Wakuu msaada wenu, bado sijapata kazi

faru joni

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
478
733
Nililetaga nyuzi yangu mwaka jana ilisomeka ivi



Habarini za jioni, poleni na miangaiko ya hapa na pale kuakikisha tunajenga familia na nchi kwa ujumla...

Kwa wale wanaouguza na kuugua nawapa pole na nawaombea kwa muumba mbingu na nchi awaponye nyote na mrejee kwenye hali nzuri ili kuendeleza majukumu yenu
.
.
Niende kwenye maada moja kwa moja
.
.
Yapata week moja na kidogo tangu nilete uzi wangu wa kuomba watanzania wanisaidie nafasi ya kazi yeyote ile
.
.
Wengi walinibeza ( nawashukuru coz ni sehemu ya maisha pia) kunitolea kauli chafu na wengine walinitia moyo (nawashukuru pia)
.
.
Ndugu zangu, watanzania wenzangu nakuja tena mbele yenu naombeni mnisaidie sehemu yeyote ya kujishkiza au nafasi yeyote ya kazi nipo chini ya miguu yenu
.
.
Nimefanya sana application pasipo mafanikio yeyote yale
.
.
Mpaka nahisi kukata kabisa tamaa na aya maisha...
.
.
Kila siku naamini labda zamu yangu bado, ila ndio jua kwangu linazama maana umri nao unanitupa moon I
.
.
.
Elimu yangu: Degree ya Compute Security (Bsc in cyber security)

Napatikana: Dar es Saalam

Namba yangu ya simu: 0755-836-347

Nipo chini ya miguu yenu watanzania wenzagu aombeni msaada wenu ndugu zangu, watanzania wenzangu.

Nimechoka kulia peke yangu, naomba niwalilie ninyi ndugu zangu mnisaidie.

Asante pia kwa kuchukua muda wako kusoma andiko langu

Mungu awabariki sana sana.

Note: BADO SIJAPATA KAZI WANA JF NAOMBENI MSAADA WENU NDUGU ZANGU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ungesema hata kazi mnazofanya wengi wataelewa
E.g: ni kuprotect website,app au Organization systeam isi be harked,
 
Write your reply...Nenda pale kariakoo maduka ya simu,waombe vijana mafundi simu ili wawe wanakupa "deiwaka" ya kutengeneza simu kubali kupewa chochote imradi upate uzoefu!! hata ukipewa nauli shukuru ili kesho urudi tena!! Acha kulia lia msomi mzima.
 
Hutaki ata kutembeza Maji mtaani walau upate hela ya kula unabaki kulia lia, Rudi kijijini ukapige jembe, Ni aibu apa mtoto wa kiume kuja kusema eti umechoka kulia mwenyewe, Ww unafikiri wote tuliopo mjini tuna Bachelor degree sijui Masters degree, Mbona hatuna na Watoto wanakula, Wanavaa na chooni wanaenda sasa endelea kuulamba hutaki kuchafuka ukitembeza biashara mpaka siku ulale njaa ndio akili ikukae
 
Usikate tamaa.

Mambo mazuri hayataki haraka.

Ukiwa unasubiri Michongo ya Kazi.

Jaribu hata Biashara ndogo ndogo kukidhi mahitaji yako ya hapa na pale
 
Write your reply...Nenda pale kariakoo maduka ya simu,waombe vijana mafundi simu ili wawe wanakupa "deiwaka" ya kutengeneza simu kubali kupewa chochote imradi upate uzoefu!! hata ukipewa nauli shukuru ili kesho urudi tena!! Acha kulia lia msomi mzima.
Nakuunga mkono kwa hoja yako mkuu, nakumbuka miaka ile nipo kitaa sina mia nyekundu na degree isiyo na manufaa kwa wakati ule ikabidi nijiongeze. Nikaanza kwanza kua fundi simu mtaani kibishi nkawa nkiletewa simu ikinishinda napeleka kariakoo kwa wanangu wanaitibu kwa bei chee in short nlikua dalali wa fundi simu. Nikahamia kwenye computers especially laptops both hardware na software ila nlikua mtamu sana software. Mpaka napata kazi ya profession yangu tayari nishakua fundi expert na mpaka now laptop ikinishinda kutengeneza kaitupe tu haitapona tena. Huyo mkuu hapo juu kwa profession yake ya cyber security atachina kusubiri kazi rasmi. Aanze kua fundi computer ataingiza hela na anaweza kusahau kuajiriwa tena, aende Machinga Complex floor ya pili upande wa kushoto kwa mafundi computer amtafute jamaa mmoja anaitwa "MADATA" jamaa ni mkarimu sana atamsaidia kwenye ofisi ya kujishikiza... Kikubwa usharobaro na ujuaji aweke pembeni kabisa kule aanze moja
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom