Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Wale wa zamani mnakumbuka haya Mashirika?

Inkoskaz

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Posts
6,359
Reaction score
2,389
Mengi ni historia,wengi wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?
 
mimi nachokumbukawaliokuwa viongozi waliviuwa hayo mashirika sasa tuwashitaki kwenye makanisa au misikitini kufuatana na imani zao
 
duh! bora shoes hiyo khabari nyingene! kuna kiatu nilinunuliwa miaka miwili bado kizimaa, nikakichoka ikawa nikitoka shule kila jiwe halali yangu lakini wapi kikakaa kama mwaka ndio kikaisha.
 
mimi nachokumbukawaliokuwa viongozi waliviuwa hayo mashirika sasa tuwashitaki kwenye makanisa au misikitini kufuatana na imani zao

Mkuu mbona wanajulikana!
Wameuza majumba Oysterbay na Masaki na sasa wanauziwa wageni kwa bei ya Mgodi!!
Poor Tanzania!
 
duh! bora shoes hiyo khabari nyingene! kuna kiatu nilinunuliwa miaka miwili bado kizimaa, nikakichoka ikawa nikitoka shule kila jiwe halali yangu lakini wapi kikakaa kama mwaka ndio kikaisha.
Wenzetu Kenya BATA shoes bado inadunda sisi tu ndio hatujithamini
 
Meli za TACOSHILI DAR MTWARA 34 HOURS FULL KUTAPIKIANA. MV MAPINDUZI UNABUKU PALE VIJANA ZANZIBAR UNAFIKA KESHO YAKE.

TACOSHILI...NASACO...SINOTASHIP

Watu wa Lindi na Mtwara wanaikumbuka sana MV Mapinduzi..wakifika Dar wanapand Treni au mabasi ya TRC na KWACHA au ZAINABS
 
Mie nakumbuka mengi, gari ya serikali 'ST' kusimama na kukupa 'lifti' uendako,

Nakumbuka huduma bora hospitalini licha ya vifaa haba changamoto ya teknolojia wakati huo,

Nakumbuka jinsi benki ilivyokuwa ikithamnini wateja wake, usiri wa habari za wateja, kumbukumbu nzuri licha ya kutokuwepo tarakilishi, nk.

Nakumbuka simu za REVERSE CALL, nilitumia sana hii...

Nakumbuka MONEY ORDER, raha sana ukipata hiyo ukiwa boarding... Hata barua tu, wengine walijiandikia ilimradi aonekana naye kapata barua, nimekumbuka hii pia "... ama baada ya salaam, utakapo kujua hali yangu mimi ni mzima hofu na mashaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu...'

Nakumbuka Ikarus kumbakumba na UDA enzi hizo kabla ya ujio wa Benz na Isuzu,

Nakumbuka mshahara KCC TSh. 275 uliotosha matumizi yote (muhimu) ya mwezi na chenji kubaki...

Hahahaa nimekumbuka mchakato wa kumtongoza umpendaye! Looooooong process hadi ukubaliwe du! Na ladha ilikuwepo ukimpata.

Nimekumbuka mengi...
 
Simu za kuomba kwa operator au kupiga kwa mafundi wa posta kwenye mashimo ya distribution Boxes
 
Simu ya kuzungusga dial pad na simu ya kukoroga handle ioate chaji!!
 
Mengi ni historia,wengi
wamepitia na kupata huduma zake.Wapo ambao familia zao zimefadika nayo
na wengine bado wana kumbukumbu zake na kadhalika
Hebu tujikumbushe

TAFICO,MWATEX,SUNGURATEX,URAFIKI,MORO SHOE,TANGANYIKA PARKERS,NARCO

TFA,BORA SHOES,GENERAL TYRE,SUDECO,SUKITA,SHIHATA,RTD,TFC

UDA,KAMATA,DMT,KAUDO,KAURU,KAUMU,CORETCO,MORETCO ETC

BESCO,HOSO,CDA,NMC,NDL,RUBADA

Je umetumia daftari la Tanzania Elimu Supplies
Binafsi nimevaa raba za Moro shoes,Safariboot za BORA!
Magazeti ya Mfanyakazi
Cartoon za Chakubanga,Polo,Bushiri na akina MZEE KIBOGOYO
Sabuni za Mbuni na Gardenia
Mafuta ya Supa Ghee na Voil
Je umekunywa Fanta ya Kidonge?
Chai ya Sukari guru je?
Basi la Railway Dar Mby siku tatu
Kutumiwa pesa kwa Telegram
Ulishakutana na TT na mzee Kipara wa TRC?
Mkate wa Siha?
Tiper za Bedford
Leyland CD
Baiskeli za Phonex
Cherehani za Singer
Battery za National
Kanda za Phillips
Mashati ya Juliana
Saa za Mortima

Duh!

Tumetoka mbali
Nimekumbuka tu
Je wewe unakumbuka nini?

Umenikumbusha mbali sana, naumiss sana Mkate wa Siha.....
 
Kilimanjaro Machine Tools, tungekuwa tunaunda hata ndege sasa! Jamaa walikuwa wanatengeneza vipuri vya mashine hatari kabisa
 
SPM Mgololo wameniacha na painfully memorial!

Hiki ni kile kiwanda cha karatasi?? Nasikia kulikuwa kuna kiwanda cha kutengeneza spares za machine huko Mufindi hatari kabisaa na wamekiua??
 
Kilimanjaro Machine Tools, tungekuwa tunaunda hata ndege sasa! Jamaa walikuwa wanatengeneza vipuri vya mashine hatari kabisa
Hao pamoja na MANG`ULA Machines na NYUMBU JWTZ KIBAHA
Bora hata zingegeuzwa kuwa Polytechnic Colleges
 
Shirika la Nyanza,mafuta ya mamis,bright light,chupi za Tyson ndala za umoja
 
Back
Top Bottom