Kwa faida ya wote hasa vijana wa kileo ni hivi hapo zamani sehemu kubwa za miji mingi haikuwa na lami.
Barabara nyingi zilikuwa ni za vumbi. Sasa hawa funza walikuwa ni wadudu wadogo mithiri ya viroboto wanaokaa kuzunguka sehemu ya jicho la kuku hawa wakijificha ndani ya hilo vumbi la barabarani. Wewe ukipita tu hapo basi tayari unao!
Funza aliingia kidoleni pale sehemu ya chini au juu ya ukucha na kuweka himaya yake hapo. Usipomtoa anataga mayai yasiyo idadi na kuzaliana hapo.
Ukichelewa zaidi kumtoa yale mazalia yanaenea maeneo mengine ya mguu. Usipokaa sawa mguu unapinda kuelekea upande mmoja yani kama ni wa kulia utapinda kuelekea kulia na kama ni wa kushoto utaelekea kushoto. bdae unaweza ukashindwa kabisa kutembea.
Hawa funza walikuingia kama umepita sehemu yenye vumbi hasa vumbi lile laini sana bila kuvaa viatu vya kufunika. Yaani ukivaa ndala, sendo, kobazi lazma uondoke nao. Leo hii ukimuona mhenga aliyepinda miguu kuna uwezekano mkubwa alipitiwa na funza miaka hiyoo!
Leo hii kwa maeneo mengi funza wamebaki kuwa ni hadithi ya kale kwani walitokomea wenyewe tu. Hadi sasa hakujawa na maelezo rasmi ya nini kilichosababisha funza kutokomea.