Wale mliowahi kuagiza magari online

Mjema Vushanje

Senior Member
Sep 24, 2017
159
353
27a8ead64c2800e8be127e4d5aa8e795.jpg


Naomba kuuliza hizi bei Ni kweli?

Je utatibu wao Ni salama hauna utapeli?
 
Kwakuwa hao BEFORWARD wana ofisi zao Dar esa Salaam na Mwanza kama sikosei, nenda uingie nao mkataba uwambie wakuletee hiyo gari uliyochagua utalipia ikifika Tanzania. Hapo utakuwa na uhakika zaidi. Kwa uzoefu wangu nimewahi kuagiza gari mara moja kutoka kampuni ya tradecarview, wale wana insurance policy ya hela zako. Hata hivyo sikupata tatizo lolote, gari ilifika salama kama nilivyooiona na kuichagua mtandaoni.
 
wapo sawa sema hapo ni bei ya gari na kulisafirisha mpaka dar, hapo ongezea na kodi utajua gharama yake mpaka linakufiikia kwako, jamaaa wapo sahihi, pia kama unatuma pesa tumia TT Na sio western union
 
Hizo bei ni kweli,
Ila hakikisha zina INSPECTION FEES.
Pili hizo ni bei mpaka gari inafika bandarini dar es salaam,
Hapo kodi, hela ya clearing agent, hela ya bandari hujaweka bado.
Oky roughly kama gari Ni ya $2000 hizo garama zingine zinaweza kuipaisha mpaka sh ngapi mpaka naondoka nayo?
 
Beforward wapo vizuri sana na hawana ubabaishaji. Hizo bei unazoziona ni bei ya gari bila gharama za usafirishaji kufika Dar (FOB). Kumbuka hapo bado hujakutana na rungu la TRA. Hiyo ya USD 300 FOB mpaka unaiingiza barabarani hazipungui mil 7 mpaka 8 za kibongo
 
Ile price ni insignificant. Yaani hata kama price ni $ 0.00 (maana kule gari likifika umri wa miaka mitano tangu litengenezwe irrespective of its condition halipaswi kuonekana barabarani) jitayarishe kulipa kiasi kama Tsh 8 million kama gharama kuLisa irisha hadi Dar (Tsh 2.5 million) na gharama za kodi mbali mbali za serikali ya Tanzania (si chini ya Tsh 5.5 million). Hako ka calculator kwenye website ya TRA katakupa rough estimate tu ya kodi utakazopaswa kulipa pale TRA. Bado kuna kodi za mamlaka zingine za serikali, mawakala wa bandarini pamoja na mamlaka yenyewe ya bandari na kadhalika.

Lakini mwisho wa yote utakuwa ume serve TSh 3 million au hata 5 million kama gari hilo ungalinunua kutoka kwenye show rooms za hapa Tanzania. Kwani hao wenye showrooms hizo nao hupitia utaratibu huo huo wa online purchase halafu wanaweka faida yao isiyopungua 50%. Ukikuta mwenye showroom anauza chini ya hapo basi ujue aidha huyo ni mkwepa kodi au ghari hiyo haina kiwango na itakusumbua baada ya muda mfupi. Kuepuka kutapeliwa katika manunuzi ya mtandaoni, nunua kutoka kwenye kampuni ambazo zinajulikana na zinazotumiwa na watanzania walio wengi ikiwamo hao wenye hizk car showrooms.
 
27a8ead64c2800e8be127e4d5aa8e795.jpg


Naomba kuuliza hizi bei Ni kweli?

Je utatibu wao Ni salama hauna utapeli?
Ni kweli na hakuna utapeli. Angalia gari, bei iwe CIF sio FOB, ingia website ya TRA angalia ushuru, badili iyo dollars kuwa shilingi, jumlisha na ushuru upate gharama kwa ujumla hadi gari inafika Tz.
 
kifupi,,bei utayonununulia ndo bei utayolipia kama kodi gari ikifika dar,,,
Sio kweli wakati wote. Mie hadi linafika ilikuwa 3.3mil, ushuru ulikuwa 4.3mil (ushuru+usajili). Tofauti ya milioni moja na hapo bado gharama za bandari.
 
Sio kweli wakati wote. Mie hadi linafika ilikuwa 3.3mil, ushuru ulikuwa 4.3mil (ushuru+usajili). Tofauti ya milioni moja na hapo bado gharama za bandari.
pole agent wako alikua kilaza..next time nambie nikupe agent,,,akikosea kwenye invoice submission tu umeliwaa
 
Back
Top Bottom