Niache Nteseke
JF-Expert Member
- Apr 29, 2020
- 2,736
- 3,638
Yaaani mtu ako na first class GPA ya 4 unamuacha kwenye shortlisted?
Hii haikubaliki.
Ndo inakuja ishu ya ubora wa vyuo, maana huwezi kuipata GPA kubwa kwenye vyuo makini kama ukiwa kilaza.Kwa kweli mtu anaweza kuwa na hiyo GPA kubwa lakini uandishi ukawa kama "MTU AKO..." hata kama mimi ndio HR kiukweli nitakuwa na kila sababu ya kumuacha huyo mtu.
Ubora wa vyuo unapimwaje kaka? Kwa kufaulisha sana au kwa kufundisha vizuri au kutoa mitihani mepesi au migumu? Hebu fikiria hili na lipo sana vyuoni, chuo ni bora sana ila mwanafunzi anajibebisha kwa walimu wamuongezee marks na wengine wanajiliza kabisa na kutoa sababu kemkem kama Mimi ni maskini nikifeli nitaenda wapi? Mwalimu anashikwa na huruma anamuongezea hata marks 10 kwenye coursework na ikatokea final UE akapambana akapata B+ ,unataka kusema huyo akipata GPA 4 Kwa nyongeza za marks atakuwa na uwezo mkubwa kuliko aliyepata 3.8 bila nyongeza ya marks?Ndo inakuja ishu ya ubora wa vyuo, maana huwezi kuipata GPA kubwa kwenye vyuo makini kama ukiwa kilaza.
Ndo inakuja ishu ya ubora wa vyuo, maana huwezi kuipata GPA kubwa kwenye vyuo makini kama ukiwa kilaza.
Ni mawazo yako tu. jifunze kufanya vitu Kwa umakini uone faida zake. Unaweza kuta kampuni inatangaza ajira huambiwi uambatanishe vyeti wala nini ila utume CV tu au mara nyingine CV na Barua. Unadhani hii kampuni itatumia kigezo Cha ufaulu au GPA kufanya shortlisting wakati umetuma CV tu?Kweli kabisa .
Sema wachangiaji wengi humu ni lower performance ndio maana wanatetea kuacha kwa wenye GPA kubwa sababu ya wivu n.k.
Kama una gpa ndogo ni dalili kwamba wewe sio mtu uliye serious na hujitumi.You are bitter and sour, mafanikio hayaji ukiwa na mentality hiyo. Huyo wa Lower maana yake amejiuza vizuri kwenye CV na Cover letter, huko kazini hawaendi kufundisha bali kuperform sasa GPA ni jambo moja na performance ya kazi kwa kutumia pattern zile zile kila siku zinahitaji mtu mchakalikaji,mbunifu na anayejua kujieleza.
Unaonekana hata ofisini akija mteja utakuwa unamtishia na GPA. Tumia huu muda kuandaa CV nzuri hawa TRA hawatachukua muda watatangaza kazi nyingine sasa kama wewe utakuwa umekaa kuringia GPA badala ya kuangalia ulipo jikwaa na zenyewe zitakupita ingawa nakuombea ufanikiwe.
Jumapili njema.
Kwa hiyo unategemea watu wanaosoma feza boys au girls secondary wawe na uwezo sawa kama wale wanaosoma makamba secondary Kwa sababu wote wanasoma masomo yaleyale ya sekondari?Ni muhimu sasa kuvipima hivi vyuo vyetu kama vinatoa elimu yenye ubora unaotakiwa.......nilitegemea watu waliosoma kozi ya aina moja na wakapata first class wawe na uwezo uleule bila kujali chuo walichosoma.
We jamaa mshamba wa wapi ?kama GPA Ya uwizi.Kuna mtu ako na GPA ya 4 lakini jina halijatoka shortlisted [emoji848][emoji848]
Lakini wenye lower second majina yametokea kwenye shortlisted,
Hii inaingiaje akilini?
