Nasema hivyo kwa sababu nyuma nilikuwa napata vitu free kabisa sasa siku moja nikaona thread moja humu ikielezea kuhusu codes zinazoongeza channels na kuangalia free, aisee nikajitia kiherehere nilivyozaja nikakatiwa zooote ..nilihangaika wee nika nikawa nachange freq wapi! Ila baadae ikakubali lakini zikaonesha chache. Baada ya siku kadhaa zikakata tena ikabidi nilipie tu Hamna namna, sasa hapa kifurushi kimeisha na nikiwaza nyuma nilikuwa nakula vitu bure nafikiria nikifanya maujanja either unaweza rudishiwa kama zamani Ila imani sina kabisa kama itawezekana maana card washaijua tayari... Hapa nimescan zinaonesha channel 3 tu zile mpya, kungfu plus, novela plus na movie plus