Walalahoi wa Marekani

Ninavo jua mimi USA wako maskini wa kutupwa wengi tuu na wana zidi kuongezeka

Na US kwa sasa bado uchumi wao hauja kaa vizuri wataongezeka zaidi miaka ijayo
 
mkuu Tokyo, hivi fukara wa USA ana tofauti yoyote na huyu wa bongo?

Tofauti ipo. Wamarekani wanapata msaada zaidi kutoka serikali yao na jamii.

Karibu kila mji kuna sehemu unaweza kupata mlo mmoja au miwili bure. Makanisa mengi yanatoa msaada wa chakula na kuna vituo vya kuomba kazi.
Makampuni yanatoa misaada ya vyakula na kupeleka katika vituo kadhaa vya kutoa misaada (food bank).

Tatizo lipo kwenye mshahara. Mshahara ni mdogo kwa baadhi ya watu na raia wengi wapo mitaani hawana uwezo wa kulipa kodi ya nyumba na gharama nyingine za maisha.
 
Ninavo jua mimi USA wako maskini wa kutupwa wengi tuu na wana zidi kuongezeka

Na US kwa sasa bado uchumi wao hauja kaa vizuri wataongezeka zaidi miaka ijayo

Masikini wapo na matajiri wa kutisha wapo.

Nia yangu ni kuonyesha kuwa maisha ya Marekani siyo tu yale tunayoiona katika picha za Hollywood. Kuna watu wanaishi vizuri sana na wengine wanaishi kama wapo katika nchi masikini (Third World Country).
 
Masikini wapo na matajiri wa kutisha wapo.

Nia yangu ni kuonyesha kuwa maisha ya Marekani siyo tu yale tunayoiona katika picha za Hollywood. Kuna watu wanaishi vizuri sana na wengine wanaishi kama wapo katika nchi masikini (Third World Country).
Sawa na mimi nia yangu ni ku ongezea kuwa
USA ya sasi si kama ya zamani, umaskini utazidi zaid
Nadhan tuko pamoja
 


Lkn hiyo ndiyo iliyojaza military base Dunia nzima, ndiyo inayoguarantee usalama wa nchi tajiri kama Ujapani, Ujerumani, Korea Kusini wako USA ndiyo mlipaji mkubwa NATO, USA ndiyo anayepigana vita kwa ajili ya maslahi ya wachache kila siku kama hiyo hela yote USA wangewekeza kwa raia USA usingeona hao watu masikini wakilala br. na ndiyo D. Trump anachosema, akiingia huo ushenzi na ujinga wa Superpower wote STOP!

Ni aibu nchi tajiri namna hiyo watu kukosa maji ya kunywa, kuna Wamarekani wengi hawawezi hata kilipia Ada Chuo lkn nchi inajipiga kifua Dunia nzima!
 
Hilo wazi kipindi cha wakimbizi huko kagera kuna wazungu walikuwa wanapanga mojawapo ya nyumba yetu sasa kipindi mkataba wao unaisha na wanatakiwa kurudi USA dingi yetu alifurahi sana akijua nyumba yetu itabaki na mazagazaga kibao cha ajabu walibeba kila kitu mpk pasi tulishangaa!!Dingi akajitosa kumuuliza mmojawapo jamaa akajibu kuwa kule kwao si rahisi kununua salami hizi,shit! !!
 

Sorry,l mean samani not salami
 
Assets walizonazo hao walala hoi wa huko ni mwananchi wa kipato cha kati kwa Tanzania.
 
Ndio naelewa kwa nini kuna watu huko USA, wanamaliza hadi 10yrs, bila kugusa Tanzania, mbaya zaidi hata kuja kuzika wapendwa wanashindwa!
 
Assets walizonazo hao walala hoi wa huko ni mwananchi wa kipato cha kati kwa Tanzania.

Siyo kweli.

Mtanzania wa kipato cha kati anaweza kumudu maisha vizuri zaidi.

Kumbuka gharama za maisha yao ni makubwa zaidi yetu.

Mtanzania wa kipato cha kati anaweza kwenda kutembea Dubai na kupeleka watoto wake shule Afrika Kusini au Kenya.

Mlalahoi wa Marekani hawezi kusafiri hata mji jirani sembuse nje ya nchi.
Ukiwa mlalahoi huna asset.

Kama vitu vya matumizi ya nyumbani wananunua Walmart.
Walmart anaagiza China kwa sababu ni rahisi sana na ananunua kwa wingi.

Labda unaongelea asset nyingine.
 
Kwa hiyo mimi ndo nimekuwa mjadala? Laughable[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…