Kwa hiyo GPA ya 4.5 ya IAA ni bora GPA ya 3.0 kutoka Havard? Mwenye GPA kubwa ya IAA na GPA ya Havard ,nani anauzika zaidi?Kama una gpa ndogo ni dalili kwamba wewe sio mtu uliye serious na hujitumi.
Huwezi linganisha mtu mwenye 4.5 na mtu mwenye 2.1 gpa.
Kwa hiyo unategemea watu wanaosoma feza boys au girls secondary wawe na uwezo sawa kama wale wanaosoma makamba secondary Kwa sababu wote wanasoma masomo yaleyale ya sekondari?
Huwezi kutegemea hivyo Kwa sababu ya heshima na ubora vyuo vilivyojijengea. Hata Kwa Marekani Havard ni chuo Bora kuliko vingine ,ipo hivyo. Mtu aliyesoma Havard na kupata GPA ya 3.5 ya uchumi ni bora kuliko aliyesoma IAA na kupata GPA 4.8 kwenye uchumi
GPA za vyuo ni kitu universal ndio maana Kwa degree iliyopatika mlimani inatambuliwa pia Marekani lakini swali ni kwamba hata kama elimu ya chuo ni universal ,ni kweli Havard ni sawa na UDSM kwenye ubora?Naongelea vyuo vya hapa ndani maana vyote viko regulated na TCU......kwa nini ionekane vyuo vingine vinafyatua vilaza wenye first class, tatizo linakuwa ni nini?
Kwa mujibu wa mawazo yako.Kama una gpa ndogo ni dalili kwamba wewe sio mtu uliye serious na hujitumi.
Huwezi linganisha mtu mwenye 4.5 na mtu mwenye 2.1 gpa.
Kuna swala la uwezo binafsi wa mtu haijalishi kasomea chuo gani, kama contents za UDSM ziko sawa na Havard hapo kinachoamua ni kichwa na siyo jina la chuo.GPA za vyuo ni kitu universal ndio maana Kwa degree iliyopatika mlimani inatambuliwa pia Marekani lakini swali ni kwamba hata kama elimu ya chuo ni universal ,ni kweli Havard ni sawa na UDSM kwenye ubora?
Ipo hivyo dunia nzima na hata Marekani GPA ya Havard ni tofauti na za vyuo vingine
Unanifurahisha sana. Tuzungumze Kwa mifano halisi sana: kama content za Havard na za UDSM zipo tofauti ina maana ya kwamba content za Havrard ni Kwa mazingira ya Marekani na Content za UDSM ni Kwa mazingira ya Tanzania ,swali: Mbona watanzania waliosoma UDSM Uchumi wanaenda kufanya kazi Marekani na wakati content za UDSM hazijawaanda Kwa mazingira ya Marekani?Kuna swala la uwezo binafsi wa mtu haijalishi kasomea chuo gani, kama contents za UDSM ziko sawa na Havard hapo kinachoamua ni kichwa na siyo jina la chuo.
Tuzungumzie suala la uwezo binafsi wa mtu Kwa kuangalia na suala la ajira kwa hiyo unakubaliana na Mimi kwamba GPA sio kigezo rasmi Cha kupima uwezo wa mtu kwenye ajira Kwa sababu inawezekana mwenye uwezo mkubwa sana lakini kwa kusoma Havard akashindwa kupata GPA kubwa lakini mwenye uwezo mdogo lakini Kwa kusoma IAA akapata ufaulu mkubwa sana. Je, kwenye suala la ajira tumfanye huyu mwenye GPA kubwa ni genius na huyu mwenye ndogo ni kilaza Kwa sababu tunaangalia GPA?Kuna swala la uwezo binafsi wa mtu haijalishi kasomea chuo gani, kama contents za UDSM ziko sawa na Havard hapo kinachoamua ni kichwa na siyo jina la chuo.
Ndugu zenu au ni wewe mwenyewe?Wandugu kama una desa lolote la Tax Mgt officer tafadhali tuwekee hapa, tuwafanyie wepesi ndugu zetu wapate pakuanzia, karibuni tafadhali
Sawa tufanye ni mimiNdugu zenu au ni wewe mwenyewe?