Wale tulioanza maisha ya kujitegemea kigumu tukutane hapa

The Initiator huru

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
1,531
1,735
Kama kichwa cha habari kinavyosomeka, nimeanzisha huu uzi ili ulete hamasa kwa vijana ambao bado wanaishi makwao jinsi wengine tulivyo anza maisha ya kujitegemea kigumu.

Ipo hivi binafsi baada ya kuhitimu masomo ya chuo kikuu, nilienda kuishi kwa msela wangu ambapo mimi nilikua katika harakati za kutafuta kazi. Mungu sio athuman nilipata sehemu ya kujishikiza kwa kulipwa posho tu, lakini posho hiyo ilitosha kusukuma maisha, kwa ni hela hiyo hiyo nilitumia kwa msosi, umeme, na kuwasapoti ndugu.

Mshikaji yeye alikua hana kazi nae alikua anabangaiza akipata hela yeye anapiga gambe akawa ananitegemea kwa kila kitu nimsupport. Ilitokea kipindi tukagombana hivyo mimi nikaamua kuondoka, kiukweli sikua na pakwenda siku hiyo hivyo nilienda kutafuta gesti ya bei rahisi nikalala.

asubuhi ile kukucha ikanibidi niende job huku nikiwa ni mwenye mawazo lukuki. Hakika sitoisahau hiyo siku nilitafuta madalali tofauti tofauti na kuwaambia wanitafutie room, mawasiliano yote yalikua kwa simu.

Ilipofika sa kumi nilitoka kibaruani na kuanza kuzunguka na madalali, mpaka sa 12 jioni ndio napata room. Ilinilazimu kwenda kwenye ile gesti na kuchukua nguo zangu kisha kuhamia kwenye room yangu ambayo niliilipia 60,000 huku nikidaiwa 30,000 ili itimie kodi ya miezi 3 huku nikiahidi kumalizia iliyobaki baada ya wiki mbili.

Baada ya kuchukua nguo nilizitandaza chini baadhi nikapiga usingizi na kulipo kucha kabla ya kwenda job niliomba ruhusa ya kuchelewa kidogo kisaha nikaenda nunua godoro, ndoo, kashuka,pazia, kisi na kikombe kisha nikavipeleka kwenye room yangu.

Nililala chini takriban 4 months, cha ajabu wakati nalala chini nilipata mwanamke ambaye alikua akinyanyaswa na baba yake but before nilikua nishamtongoza, hivyo kilingana na alivyokuwa akinyanyaswa akaja tukaishi naye pamoja, tulilala chini naye kwa kama miezi mitatu hivi kama mume na mke kabla ya yeye kupata kazi mkoa mwingine na hivyo akaondoka.

hakika huyu mwanamke ameolewa but bado tunapendana sana kwani hata mimi nilishangaa sana mwanamke ambaye pamoja na uzuri wake alikubali kulala chini na mimi pasipo dharau ya aina yeyote.

Maisha ya kuwa na godoro peke yake na kulala chini yalinifanya muda wote room yangu kuwa imefungwa hata kama niko ndani na kuna joto. Baada ya miezi 4 ya kulala chini nilifanikiwa kununu kitanda, kapeti, radio ya sabufa kwa hela ambayo niliisave na kuwa na budget nzuri.

Baada ya kupata vitu vyote hivyo niliendelea kununua vitu kidogo kidogo mpaka room ikaja kujaa kabisa na nafasi ikawa finyu japo room ilikua kubwa sana.

Sasa angalau Mungu amebariki japo bado naendelea na harakati ya kuzisaka hela na kuisaidia familia yangu.

NB: Usikate tamaa hata siku moja jipe moyo utafanikisha malengo yako, usiogope kujaribu kufanya kitu au kulifanyia wazo lako kazi, kwa kuwa eti unaona hautaweza, wala usikubali kukatisha tamaa.

Enjoy the rest of the day

Asanteni (True Story)
 
Sio ufahari kulala chini. Tafuta hela wewe acha Julia-lia. Maisha mazuri yanatafutwa
 
Nasemaje jf itabaki kileleni coz inagusa wengi hivyo tu basii

Similar Discussions

Back
Top Bottom