Wale tuliowahi kupata Division 1 A-Level na O-Level tukutane hapa!

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,716
45,117
Wakuu leo nimeona tujuane wale ambao tumewahi kutusua katika elimu ya bongo, yaani tulipata division one katika mitihani ya Taifa aidha wa O-level au A-level.

Kama uliwahi kupata division one A-level sio mbaya ukatutajia na kombinesheni uliyosoma ili kusudi tujuane na tuwahamasishe wadogo zetu wanaosoma kwa kutoa mbinu zilizopelekea tukapata hizo division one.

Karibuni kwa mjadala...
 
Maisha sio Vyeti mpaka sasa mnamaendeleo gani kama bado mpo kwa wazazi na bado hamjaanza kujitegemea hizo Div one na First Class ni Useless mnashindwa hata na wamachinga wa pale K/koo wanalaza kwa siku 20-60 kwa siku na wanauza underwear ww hayo ma A yako yanafaida gani ikiwa hela ya kula tu inakupiga chenga

Sent using Jamii Forums mobile app
mkuu kila mtu ana ndoto zake, yawezekana aliye pata one ndio ilikuwa ndoto yake katika maisha.hata akiishi kikawaida ila ana furaha katimiza ndoto yake.

ww ndoto yako ilikuwa kuwa na hela ukaitimiza una furaha japo kusikia mtu anajisifia one inakuuma kuona una hela ila huna division one.

kuna mtu ana maisha mazuri kunizidi ila huwa hana amani sijui kwa nini? maana nimemzidi kiwango cha elimu (kila siku analalamika kujiendeleza) wakati hela anayo maisha mazuri yapo kisa kumzidi elimu.

Nilicho gundua kuwa na hela,(maisha mazuri) bila elimu kiasi nayo inakosesha furaha.
 
Mi nilipata one enzi hizo makongo ilikua ishu ya kawaida tu manake darasa zima lilikua linaenda chuo kikuu siku hizi mambo sijui yakoje.Kuna siku nilienda pale shule kuchukua result slip yangu nikakutana na captain mmoja nikamwambia nimefata result slip nazani alienda kunitafutia kwa nyodo hivi alivyoludi nayo akawa anajichekesha eti kumbe ulituletea sifa hongera sana akawa ananiuliza niko wapi nafanya nini nikamchapa bakora nikasepa zangu(kuchapa bakora kumlingishia kuwa nimetoboa na ninapofanya kazi pazuri nazani alijiona zuzu ha ha ha ha )ila kusema ukweli mi sijawai kusoma saaana ile kukesha sijui sijawai.
 
mkuu kila mtu ana ndoto zake, yawezekana aliye pata one ndio ilikuwa ndoto yake katika maisha.hata akiishi kikawaida ila ana furaha katimiza ndoto yake.

ww ndoto yako ilikuwa kuwa na hela ukaitimiza una furaha japo kusikia mtu anajisifia one inakuuma kuona una hela ila huna division one.

kuna mtu ana maisha mazuri kunizidi ila huwa hana amani sijui kwa nini? maana nimemzidi kiwango cha elimu (kila siku analalamika kujiendeleza) wakati hela anayo maisha mazuri yapo kisa kumzidi elimu.

Nilicho gundua kuwa na hela,(maisha mazuri) bila elimu kiasi nayo inakosesha furaha.
Mm hainiumi kitu kabisa lakini sioni haja kujitaba kuwa na one alafu ni Jobless unaona Aibu hata kuchoma maindi barabarani kuuuza matunda alafu Darasa la saba Failure anafanya shughuli hizo na amepanga na analisha familia yake

Kisha msomi wa Div one na first class darasani alafu mtaani Ziro maisha yanakuchapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha sio Vyeti mpaka sasa mnamaendeleo gani kama bado mpo kwa wazazi na bado hamjaanza kujitegemea hizo Div one na First Class ni Useless mnashindwa hata na wamachinga wa pale K/koo wanalaza kwa siku 20-60 kwa siku na wanauza underwear ww hayo ma A yako yanafaida gani ikiwa hela ya kula tu inakupiga chenga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama unaumia sio kwa hasira hizi aseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom