Sherehe kubwa itakayowakutanisha Watanzania kutoka Kabila la Wangoni inakuja. Itafanyika jijini Dar es Salaam. Lakini pia watu kutoka makabila mengine watapokelewa kuhudhuria.
Sherehe hii itakuwa endelevu. Itakuwa ikifanyika kila mwaka katika ukumbi au eneo litakalopendekezwa na kamati ya maandalizi.
Lengo la sherehe hii ni kudumisha na kukumbusha mila, desturi na tamaduni za Kabila la Wangoni.
1. WAHUDHURIAJI:
Watu wote wanakaribishwa kuhudhuria siku hiyo kwa sababu itakuwa siku ya kipekee na kuvutia mno.
2.UKUMBI:
UKUMBI UTAKUWA MAKUMBUSHO YA TAIFA AU POPOTE PANAPOFAA KWA HADHI NA MAZINGIRA YAKE.
Ukumbi utakuwa wa nje, uliyozungukwa na nyasi zenye mwonekano wa ubichi.
Rangi nzuri ya kijani iliyoiva na mapambo ya asili ya jamii ya
Wangoni yenye kitambaa cha chuichui na ngozi na magome ya
miti ya migomba nk.
Kutakuwa na vyakula vya asili ya Wangoni; kama vile nyama
choma (zitazochomwa kwenye grill) na ugali wa unga wa ulezi, mtama na mahindi utakaosongwa pembeni.
Pia kutakuwa na kachumbari iliyoandaliwa vizuri na mboga za majani, ikiwemo mboga maarufu ya Wangoni ya majani ya maboga, yaani 'likolo la nanyungu'. Hivi ni vyakula vya asili vya Wangoni.
Kutakuwa na hali ya utulivu na kifahari na wageni
watakaohudhuria wote watakuwa na furaha na mavazi ya asili
ya Wangoni.
Wageni wakiwa wanaongea, watafurahia kusikia muziki (wa back ground) ambao nao ni nyimbo za Kingoni zinazofahamika.
Kutakuwa na wasanii maarufu, Wangoni na wa makabila mengine.
Kutakuwa na vinywaji vya aina nyingi mchanganyiko. Vyenye kilevi,
vinywaji laini, coctail na maji. Pia kutakuwa na pombe za asili; kama vile kangara, mnazi, mtama, kangara n.k.
Kutakuwa na Mgeni Rasmi ambaye uhitaji unataka awe Mngoni au mwakilishi kutoka kwa mgeni rasmi Mngoni endapo atakuwa amepata udhuru wa ghafla.
Wasanii wa nyimbo za jamii ya Wangoni wataimba kwaya na kucheza ngoma mbalimbali za Kingoni zikiwemo Kitoto, Ligwamba, Lizombe, Beta n.k.
MC (Master of Ceremony) atatakiwa kuwa Mngoni au kujua lugha ya Kingoni kama kiasili yeye atakuwa siyo Mngoni. Vizuri awe Mngoni.
MC atawasimulia wageni waalikwa na Mgeni Rasmi Historia ya Kabila la Wangoni.
Waandaaji watatoa Tuzo kwa msanii Mngoni aliyedumisha/anayedumisha mila, desturi na tamaduni za Wangoni kwa zama hizi.
3. KIINGILIO
Kiingilio kinatarajiwa kuwa 50,000 (kwa ngazi ya mwisho) 100,000 (kwa ngazi ya kati) na 150,000 (kwa ngazi ya kwanza). Ngazi zitabadilika ubora kulingana na kiwango cha pesa ya kiingilio. Kila atakayelipia atapewa kadi maalum yenye jina lake kwa ajili ya kukubali ushiriki wake. Maelekezo zaidi yatatolewa siku si nyingi.
4. MAPAMBO
Mapambo siku ya shughuli yatakuwa ya asili ya ngozi ya chui na magome ya miti n.k.
DJ (Disco Joker); Anafaa awe DJ Hemedy Kavu.
MC; anafaa kuwa Mrisho Mpoto na Bambo.
MUZIKI; Tuselebuke (Ninapotaka Mimi ni Hapo tu) na mingine ambayo itaendana na shughuli husika.
