Wakurugezi wa Halmashauri ni mchwa. Uangaliwe utaratibu mpya wa kuwapata

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,400
4,074
Wakati umefika wa kuangalia utaratibu mpya wa kuwapata Wakurugenzi wa hizi Halmashauri. Utaratibu wa kuwateua upo kisiasa sana ili kuisaidia CCM wakati wa chaguzi mbalimbali lakini kiuchumi ni hasara sana kwani wanapiga pesa nyingi za miradi na makusanyo ya hizi halmashauri.

Hivi karibuni Waziri Mkuu alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa ubadhilifu wa mamilioni ya fedha na leo kamsimamisha Mkurugenzi wa jiji la DSM kwa ubadhilifu wa shilingi bil.10

Ushauri

Wakati umefika wa kuwapata hawa Wakurugenzi kwa kutangaza nafasi watanzania wenye sifa waombe ili wapatikane wakurugenzi wenye uwezo na elimu ya mambo ya fedha na uchumi na kuachana na huu utaratibu wa kuwateua utaratibu ambao upo kwa manufaa ya kisiasa wakati wa chaguzi mbalimbali zinazifanyika
 
Kula bia wewe acha mboyoyo
 
Attachments

  • IMG_20220711_232714.jpg
    IMG_20220711_232714.jpg
    2 MB · Views: 5
Mkurugenzi aajiriwe na halmashauri tena kwa ushindani! Na awe anapangiwa vha kufanya na baraza kuanzia kukusanya mpaka kutumia pesa.

Hii ya mkurugenzi kuchaguliwa na Rais na wengi wao ikiwa ni walie walioshindwa michakato ya kupata wabunge chama fulani, unamfanya mkurugenzi kuwa mwajibikajo kwa Rais tu!! Yeye ndio anaamua atafanya nini na pesa anazokusanya!!

Raisi hawezi kuwa anawajibisha mawaziri, majaji, manaibu waziri, makatibu wakuu, wakuu wa vyombo vya usalama, wakurugenzi wa mashirika ya umma, wenyeviti wa bodi wa mashirika ya umma, wakuu wa majeshi, wakuu wa mikoa, wakuu wa willaya, RAS na DAS wa mikoa na wilaya, wakurugenzi!! Hata kama Rais angekuwa mchapa kazi haswaaa - kuangalia watu wote hawa sio jambo rahisi!!
 
Wakati umefika wa kuangalia utaratibu mpya wa kuwapata Wakurugenzi wa hizi Halmashauri. Utaratibu wa kuwateua upo kisiasa sana ili kuisaidia CCM wakati wa chaguzi mbalimbali lakini kiuchumi ni hasara sana kwani wanapiga pesa nyingi za miradi na makusanyo ya hizi halmashauri.

Hivi karibuni Waziri Mkuu alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa ubadhilifu wa mamilioni ya fedha na leo kamsimamisha Mkurugenzi wa jiji la DSM kwa ubadhilifu wa shilingi bil.10

Ushauri

Wakati umefika wa kuwapata hawa Wakurugenzi kwa kutangaza nafasi watanzania wenye sifa waombe ili wapatikane wakurugenzi wenye uwezo na elimu ya mambo ya fedha na uchumi na kuachana na huu utaratibu wa kuwateua utaratibu ambao upo kwa manufaa ya kisiasa wakati wa chaguzi mbalimbali zinazifanyika
Ndio maana tunahitaji katiba mpya
 
Sisi tuchague wabunge, ndani ya bunge wapige kura ya uraisi,maoni yangu kwenye katiba mpya.
 
Mkurugenzi aajiriwe na halmashauri tena kwa ushindani! Na awe anapangiwa vha kufanya na baraza kuanzia kukusanya mpaka kutumia pesa.
Hii ndiyo njia nzuri na muafaka zaidi kudhibiti wizi wanaoufanya. Akiajiriwa na halmashauri, halmashauri yenyewe itamsimamia na kudhibiti utendaji kazi wake. Akishindwana na mwajiri wake anatupiwa virago .
 
Wakati umefika wa kuangalia utaratibu mpya wa kuwapata Wakurugenzi wa hizi Halmashauri. Utaratibu wa kuwateua upo kisiasa sana ili kuisaidia CCM wakati wa chaguzi mbalimbali lakini kiuchumi ni hasara sana kwani wanapiga pesa nyingi za miradi na makusanyo ya hizi halmashauri.

Hivi karibuni Waziri Mkuu alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Arusha kwa ubadhilifu wa mamilioni ya fedha na leo kamsimamisha Mkurugenzi wa jiji la DSM kwa ubadhilifu wa shilingi bil.10

Ushauri

Wakati umefika wa kuwapata hawa Wakurugenzi kwa kutangaza nafasi watanzania wenye sifa waombe ili wapatikane wakurugenzi wenye uwezo na elimu ya mambo ya fedha na uchumi na kuachana na huu utaratibu wa kuwateua utaratibu ambao upo kwa manufaa ya kisiasa wakati wa chaguzi mbalimbali zinazifanyika
Kosa kubwa alifanya Rais mwenyewe, pale alipotoa "green light" kuwa wanaweza kula kwa urefu wa kamba zao!🥺

Matokeo yake ndiyo hayo, kila siku Waziri Mkuu atakuwa anafanya Kazi moja tu, kuwasimamisha Kazi!

Alianza pale Arusha kumsimamisha Kazi Mkurugenzi, ambaye anaendelea kusota Gerezani na hivi sasa Mkurugenzi wa Dar!

Who is next?

Tatizo ni mfumo, kila kitu anateua Rais, tena anateua wanaccm kindakindaki!

Bila kupata Katiba mpya, nchi yetu itafilisika, kama ilivyofilisika Sri lanka, na hatimaye wananchi wataamua kwenda kufanya "selfi" Ikulu!🥺
 
Na ukute ili waziri mkuu aende kwenye tukio kama hilo si ajabu mpaka aongee na mhe rais ampe maelekezo.
 
Absolutely true

Yaani hii Katiba ya sasa ni uozo mtupu!🥺

Halafu unakuta wanaccm wanasema wananchi Wana mahitaji ya maji safi, Katiba siyo Kipaumbele chao kwa sasa!
 
Ni wakati wa kudai Katiba Bora, tuwe na taasisi na mifumo imara.
 
Back
Top Bottom