Wale mliowahi kuagiza magari online

pole agent wako alikua kilaza..next time nambie nikupe agent,,,akikosea kwenye invoice submission tu umeliwaa
Hatukosea kwenye invoice kwa sababu custom value (CIF) haikuzidi CIF ya gari. Labda kama unazungumzia kuchakachua invoice ambayo bad isingesaidia. Custom Value (bei elekezi ya TRA) ilikuwa $2145, mie nililinunu kwa $1900.
 
pole agent wako alikua kilaza..next time nambie nikupe agent,,,akikosea kwenye invoice submission tu umeliwaa
Ile gari, bei elekezi ya TRA (custom value CIF) ilikuwa $2145, ushuru 4.1mil (bila registration) mie nililinunua kwa $1900. Je, unazungumzia kuchakachua invoice?
 
27a8ead64c2800e8be127e4d5aa8e795.jpg


Naomba kuuliza hizi bei Ni kweli?

Je utatibu wao Ni salama hauna utapeli?
Ni bei halali. Kuna nyingine mpaka unapata kwa $30-100. Jumlisha na bei ya kulisafirisha mpaka Bongo inafika $1000+. Kazi ipo hapo TRA.Wao hawajali umenunua gari kwa kiasi gani,hata kama umepewa bure ingiza details za gari husika kwenye Calculator ya TRA utapata bei ya gari kuwa barabarani
 
Mbona hizo bei ni sahihi tu ila hapo inabidi kuchagua bei with inspection na km utaamua hela kuwaeekea ktk acc yao ya tz iliyopo crdb utaongeza 40$ ya ku reprocess tt to japan na ushuru kulingana na tra calculator plus ghalama nyingine like 800k hapo gari itakuwa mkononi hii kampuni ya beforward ni uhakika haina ubabaishaji office zao kwa dar zipo opposite Ocean Road Hospital na cleaning wanafinya gari yako utaipokelea kurasini kamata kwenye car park yao
 
Beforward wapo vizuri sana na hawana ubabaishaji. Hizo bei unazoziona ni bei ya gari bila gharama za usafirishaji kufika Dar (FOB). Kumbuka hapo bado hujakutana na rungu la TRA. Hiyo ya USD 300 FOB mpaka unaiingiza barabarani hazipungui mil 7 mpaka 8 za kibongo
Uko sahihi kabisa
 
Maishani usipende kukimbilia vitu rahisi, vina gharama kubwa sana. Hilo gari ni takataka, nakushauri usilinunue, subiri ujipange,uagize gari.
 
27a8ead64c2800e8be127e4d5aa8e795.jpg


Naomba kuuliza hizi bei Ni kweli?

Je utatibu wao Ni salama hauna utapeli?
Hizo bei ni kweli, wala usiwe na wasi wasi nazo.. unaweza kwenda ofisini kwao iko mkabala na tigoshop ya ocean road hospital pale posta.. (kama unaelekea southern sun hotel)


Mimi ni kampuni changa, inayochipukia. Hivyo bei zangu ni chini zaid hata ya be forward


Kwangu, hio ya blue naweza kukuletea kwa Tshs 6,650,000 (mpaka barabarani kasoro bima)

Na hio ya silver Tshs 6,250,000 ( mpaka barabarani kasoro bima)

N.B ; NINAPOSEMA MPAKA BARABARANI, NAMAANISHA INAKUA IMEJUMLISHA GHARAMA ZOTE YAANI, CLEARING, PORT CHARGES, SHIPPING LINE.

MUDA WA KUFIKA NI WEEK 6 MPAKA 8.

KILA KITU TUNAANDIKISHIANA MKATABA KISHERIA.

KARIBU SANA.
 
Usijaribu weka mbali na watoto, utalia kama mtoto anavokunywa dawa chungu

wewe utakuwa dalali wa magari hapa mjini maana unavomtisha mwenzako unataka akutafute umtafutie gari bovu Zaidi umpige. acha hiyo

We unayetaka kuagiza through BEFORWARD agiza tu hakuna tatizo. hakikisha tu lina insurance, kuna gharama ya inspection na gharama ya transportation. kuhusu kodi na ushuru wa bandari chukua hiyo gharama yote ya gari pamoja na usafirishaji geuza katika hela za kitanzania halafu zidisha na 1.2 hivi itakupa kisio la hizo gharama litakapofika gari bandarini. halafu subiri miezi miwili
 
wapo sawa sema hapo ni bei ya gari na kulisafirisha mpaka dar, hapo ongezea na kodi utajua gharama yake mpaka linakufiikia kwako, jamaaa wapo sahihi, pia kama unatuma pesa tumia TT Na sio western union
TT ni nini kaka
 
Ile price ni insignificant. Yaani hata kama price ni $ 0.00 (maana kule gari likifika umri wa miaka mitano tangu litengenezwe irrespective of its condition halipaswi kuonekana barabarani) jitayarishe kulipa kiasi kama Tsh 8 million kama gharama kuLisa irisha hadi Dar (Tsh 2.5 million) na gharama za kodi mbali mbali za serikali ya Tanzania (si chini ya Tsh 5.5 million). Hako ka calculator kwenye website ya TRA katakupa rough estimate tu ya kodi utakazopaswa kulipa pale TRA. Bado kuna kodi za mamlaka zingine za serikali, mawakala wa bandarini pamoja na mamlaka yenyewe ya bandari na kadhalika.

Lakini mwisho wa yote utakuwa ume serve TSh 3 million au hata 5 million kama gari hilo ungalinunua kutoka kwenye show rooms za hapa Tanzania. Kwani hao wenye showrooms hizo nao hupitia utaratibu huo huo wa online purchase halafu wanaweka faida yao isiyopungua 50%. Ukikuta mwenye showroom anauza chini ya hapo basi ujue aidha huyo ni mkwepa kodi au ghari hiyo haina kiwango na itakusumbua baada ya muda mfupi. Kuepuka kutapeliwa katika manunuzi ya mtandaoni, nunua kutoka kwenye kampuni ambazo zinajulikana na zinazotumiwa na watanzania walio wengi ikiwamo hao wenye hizk car showrooms.
Umeeleza vizuri sana kaka.Pongezi kwako
 
Hizo bei ni kweli, wala usiwe na wasi wasi nazo.. unaweza kwenda ofisini kwao iko mkabala na tigoshop ya ocean road hospital pale posta.. (kama unaelekea southern sun hotel)


Mimi ni kampuni changa, inayochipukia. Hivyo bei zangu ni chini zaid hata ya be forward


Kwangu, hio ya blue naweza kukuletea kwa Tshs 6,650,000 (mpaka barabarani kasoro bima)

Na hio ya silver Tshs 6,250,000 ( mpaka barabarani kasoro bima)

N.B ; NINAPOSEMA MPAKA BARABARANI, NAMAANISHA INAKUA IMEJUMLISHA GHARAMA ZOTE YAANI, CLEARING, PORT CHARGES, SHIPPING LINE.

MUDA WA KUFIKA NI WEEK 6 MPAKA 8.

KILA KITU TUNAANDIKISHIANA MKATABA KISHERIA.

KARIBU SANA.
mkuu hebu nichanganulie Land lover Discovery 3
 
Hizo bei ni kweli,
Ila hakikisha zina INSPECTION FEES.
Pili hizo ni bei mpaka gari inafika bandarini dar es salaam,
Hapo kodi, hela ya clearing agent, hela ya bandari hujaweka bado.
Mkuu hiyo INSPECTION FEE wasipo weka inamadhara gani?
 
Back
Top Bottom