Shida na raha
JF-Expert Member
- Aug 8, 2014
- 3,773
- 3,471
Wakuu kwa mfano umepata safari ya kwenda nchi nyingine wakati huo huku Tz umeacha mchumba ambaye ana ujauzito, ghafla unarudi ameshajifungua, kwa ham na shauku unamtafuta kwenda kujua wapi alipo kwasababu kipindi upo kule mawasiliano hayakuwepo kati yenu. Dini zenu ni tofauti ghafla unamkuta mtoto kamuita jina ambalo hulitaki na yeye akawa anang'ng'nia hilo hilo. Kumbuka hapo mahusiano yamesharudi kama awali na umempa fidia ya kipindi chote ulichoondoka. Sasa nakuja na swali je wewe utakua una power au yeye ndo mwenye power? Samahani kwa kuwachosha maelezo yangu kama hayakufahamika.