Wala watu wa Tsavo

Wala watu wa Tsavo

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,646
Wala-Watu wa Tsavo walikuwa Simba wawili waliojulikana sana kwa kuwala binadamu. Simba hawa walisababisha vifo vya idadi kubwa ya wajenzi wa Reli ya Kenya-Uganda , tangu Desemba,
1898.
57f68fcc4aa09a4ec105c9b6c1961986.jpg


HISTORIA

Mnamo Machi 1898, wakati wa ujenzi wa Reli ya Kenya-Uganda , mhandisi
John Henry Patterson aliongoza ujenzi wa daraja juu ya Mto Tsavo nchini
Kenya. Wakati wa ujenzi huu, wafanyikazi wengi wa India waliuawa na simba wawili wa kiume (Simba wa Tsavo ), ambao walivamia watu hemani mwao na kuwararua.

Wajenzi hawa walijenga maboma yenye kuta za miiba kuzunguka hema zao ili kuwaepuka wala-watu hawa; lakini simba hawa waliweza kujipenyeza. Patterson alijaribu mara kadhaa kuwawekea mitego na kuwafukuza usiku kutika mtini. Baaada ya majaribio mengi bila mafanikio, hatimaye alimpiga risasi mmoja wao mnamo 9 Desemba 1898. Wiki tatu baadaye, mnyama wa pili alipatikana na kuuawa. Idadi kamili ya watu waliouawa na wanyama hawa haijadhihirika. Wakati wa uhai wake, Patterson alitoa takwimu nyingi tofauti tofauti, moja ikikisia kwamba kulikuwa na waadhiriwa wengi, takribani 135.

Utafiti wa hivi maajuzi unaonyesha kwamba takwimu hizi zilikuwa takribani 35.
Patterson anaandika kuwa alimjeruhi simba wa kwanza akitumia risasi kutoka bunduki aina ya martini-Enfield .303. Risasi hii ilimpata katika miguu ya nyuma na akafanikiwa kutoroka. alirudi usiku akijaribu kumsaka Patterson hata alipojaribu kumwinda. patterson alimpiga risasi mara kadhaa akitumia bunduki ya .303 Lee Enfield, huku akimfuatilia keshoye na kumpata akiwa amefariki. Kwa ujumla, alimpiga risasi mara tano. Simba wa pili alipigwa risasi mara tano kwa kutumia bunduki ya .303 Lee Enfield, lakini bado aliweza kusimama na kujaribu kumsogelea kwa maumivu makali, ambapo alimpiga risasi mbili zaidi, moja katika kifua na ya pili kwa kichwa na akamuua. Anadai kuwa simba huyo alifariki huku akining'ini katika taga la mti lililoanguka, bado akijaribu kumfikia Patterson.

Baada ya kutumika kwa miongo miwili na nusu kama matandiko ya Patterson, ngozi za simba hao ziliuzwa kwa
Musiamu ya Uwanjani ya Chicago kwa jumla ya Dola za Marekani 5,000. Simba hao walifika kwa Musiamu katika hali mbaya. Walijengwa upya na sasa hivi wako katika maonyeshho ya kudumu pamoja na viwiliwili vyao. Simba waliopandikwa hapo wako na kipimo kidogo kuliko unene wa kutisha ambao Patterson anausimulia, pengine kwa kuwa Patterson alidanganya juu ya unene huo, au kwa sababu walikuwa wamepunguzwa ili kutumika kama matandiko ya Kombe nyumbani mwa Patterson.



Masimulizi ya Patterson yalichapishwa katika kitabu chake cha 1907, The Man-Eaters of Tsavo .


UTAFITI WA KISASA.


Sampuli za wanyama hawa wawili katika Musiamu ya Chicago wanajulikana kama FMNH 23970 (aliyeuawa Desemba 9) na FMNH 23969 (aliyeuawa 29 Desemba). utafiti wa hivi maajuzi umefanya kutokana na uchambuzi wa sahii ya Kiisotopia (Isotopic Signature ) mabadiliko ya
Carbon-13 (Δ13C ) na Nitrogen-15 katika collagen ya mifupa yao na
keratin katika nywele yao. Kwa kutumia makisio kuwa binadamu walioasiriwa walikuwa na kilo 20 za nyama ya kulika pamoja na hati tofauti za kiisotopia (Isotopic Signatures ) za nyama ya binadamu ikilinganishwa na windo la kawaida la simba, uchambuzi huu unakisia kuwa FMNH 23969 alikula kiwango cha watu 10.5 na FMNH 23970 akala kiwango cha binadamu 24.5. [4] Takwimu hizi zinatoa idadi ya waasiriwa 35 ambayo Patterson alikuwa amedai kuwa 135..


Vyanzo Vilivyokisiwa Kuchangia Ulaji wa Binadamu




Madhanio mbalimbali kuhusu tabia ya ulaji watu yamepitiwa na Kerbis Peterhans na Gnoske (2001) na Patterson (2004). majadiliano yao yanajumuisha yafuatayo:


1.Kuzuka kwa maradhi ya Nagana mnamo 1898 yalipunguza windo la kawaida la simba, wakilazimishwa kutafuta pato jingine la chakula.
Simba wa Tsavo wanaweza kuwa walizoea kuwapata watu waliokufa wakivuka Mto Tsavo . Wafanyi biashara ya kuuuza watumwa waliojikita
Uunguja walikuwa wakivuka mto huo mara kwa mara.


2.mila ya Wajenzi wa reli wa dini ya
Hindu ya kuwatupa wafu baada ya kuwachoma ilipelekea simba hao kuwala wafu hao.


3.Madai mengine ni kuwa simba wa kwanza alikuwa na jino lililoumia sana na hili linaweza kuwa lilikandamiza uwezo wake wa kutafuta windo la kawaida, kwa hivyo akawageukia binadamu. Ushahidi kuhusu madai haya umeonyeshwa katika karatasi zilizopitiwa kwa undani na Neiburger na Patterson (2000, 2001, 2002)na pia katika kitabu cha Bruce Patterson (2004)
Utamaduni Uliofana
Kitabu cha Patterson kilitumiwa kama msingi wa filamu Bwana Devil (1952) na The Ghost and the Darkness (1996) ("The Ghost" na "The Darkness" ni majina waliyopewa Simba hawa wawili wala-watu).



=THE MONK WHO SOLD HIS FERRARI
 
Kuna idea nyingine kwamba hawa simba walikuwa wa mchongo .. Yaani walikuwa wa nguvu za giza kutoka kwa wazee wetu ambao walikuwa wanapinga ujenzi wa reli ile , so sokomoko zima lilikuwa ni LA kufifisha juhudi za ujenzi wa reli not to advance into hinterlands of Kenya
 
Back
Top Bottom