halfcastmangi
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 391
- 1,007
Niseme tu wazi wengi tuliozaliwa kidogo 90 kurudi nyuma, 80, 70 aisee hii nchi imetutesa sana, ufukara ulikuwa wa kiwango cha juu sana, ukianza uvaaji wa viatu shida, chupi za VP, mafuta yalikuwa petroleum jelly tu, yani zao la kutoka ktk bidhaa ya petrol, ustaarabu ulikuwa bado sana, usafiri shida ile mbaya kabisa.
Watu walikuwa wanavuta sigara kama fashion, iwe kwenye basi, mgahawani au popote pale akiona watu anawasha manake ni fashion.
Viatu shida, kama ukipata sana unakuwa na araiyoo au ng'inyira, familia yenu ikiwa safi basi unapata chachacha, au kama wa kike utapata loso, zikaja zico n.k
Usafiri full tabu, basi likipita sahau lingine mpaka kesho yake, idadi ya waliosimama ni wengi kuliko walio na siti, mwaka 89 niliwahi safiri toka moshi mjini mpaka iringa mjini nikiwa nimesimama, basi la kampuni ya comfort la mchaga wa marangu, plate number MSB......
Yani mzee mkapa ashukuriwe mno na asamehewe madhambi yake.
Funza kuwa nazo haikuwa aibu manake ilikuwa kampeni mpaka mashuleni kutoana.