6. WANGONI WAMEJAA KWENYE TASNIA YA BURUDANI TANZANIA
Wangoni wako vizuri katika sanaa ya muziki na maigizo. Pia
katika maswala ya elimu na biashara, lakini mwamko wao ni
mdogo. Wangoni walio kwenye sanaa hizi hapa nchini ni;
(i). Lucy Fancis Komba (maigizo).
(ii). Rose Donatus Ndauka (maigizo na muziki).
(iii). Dickson Samson Makwaya (Bambo) (muigizaji/mchekeshaji).
(iv). Lulu Mapunda (Aunt Lulu) (maigizo).
(v). Jacqueline Nachale (Jack Mngoni) (mchekeshaji).
(vi). Joseph Leonard Haule (Professor J) (mwanamuziki).
(vii). Mkono wa Mkonole (muigizaji na mchekeshaji).
(viii). Paul Mbena 'Mr Paul' (mwanamuziki wa R & B).
(ix). Jokate Urban Mwegelo (mwanasiasa/ miss/mwimbaji).
(x). Producer Mr. T
(xi). Producer C9 Kanjenje.
(xii). Mrisho Mpoto 'Mjomba' (mwanamuziki).
(xiii). Walter Chilambo (mwimbaji).
(xiv). Cosmas Thobias Chidumule (mwanamuziki).
(xv). Joseph Osimundi Mbilinyi (Sugu) (mwanamuziki).
(xvi). Angel John Komba (Winter) (mwigizaji).
7. WASANII WANGONI TUNAOENDELEA KUWAENZI AMBAO WALIFARIKI DUNIA
Marehemu Kapteni John Damiani Komba (alikuwa mwimbaji wa kwaya na mbunge).
Marehemu Albert Kenneth Mangweha ( alikuwa mwanamuziki).
Marehemu D. Rob (kutoka Kundi la Kwanza Unit)
Catherine Komba (Bi. Nyakomba alikuwa kwenye maigizo) na Grace Mapunda ( alikuwa mwigizaji).
8. TABIA ZA WANGONI
Wangoni wana tabia ya heshima. Mwanamke au mwanamume
anaposalimia anakaa kabisa chini ndipo atoe salamu (aamkie). Lakini
zamani salamu ilikuwa Mngoni analala kabisa chini ndipo
anasalimia. Yaani anagalagala.
Hata hivyo, ukienda kwenye
sherehe za Wangoni utakuta baadhi yao wanalala kabisa chini
na kugalagala ili kudumisha mila walizoacha mababu zetu.
Tulikuwa tukiona picha mjengeo za aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, marehemu Jenista Mhagama alivyokuwa akigalagala ardhini katika sherehe mbalimbali zilizokuwa zikifanyika jimboni kwake Peramiho.
9. MGENI RASMI (ANAYETARAJIWA)
Makamu wa Rais wa Jamhuri yaMuunganowaTanzania- Emmanuel John Nchimbi.
10. WAGENI WAALIKWA (WANAOTARAJIWA)
1. Chifu wa Wangoni.
2. Jokate Mwegelo.
3. Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Kasim Majaliwa, Mary Majaliwa.
4. Mke wa Rais wa Zanzibar, Mariam Mwinyi.
11. DHAMIRA NA MALENGO YA WAKUNYUMBA'S TRADITION PARTY KUFANYA SHEREHE
Kuendeleza urithi wao ulioachwa na mababu zao. Kujenga na
kudumisha mila na tamaduni zao. Wangoni wamekuwa wakipoteza
uhalisia wao kwa sababu ya kulowea.
Miaka ijayo, wanaweza kukosa asili yao moja kwa moja kutokana na
kujichanganya mapema na tamaduni za makabila mbalimbali. Kwa
mfano miaka ya sasa, kuna Wangoni- Wamatengo. Wangoni -Wanyasa na Wangoni-Wampoto n.k.
Imeandaliwa na: Lucy F. Komba, Mkurugenzi Mtendaji wa MS PRODUCTION
[U+1F4DE][U+FFFD] +45 25548584 [U+1F4E7][U+FFFD]
lucy_komba@yahoo.com.