Wakuu wa mikoa taarifa zenu zitaje pia changamoto zilizopo

Wakuu wa mikoa taarifa zenu zitaje pia changamoto zilizopo

EMACHA

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
955
Reaction score
1,776
Tangu juzi tumeona Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali ikiwaleta Wakuu wa Mikoa kueleza kilichofanyika katika mikoa yao katika kipindi cha miaka minne ya uongozi uliopo madarakani.

Ni wazi kuwa katika kila mafanikio changamoto hazikosekani. Sasa mimi hupenda kufuatilia mawasilisho hayo, lakini ajabu hakuna anayeeleza mapungufu yaliyopo. Kweli Mkuu anaposema kila kitu kipo sawa na maisha ni mazuri, aaah...hajatutendea haki.

Ni wazi mafanikio ni mengi na mazuri yamefanywa na serikali yetu. Lakini hii haijawanyima fursa ya kusema wapi tumekwama na wapi tunapungukiwa ili parekebishwe.

Nachelea kila Mkuu akija akasema mambo yote kwake ni safi, sasa tunaenda kuuza sera gani kwa uchaguzi ujao?
Labda mi ndiye mjinga sielewi kinachoendelea!
 
Back
Top Bottom