Walalamikia kupokwa mamlaka

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
SERIKALI imesema kuanzishwa kwa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, hakujakiuka sheria ya serikali za mitaa inayosisitiza kupeleka madaraka kwa umma. Mkuu wa Habari, Elimu na Mawasiliano katika Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Zamaradi Kawawa, alisema hayo juzi mjini hapa kufuatia hoja za baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mabadiliko ya utumishi wa umma wilayani Biharamulo.

Baadhi ya washiriki walihoji ni kwa nini serikali imechukua tena majukumu ya kuajiri watumishi wa halmashauri, wakiwemo walinzi na maofisa watendaji wa kata.

Ofisa Utumishi Mwandamizi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Philemon Magessa, alisema hatua ya kuhamishwa kwa ajira na kupeleka serikali kuu, kumekiuka sheria Na.8 ya serikali za mitaa ya mwaka 2002 inayozipa halmashauri mamlaka ya kuajiri na kuwawajibisha watumishi.

Magessa alisema jukumu la kuajiri watumishi kurudishwa serikali kuu, kunazifanya halmashauri kukosa mamlaka juu ya watumishi wake, kwa kuwa mamlaka ya ajira si ya ngazi hiyo ya serikali.

Kwa mantiki hiyo, alisema hali hiyo inazifanya halmashauri kuwa wapokeaji na watekelezaji tu wa maagizo na uamuzi vinavyofanywa na serikali kuu.

Naye Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Biharamulo, Josephat Kamugisha, alisema uamuzi huo unaweza kuzifanya baadhi ya halmashauri kukosa watumishi, kwa kuwa mfumo wa sasa una upungufu mkubwa.

Kufuatia hoja hizo, Zamaradi alisema pamoja na ajira kufanywa na sekretarieti, halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji, zitaendelea kuwa na mamlaka juu ya watumishi watakaoajiriwa.

Alisema uamuzi huo wa serikali unalenga kuondoa upungufu uliokuwepo katika kutekeleza zoezi la ajira.

Aliongeza kuwa, lengo la serikali ni kuweka uwazi katika ajira pamoja na kupunguza udanganyifu uliokuwa ukifanywa na watu waliokuwa wakiajiriwa na kushindwa kuripoti katika vituo vya kazi.
 
Mkuu there has never been a willingness of the GoT to decentralize powers! Kuna kijana mmoja alifanya utafiti hapo chuo kikuu cha DSM na kukonclude kwamba mpaka hapo jamii ya WaTZ, madiwani, vyama vya siasa na taasisi za kirai zitakapo simama na kudai madaraka kwa umma, ugatuaji madaraka utabaki kuwa ndoto Tanzania.
 
kweli kazi ipo
Mkuu there has never been a willingness of the GoT to decentralize powers! Kuna kijana mmoja alifanya utafiti hapo chuo kikuu cha DSM na kukonclude kwamba mpaka hapo jamii ya WaTZ, madiwani, vyama vya siasa na taasisi za kirai zitakapo simama na kudai madaraka kwa umma, ugatuaji madaraka utabaki kuwa ndoto Tanzania.
 
Back
Top Bottom