Mwenye Job discpription ya wakuu wa wilaya na mkoa tafadhari, hadi sasa sijajua hua wanaenda ofisini kufanya nini, ni kama makamu wa kwanza wa rais, nae pia hua sielewi hasa ofisini hua anafanya nini though huyu akitoka ofisini atleast hua anamkasi wa kukatia utepe.
Ebu tuanze na majukumu yaliyomo ndani ya serikali za mitaa kama sheria zinavyoanisha and then tutakwenda katika serikali kuu.Sababu,kwa utendaji wa serikali za mitaa na ule wa serikali kuu unafanyika katika maeneo yale yale hivyo inapasa kuwa na upeo wa kutosha kuhusu mgawanyo wa majukumu kwa ngazi tatu,yaani wizara,mkoa na wilaya
MADARAKA YA WAZIRI MWENYE DHAMANA YA SERIKALI ZA MITAA
kwa mujibu wa kifungu namba 4 vya sheria namba 7 na 8 za mwaka 1982,majukumu ya waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa ni kuhakikisha kwamba mamlaka zote za serikali za mitaa zinajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.Uwezo huo wa serikali za mitaa unaangaliwa katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha,utumishi,usimamizi wa sheria na nidhamu.
MADARAKA YA MKUU WA MKOA
Kifungu cha 5(3) cha sheria za tawala za mikoa Namba 19 ya mwaka 1997 kinaeleza wajibu wa mkuu wa mkoa kwa mamlaka ya serikali za mitaa ni kuziwezesha na kuzijengea mazingira ya kutekeleza majukumu yao ya kisheria.Dhana hii ya uhuru wa mamlaka ya serikali za mitaa inaegemea katika sharti kuwa,mamlaka hizi zitakuwa zinajiendesha kisheria.Lakini pale itakapobainika kuwa sheria haifuatwi,basi uhuru huo hautalindwa,bali serikali kuu ikiwa ni pamoja na mkuu wa mkoa itaingilia kati kuona kuwa sheria zinatekelezwa.Msingi huu wa fikra ndiyo uliosababisha kumpa mkuu wa mkoa uwezo wa kuingilia au kuwaruhusu maofisa wa serikali kuu kuchunguza nyaraka pamoja na kumbukumbu nyingine za fedha za mamlaka ya serikali za mitaa.Lengo ni kutaka kugundua endapo kuna ukiukwaji wa sheria au kanuni za fedha.Hatua hizi ni kwa mujibu wa kifungu cha 44 cha sheria ya fedha za serikali za mitaa namba 9 ya mwaka 1982.Kifungu cha 78A cha sheria namba 8 ya mwaka 1982,Kinampa mkuu wa mkoa madaraka ya kusimamia utekelezaji wa sheria za mamlaka za serikali(Mamlaka za Miji),ikiwa ni pamoja na kuchunguza uhalali wa vitendo na maamuzi ya mamlaka hizo na kumuarifu waziri ikiwa kuna ulazima wa kuingilia kati endapo vitendo na maamuzi vinakiuka misingi ya sheria.
MADARAKA ya MKUU WA WILAYA
Kifungu cha 14 cha sheria za tawala za mikoa namba 19 ya mwaka 1997,kinampa mkuu wa wilaya majukumu ya kuziwezesha na kuzijengea mazingira mazuri mamlaka za serikali za mitaa zilizomo ndani ya eneo lake ili ziweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.Aidha kifungu cha 78A cha sheria namba 8 ya mwaka 1982,kama ilivyo kwa mkuu wa mkoa,Vimetoa uwezo wa mkuu wa wilaya kuchunguza uhalali wa vitendo na maamuzi ya Mamlaka ya Serikali za mitaa katika eneo lake.
Mkuu huyo anatakiwa kumjulisha waziri mwenye dhamana ya serikali za Mitaa ikiwa kuna ukiukwaji na uvunjaji wa sheria na kanuni za nchi katika utekelezaji wa majukumu na maamuzi ya mamlaka za serikali za mitaa.Mkuu wa wilaya atakuwa mwenyekiti wa kamati ya ushauri ya wilaya(DCC)
NOTE: Hii ni kwa upande wa serikali za mitaa,kwa upande wa serikali kuu nitakupostia nikipata nafasi