Ntale Wi Isumbi
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 480
- 127
wakati wa chama chashika hatamu, ukuu wa wilaya ulikuwa ni cheo cha mtu wa dalasa la saba waliohitimu Hombolo au handeni. sijui siku hizi kigezo ni kipi!
halafu chuo cha mzumbe, mkoloni alikuwa nakitumia kuwafunza watumishi wa serikali na wanafunzi wengine, kuja kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, ndio maana kilikuwa kinaitwa chuo cha uongozi-Mzumbe. sasa leo watu wanateuliwa kuwa wakuu wa wilaya bila ya hata , ujuzi wa how to spend, development and recurrent fund, wewe unategemea nini hapo? ukuu wa wilaya ni vyeo nyeti sana kuliko hata ukuu wa mikoa. kwa sababu huko wilayani ndiko kwenye vijiji vingi sana na wakazi walio wengi ni masikini. sasa mkuu wa wilaya sifa zake kubwa ni mojawapo ya kujua , how to eradicate povety(kupambana na umasikini), how to create jobs, how to improve infrastuctures and peoples' wellbeing. kama serikali haitazingatia sifa hizo inapoteua wakuu wa wilaya, basi itakuwa inawafukuza wakuu wa wilaya kila mwezi!
MY take: ukuu wa wilaya kiwe cheo cha kufanyiwa interview mtu na sio okotaokota tuu bora kasoma!!!
Binafsi siungi mkono na sioni sababu ya kuendelea kuwa na wakuu wa wilaya. Kimsingi, ukuu wa wilaya ni kazi ambayo haielewiki sifa na majukumu yake. Moja, uliwahi kuona au kusikia wapi kazi ambayo mtu wenye kiwango chochote cha elimu ana qualify na anateuliwa kuifanya? Pitia tu haraka haraka orodha ya wakuu wa wilaya utaona kuna kuanzia mhitimu wa drs la saba hadi mwenye shahada ya uzamivu (PhD), kuanzia mwalimu wa shule ya msingi hadi professa wa chuo kikuu, kuanzia cruta wa jeshi hadi meja jenerali (mstaafu?) n.k. wote ni wakuu wa wilaya!
Pili, kuhusu kazi na majukumu yao, kimsingi kuna mwingiliano usio kuwa wa lazima kati ya ofisi ya mkuu wa wilaya na ofisi ya wakurugenzi wa halmashauri. Kwa hali ya sasa, tuna ofisi 2 za utawala na utendaji (ofisi ya mkuu wa wilaya na ofisi ya mkurugenzi) kwenye ngazi moja. Au kwa lugha nyingine niseme parallel structures at the same administrative level. Kazi zote zinazofanywa na mkuu wa wilaya, DAS na timu yake, zinapaswa ziwe chini ya DED ili kuondoa mwingiliano huu na kuwa na ngazi moja ya utawala na utendaji. Kisheria, majukumu yote uliyotaja hapo juu yamekasimiwa kwa mamlaka za serikali za mitaa ambazo ni halmashauri za majiji, miji, manispaa na wilaya (rejea Local Government Act ya mwaka 1982 na 1983, na marekebisho yake ya mwaka 1999) na sio kwa mkuu wa wilaya. Kwa kifupi, hayo majukumu wanapaswa kufundishwa wakurugenzi na watendaji wengine katika halmashauri na sio wakuu wa wilaya!
Tatu, baada ya serikali kuona DCs hawana kazi ya kufanya ikaamua kuanzisha District Consultative Council (DCC) ambayo mwenyekiti wake ni DC na katibu ni DED. Hata hivyo, DCC haina nguvu ya kisheria ya kupanga na kupitisha bajeti bali kutoka ushauri tu. Chombo chenye mamlaka hayo ni baraza la madiwani. Uzoefu pia unaonyesha kuwa, sehemu nyingi DCs ni chanzo kikubwa cha migogoro maana hawana mafungu na wanaingilia utendaji wa wakurugenzi kwa matakwa ya kisiasa. Jukumu pekee walilo nalo ni la uenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama za wilaya, kazi ambayo pia inaweza kufanywa na meya au mwenyekiti wa halmashauri kama tutaboresha sifa (elimu, uzoefu n.k.) na namna ya kuwapata viongozi hawa.
Nne, kibaya zaidi DC ni mwanasiasa (kada wa ccm) na mtumishi wa umma anayetekeleza majukumu yake ya kiasasa na kiutendaji kwa kutumia rasilimali za serikali (sio za chama chake). Kwa lugha nyingine, mfumo wetu una waajiriwa wa serikali wanaolipwa mishahara na serikali ili kufanya kazi za ccm! Kwa sababu ya legacy ya mfumo wa chama kimoja na chama kushika hatamu, bado tuna watendaji wengi wa namna hiyo, ingawa hili la wakuu wa wilaya liko wazi zaidi bila kificho chochote.