Wakati tuko Depo RTS Kunduchi, kipindi cha kwata kuna mkufunzi alikuwa anaitwa Ssgt Menyu alikuwa anaamuru platuni nzima ivue combat shirt, mnabaki na suruali ndio kwata linaanza, tulishamaliza kwata no.1 ya funga fungua. Tulikuwa kwenye kwata ya utembeaji, usimamaji na ugeukaji.Sasa huyu Ssgt Menyu alikuwa akitoa amri ya kutembea, sasa yale mausingizi ya wiki 6 na lile jua kali unakuta mtu anatembea huku amesinzia ngoma ina kuja pale anapoamuru platuni kuhalt,unapokosea yeye alikuwa hampigi yule aliyekosea, alikuwa anamshushia mabanzi ya mgongo mtu aliyekuwa nyuma ya yule aliyekosea huku akikuambia kwani wewe hukumuona.