Wale tulioingia chuo kwa mbwembwe na tukaishia kudisco kwa aibu tukutane hapa

Mkuu ulikua hupigi msuli sana nini? Nina jamaa yangu mmoja alikua kipanga haswa o level na advance kote kapiga one ila chuo akawa hahudhurii vipindi , anasoma karibia na mitihani akaja kudisko ila angesoma natumaini angepata gpa kubwa sana. Pole sana kaka masomo yalikua magumu au? Maana na sisi tupo hapo hapo ud tupe info yasitukumbe na sisi
Kiujumla nilichukulia masomo ya chuo simple simple sikuwa nakaza nilikuwa bize na siasa na maswala mengine,kingine niliingiza mawazo ya kuwa hakuna ajira so morale ya kusoma ikapotea,nilikuwa overconfidence sana no discussion na mtu na ishu nyingine,kuanzia second year masomo karibu yote ya uchumi ni mahesabu magumu na mie sikuwa na base nzuri ya mathematics so ikazidi kunifrustrate japo sikuwaza kama ningedisco maana nilikuwa najiamini sana hadi Leo sijui ilitokeaje
 
Kwa taarifa yako masister duu wa IFM ndio wanafaulu kuliko madume wote hapa nchini. Usiniulize wanafaulu vipi.....
Sio kweli mkuu...kama unazungumzia kutoa k ili ufaulu imekula kwako

Yaani ukiingia na gia hiyo kile chuo ni total loss

K wataila na disco or supp liko pale pale trust me!
 
Kwa kutumia pichu zao na mali asili zao
Sio kweli...nilishuhudia hiyo 1st year, madadaz semista ya kwanza coursework bila bila...utamu walitoa but at the end of results wakatupwa kanaani! Na wengi wanadanganyana pale

Niamini Mimi, hakuna wa kukufaulisha pale bila juhudi zako
 
Duh.. Mimi sikuwahi kuipata hat C tokea first year na nilikua sikomai sana. Cha muhimu nilikua sikosi lecture bila sababu ya msingi na nilijitahidi kuelewa pale pale.

Ila kuna jamaa mmoja huyo alikua mlevi balaa na lecture haudhurii lakini kwenye test, paper anatusua vizuri tu. Kuna wajinga walifata company yake wakaishia kukamatwa na juche wakadisco
 
Mlioko chuoni kiukweli mnatakiwa mkaze kweli kuliko hata advance,kwa maoni yangu chuo no kigumu kuliko advance achaneni kabisa na mambo yasiyohusiana na masomo,kwa mfano mlioko UDSM B.A economics na B.com Acc. ukipata kuanzia GPA ya second class and above ni rahisi kupata ajira, chini ya hapo utahaso mpaka ujute kusoma.
Hasara niliyopata ni kubwa coz xwez apply tena mkopo mpaka nilipe wa awali,pili kuanza kusoma degree upya tena ya engring bila ya kuwa na ajira ya serikali huku umri unasonga ni ishu,nimeamua nikomae na dip.yangu nisake pesa tu,sitegemei kuja kusoma tena official education uzuri kwenye fani ya civil uzoefu ndio chuo chenyewe ukiwa private sector
 
Daah yani kuna kipindi unasoma usipate sup yani inaitwa fighting for survivor ....tena na system ya Mzumbe ilivyo ..wanaziunganisha sup ya semester ya kwanza na ya pili if zikiwa 4 ..ndo kwaheri hiyo ...

Mu main campus .....wale wazee wa kupaki basi tunajuana 5-4-1 ndo formation yetu wana MU .....
 
Mimi nilichaguliwa UDOM Bsc in Computer Engineering mwaka 2013 na nisiwe muongo tu wakuu nilikuwa mzembe sana kipindi nipo chuo. Nilikuwa siingii class, yani me ni mtu wa Town tu Mara Jamatini, Mara nipo zangu Capetown pub pale karibu na stand ya mkoa.

Wakuu hakuna chimbo la Malaya pale Dodoma sikulijua, sio CDA wala Chakochako kote huko nilifika. Kwangu Mimi niliamini kudisco ni story tu nikasema lazima nimalize.

Wakuu Kwa mshangao mkubwa sikuamini baada ya kufungua UDOM SR yangu nikakuta Nina GPA ya 1.1 hivyo sikufika hata GPA ya 1.8 ya kufanyia supplementary hivyo nikutana na red ikisema discontinuation .

Nilipatwa na mshangao mkubwa kutokana na mawazo yangu yote kuwa kufaulu O-Level na A-Level Kwa kiwango kikuu kungenipa kinga kuendelea kubaki chuo.

Utabe wangu wa Azania O-Level maana nilitoka na div 1.12 na advance mzumbe div 1.8 haukuweza kunifanya nimudu masomo ya chuo.

Karibuni
Ulivuna ulichopanda
 
Daah yani kuna kipindi unasoma usipate sup yani inaitwa fighting for survivor ....tena na system ya Mzumbe ilivyo ..wanaziunganisha sup ya semester ya kwanza na ya pili if zikiwa 4 ..ndo kwaheri hiyo ...

Mu main campus .....wale wazee wa kupaki basi tunajuana 5-4-1 ndo formation yetu wana MU .....
Kupaki basi ndio ipoje hiyo?
 
Kaka UDOM kudisco ni kugusa tuu kama hutokua makini,nilienda na akili kama yako kwani rafiki angu alinambia udom bata ila baada ya kufika nijagundua si kweli nikakaza kinoma am still there ,kwa hawa wadogo zetu waje wasome wasidhani udom ni mchezo mchezo

Upo college gani na programme gani hapo UDOM?
 
Back
Top Bottom