Wakuu wa Wilaya kubadilishwa

Wakuu wa Wilaya kubadilishwa

Mlaleo

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
16,379
Reaction score
13,193
Kuna tetesi za ndani nimesikia kutakuwa na mabadiriko ya wakuu wa wilaya nchi nzima wengine watatoka na wengine watapangiwa sehemu zingine hii ni kutokana na wengine kushindwa kumudu nafasi walizoteuliwa.
 
Kwa hiyo inawezekana uteuzi huu ambao mapendekezo aliyafanya prince wamechemsha ni tatizo la kupeana madaraka kwa urafiki.
 
Kuna tetesi za ndani nimesikia kutakuwa na mabadiriko ya wakuu wa wilaya nchi nzima wengine watatoka na wengine watapangiwa sehemu zingine hii ni kutokana na wengine kushindwa kumudu nafasi walizoteuliwa......
wakati wa chama chashika hatamu, ukuu wa wilaya ulikuwa ni cheo cha mtu wa dalasa la saba waliohitimu Hombolo au handeni. sijui siku hizi kigezo ni kipi!
halafu chuo cha mzumbe, mkoloni alikuwa nakitumia kuwafunza watumishi wa serikali na wanafunzi wengine, kuja kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, ndio maana kilikuwa kinaitwa chuo cha uongozi-Mzumbe. sasa leo watu wanateuliwa kuwa wakuu wa wilaya bila ya hata , ujuzi wa how to spend, development and recurrent fund, wewe unategemea nini hapo? ukuu wa wilaya ni vyeo nyeti sana kuliko hata ukuu wa mikoa. kwa sababu huko wilayani ndiko kwenye vijiji vingi sana na wakazi walio wengi ni masikini. sasa mkuu wa wilaya sifa zake kubwa ni mojawapo ya kujua , how to eradicate povety(kupambana na umasikini), how to create jobs, how to improve infrastuctures and peoples' wellbeing. kama serikali haitazingatia sifa hizo inapoteua wakuu wa wilaya, basi itakuwa inawafukuza wakuu wa wilaya kila mwezi!

MY take: ukuu wa wilaya kiwe cheo cha kufanyiwa interview mtu na sio okotaokota tuu bora kasoma!!!
 
Mimi hata hawanisaidii chochote..Nawaona kama vivuli tu!! any way naona prince kwa sasa cm itakuwa bize sana!
 
Ni madaraka yanayoongeza gharama tu kwa walipa kodi.
 
Bora wafutwe wote na wale wa mikoa tubane matumizi. Vinginevyo tutegemee LeMutuz, Gumbo, Shoza, Mwambapa, Ritz, Faiza Foxy, na more Lumumba guys
 
Kuna tetesi za ndani nimesikia kutakuwa na mabadiriko ya wakuu wa wilaya nchi nzima wengine watatoka na wengine watapangiwa sehemu zingine hii ni kutokana na wengine kushindwa kumudu nafasi walizoteuliwa......

Hili si ni jambo la kawaida?
 
Kuna tetesi za ndani nimesikia kutakuwa na mabadiriko ya wakuu wa wilaya nchi nzima wengine watatoka na wengine watapangiwa sehemu zingine hii ni kutokana na wengine kushindwa kumudu nafasi walizoteuliwa......

Hii tunaita kuyatembea maneno..."walk the talk"....wakuu wa wilaya watarudishwa wanajeshi (makapten na usalama wa taifa) ili ku'monitor' wahamiaji haramu! Hizi ni jitihata za kawaida hasa nchi inapokuwa katika mazingira ya kuwa vitani muda wowote kama ilivyo hivi sasa! Mnaweza nikosoa kama nimepotoka! Unapokaa mwingine tu wala hujua mbinu za adui hata namna ya ku'mobilise watu inakuwa ni shida! Nipo pamoja nawe raisi wangu! MAwifi na mashemeji waliopo wilayani kwa sasa hawatufai kwa hili!
 
Wote hapo mnatamani hizi nafasi mtazipataje poor nyie poleni
 
Tunasubiri tuone kama Ahmed Kipozi atatemwa maana wamepiga deal la ardhi Bagamoyo big time!watumishi wengine wa halmashauri na chama wamesimamishwa!yeye anasubiria lolote kutoka juu!lakini sintashangaa maana serikali ya kishikaji!
 
Kuna tetesi za ndani nimesikia kutakuwa na mabadiriko ya wakuu wa wilaya nchi nzima wengine watatoka na wengine watapangiwa sehemu zingine hii ni kutokana na wengine kushindwa kumudu nafasi walizoteuliwa......

Katiba mpya ingeondoa kabisa hii nafasi!!! Moja ya njia mbaya za matumizi ya pesa ya mlipa kodi tuu
 
Back
Top Bottom