako Dar inakufikisha mpaka NBO kwa kutumia kuanzia njia za Buses,Rail na unakuja unganisha na meli unaunganisha tena na Train mpaka unafika ktk destination yako,je ni vipi hii EAC ya sasa inashindwa kuwa na network kama ile?au huu ubinafsishwaji wa vitu nao unachangia ktk kuturudisha nyuma kimaendeleo nini?(utandawazi).Leo mmenirudisha mbali sana marehemu mzee Kambarage Nyerere capacity yake kiuongozi namlinganisha na ya hawa wote viongozi tuliokuwa nao hivi leo ukiwajumuisha wote kwa pamoja.M/Mpamba.
 
Mie nakumbuka mengi, gari ya serikali 'ST' kusimama na kukupa 'lifti' uendako,

Nakumbuka huduma bora hospitalini licha ya vifaa haba changamoto ya teknolojia wakati huo,

Nakumbuka jinsi benki ilivyokuwa ikithamnini wateja wake, usiri wa habari za wateja, kumbukumbu nzuri licha ya kutokuwepo tarakilishi, nk.

Nakumbuka simu za REVERSE CALL, nilitumia sana hii...

Nakumbuka MONEY ORDER, raha sana ukipata hiyo ukiwa boarding... Hata barua tu, wengine walijiandikia ilimradi aonekana naye kapata barua, nimekumbuka hii pia "... ama baada ya salaam, utakapo kujua hali yangu mimi ni mzima hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu...'

Nakumbuka Ikarus kumbakumba na UDA enzi hizo kabla ya ujio wa Benz na Isuzu,

Nakumbuka mshahara KCC TSh. 275 uliotosha matumizi yote (muhimu) ya mwezi na chenji kubaki...

Hahahaa nimekumbuka mchakato wa kumtongoza umpendaye! Looooooong process hadi ukubaliwe du! Na ladha ilikuwepo ukimpata.

Nimekumbuka mengi...

Hiyo ya mwisho nimeipenda. Kutongoza ilikuwa ni issue. Unaandika barua, utume mtu nk unaweza kusota hadi miezi hujafanikiwa. Siku hizi ndani ya dakika moja mchezo umekwisha
 
Mengi ni historia,wengi wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?
wazawa wawekeza kwenye sekta binafsi wengi walichota mtaji toka mashirika hayo yaliyokua ya umma.
 
Mengi ni historia,wengi wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?

Kazi kubwa sana hii aliyofanya Nyerere. Yalipoingia majambazi na majizi haya yakauza vyote na kama haitoshi yakajigawia mpaka nyumba za serikali. Imebaki historia. Halafu yalivyokuwa majinga yanawaambia vijana wajiajiri wakati yameua nafasi za ajira.
 
Maduka ya CRSU. Kweli tumetoka mbali. Shemeji yenu nilimfukuzia miaka 2. Mwaka 2 na nusu nikala mzigo. Sasa hivi je?
 
Back
Top Bottom