Kicheko kwa Wakulima Serikali ikinunua Mahindi kwa bei nzuri

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wakulima wa mahindi mkoani Iringa wameanza kunufaika na bei mpya ya Sh. 950 kwa kilo iliyotolewa na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), baada ya serikali kuweka ruzuku ili kuwapunguzia mzigo wakulima.

Tofauti na miezi mitatu ilivopita kilo moja ilinunuliwa kwa Sh. 650 hali ilivowafanya wakulima kupaza sauti na serikali kuagiza Wakala wa Taifa wa Hifadhi va Chakula (NFRA) na PB kununua mazao hayo ili kuwaepusha wakulima na ulanguzi.

Meneja wa CPB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Dk. Jaspa Samweli alimweleza mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake kuwa ongezeko la wakulima wakubwa na wadogo kuza mahindi kwa sasa ni kubwa zaidi, kwa kuwa limesaidia kuongezeka kwa Ununuzi wa mahindi.

Aidha, alisema vituo vya ununuzi ni Songea mkoani Ruvuma, Mlowo na Tunduma Mkoa wa Songwe pamoja na Iringa Alisema, CPB imeanza kununua mahindi mwezi mmoja uliopita kwenye kituo cha Iringa kwa kilo moja
Sh. 950 wakati Kituo cha Songea ni Sh. 850, Mlowo na Tunduma mkoani Songwe kilo moia ni Sh. 850.

Aidha, alisema hadi sasa zaidi ya tani za mahindi ya wakulima 13.500 zimenunuliwa ikiwa ni kati ya tani 80.000 zinazotaraiiwa kununuliwa kutoka kwa wakulima ndani ya mikoa va Nanda za Juu Kusini.

Dk. Samweli alisema kutokana na ongezeko kubwa la wakulima kukimbilia kuuza mahindi yao CPB
Iringa wamelazimika kuweka utaratibu wa kununua gunia moja hadi tani mbili na wale wakulima wakubwa wa tani saba kuendelea lengo ni kahakikisha makundi vote vanafikiwa.

Alisema kwa wote wanaofika Kuuza mahindi yao kuwa viwango vya ubora. wa mahindi vanayotakiwa kununuliwa hivvo kabla ya ununuzi mahindi vanapimwa maabara na vale valiyokidhi viwango vananunuliwa kisha mkulima anawekewa fedha kwenve akaunti ya benki ndani va siku tatu,
 
Ni jambo jema,

Wakulima wanufaike, Nchi ipate akiba ya CHAKULA Cha kutosha.

WANUNUZI Kutoka nje waje na Dollars ghalani mwa sirikali.

MARUFUKU WANUNUZI kuingia mashambani kimagendo,

Mungu ibariki TANZANIA,

Amen
 
Hiyo bei hawatapata mahindi,ukienda kuuza mahindi NFRA unakatwa gharama kibao sijui uchafuzi,sijui magunia na mambo kibao..ikiwemo kucheleweshewa malipo.wakati huo kuna wafanyabiaashara wananunua 900 kg cash unapima mzigo unaondoka na hela yako
 
Kule Songea Serikali inanunua mahindi Kilo Tsh. 800 mkopo, na mtaani wachuuzi wananunua kwa 700 cash, lakini wakulima wako radhi kuuzia watu wa Mtaani kuliko kupeleka kwenye maghala ya Serikali.

Too much politics!
 
Jichanganye Sasa ukawauzie serikali mahindi uone Cha Moto, Mpaka ulipwe hakuna rangi utaacha kuona
 
Tatizo la kuiuzia serikali,
1. Mzigo unapeleka, hulipwi Apo Apo.
2. Utalipwa jinsi wanavojiskia wao
3. Ili ulipwe haraka, mpk utoe rushwa
3. Hata Ukilipwa bado Kuna makato lukuki
4. Ukiwa mzalendo, utakufa unaidai serikali

Mifano Ni mingi,
- Korosho kule kusini
-Pamba kule mwanza
-Kahawa kule kagera
 
Kule Songea Serikali inanunua mahindi Kilo Tsh. 800 mkopo, na mtaani wachuuzi wananunua kwa 700 cash, lakini wakulima wako radhi kuuzia watu wa Mtaani kuliko kupeleka kwenye maghala ya Serikali.

Too much politics!
Kwa sasa bei za mahindi songea zikoje??
 
Kule Songea Serikali inanunua mahindi Kilo Tsh. 800 mkopo, na mtaani wachuuzi wananunua kwa 700 cash, lakini wakulima wako radhi kuuzia watu wa Mtaani kuliko kupeleka kwenye maghala ya Serikali.

Too much politics!
Mzee upo songea
 
Back
Top Bottom