Wakulima wa Pamba waandamana kupinga bei ya pamba Kahama.

Rasib

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
395
45
Ilikua ni majira ya saa tatu asubuhi wakulima wa kijiji cha Ngaya wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga walipo amuandamana kwa makundu, wazee kwa vijana, wamama kwa wadada kuelekea ofisi za mkuu wa wilaya ya Kahama. Katika maandamano hayo wakulima walikuwa wakilalamikia bei ya pamba iliyopangwa na serikali kwa shilingi 660/= kwa kilo moja wakati mwaka jana ilikua sh1100/= kwa kilo,
wakulima hao walisema wamechoka kuona serikali yao inapowakandamiza kwa kuwapangia bei ambayo haiwezi kukizi haja yao madhalani alisema mzee mmoja "mimi ni mzazi wa watoto 13 na ninategemea Kilimo cha Pamba kusomesha watoto na kuwapatia chakula. Jitihada yao ya kuonana na mkuu wa wilaya ziligonga mwamba baada ya kupigiwa simu bila kupatikana, pia walijaribu kumtafuta mheshimiwa diwani kwa simu baada ya kumkosa ofisini na kuwaambiwa hupo Kahama kwenye kikao..
MY TAKE! Hivi kama mkulima wa chini kabisa anapata manyanyaso ya kulatakiwa kulipwa sh. 660/= kwa kilo ya Pamba hivi nini maana ya KILIMO KWANZA na Je inamsaidiaje huyu mkulima? Kweli serikali yetu ni DHAIFU..
Je? NA CHADEMA WAPO NYUMA YA MAANDAMANO HAYO? Nawasilisha!
Source - Radio Kahama..
 
Back
Top Bottom