Sio kila ililotendwa na wayahudi au waarabu liwekwe kwenye uhalali wa dini husika, mengine ni ya kimila zao tu, ni ujinga kuiga hadi mavazi, vyakula, kulala au kuongea ama salamu zao, ni kutokuzijua kweli tu. Unadhani Mtume Muhamadi angezaliwa umasaini waislamu wangevaaje ? Halali ingekuwa ng'ombe, mbuzi na kondoo tu hata kuku haramu. Waarabu walivaa wavaavyo sasa tangu kizazi cha midle persians cha miaka mia 9 kabla ya Yesu. Yesu na mamake hata madafu sijasikia kama walishawahi kuyala achilia mbali ngamia na kambale. Kama wanajamii wa kwao walikuwa na mapokeo yao toka kwa mababu zao kulingana na mila zao zilizotokana na mazingira yao husika mi hayo hayaniusu kabisa,Mungu ni wa wote, hawezi kumtenga mmasai kwa mavazi yake yanayomfaa kwa mazingira na shughuli zao.