wilcoxon
JF-Expert Member
- Jun 25, 2017
- 1,222
- 3,176
Hiki ni kichwa cha habari kwenye gazeti la Jamhuri
Kwa habari hii serikali ya awamu hii itakuwa na ufisadi mkubwa kuliko awamu zilizopita maana kila mradi una harufu ya upigaji.
==========
NA MKINGA MKINGA,
DAR ES SALAAM
Tanzania inaelekea kupoteza wastani wa Sh bilioni 90 kutokana na ujanja uliofanywa na wakubwa wachache katika mkataba wa kuchapisha hati za kusafiria za kielektroniki (e-passport), uchunguzi wa JAMHURI umebaini.
Wakati anazindua hati hizo wiki iliyopita, Rais John Magufuli alisema nchi imefanikiwa kuokoa mabilioni ya fedha ambayo yangefunjwa na ‘wajanja’ wachache kupitia mkataba wa awali ambao uchapishaji wa e-passport walitaka uligharimu taifa Sh bilioni 400.
Rais Magufuli amevisifia vyombo nyeti vya dola kuwa vimeweza kushusha gharama za mkataba huo kufikia dola milioni 57. Dola milioni 57 za Marekani ni sawa na Sh bilioni 127.68 kwa bei ya kubadili dola moja Sh 2,240 hadi mwishoni mwa wiki iliyopita.
Kwa mantiki hiyo, kauli ya Rais Magufuli inamaanisha kuwa nchi kwa mkataba huu imeokoa Sh 272.32.
Jinsi wajanja ‘walivyoipiga’ nchi
Uchunguzi wa JAMHURI, umethibitisha pasi na shaka kwamba Serikali ingeweza kuokoa zaidi ya Sh bilioni 90, kama baadhi ya viongozi waandamizi serikalini walioaminiwa na kukabidhiwa dhamana ya kusimamia suala hilo wangeongozwa na uzalendo bila kusahau thamani ya pesa (value for money).
Nyaraka zinaonesha kuwa kampuni ya DeLaRue ya Uingereza ilikuwa ipewe zabuni ya kuchapisha hati za kusafiria za kielektroniki kwa gharama ya dola milioni 16 za Marekani sawa na Sh bilioni 35.84 kwa kipindi cha miaka minane, lakini katika mazingira yasiyoelezeka imeachwa na kuchukuliwa kampuni ya HID Global inayoligharimu taifa dola milioni 57 za Marekani.
Chanzo chenye nafasi ya kipekee ya taarifa nyeti kuhusu mchezo huu, kimeliambia JAMHURI kuwa wakubwa kutoka serikalini waliitembelea kampuni ya DeLaRue, wakachunguza uzoefu wa kampuni hiyo, uhalisia wa gharama, utaalam, weledi na usalama wa teknolojia ya kuzalisha hati hizo na wakakubaliana nayo.
Viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Rais na Uhamiaji, Mei mwaka jana walikwenda nchini Uingereza kuikagua kampuni hiyo. Kati ya viongozi waliokuwa kwenye msafara ni pamoja na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI), Dk. Anna Makakala.
Ziara ya Uingereza ililenga kufanya uchunguzi wa kina (due diligence) kabla ya kutoa zabuni kwa kampuni hiyo.
Chanzo chetu kilichoshiriki ziara hiyo, kimesema viongiozi wote waandamizi waliridhishwa na viwango vya kampuni hiyo. Baada ya kurudi waliiandikia makubaliano ya awali (Memorandum of Understanding) na baadaye mkataba, ambao hata hivyo haukutiwa saini.
Mkataba huo ulikuwa na kipengele cha bei ya mkataba wa kufanya kazi hii kilichosomeka: “Serikali ya Tanzania itatakiwa kulipa kiasi cha Pauni 6, 989,468 [za Uingereza] kwa mwaka wa kwanza. Gharama hizo zikiwa zimejumuisha gharama za mfumo na vifaa vya kiusalama vya uchapaji wa nakala 400,000 kwa ajili ya kutengenezea hati za kusafiria (passport).
“Gharama za kutengeneza kitabu cha pasipoti mtandao (e-passport) pamoja na alama za siri kwa mwaka mmoja ni Pauni 6.26 (Sh 12,770.4) kwa kila kitabu cha pasipoti kilichokamilika. Gharama ya mfumo, leseni na utekelezaji kwa mwaka mmoja ni Pauni milioni 5,” inasomeka sehemu ya nyaraka zilizoonwa na Gazeti la JAMHURI.
Mfumo huu unatajwa na kampuni ya ReLaRue unajuisha, e-passport, e-boarder, e-visa, e-payment na e-immigration. “Hii kimsingi ni software, hivyo yenyewe inafanya kazi ya ku-control system na si vinginevyo. Gharama yake si kubwa kihivyo,” kimesema chanzo chetu.
Kampuni hii iliyoonekana ina sifa zote, baadaye imeachwa hewani bila maelezo ya aina yoyote.
Sifa za kuchapa e-passport
Masharti ya kampuni kupewa zabuni ya kuchapa hati za kusafiria za kielektroniki duniani, ambayo Tanzania imeyachukua yote kama sehemu ya zabuni hii, yanaitaka kampuni kuwa imewahi kufanya kazi hii ya kuchapisha hati za kielektorini kwa mikataba isiyopungua mitano.
Kwa ajili ya usalama, kampuni ya kuchapisha hati za kusafiria za kielektroniki inapaswa kuwa na mitambo yake, majengo yake, teknolojia ya kuchapa hati hizo na kitengo cha usalama bila kuhusisha mtu wa kati (third part).
Kuna vigezo tisa vya kupata zabuni ya aina hii kokote duniani, ambavyo ni:-
Hata hivyo, uchunguzi wa JAMHURI umebaini kuwa kampuni ya HID Global iliyopewa kazi hii haijawahi yenyewe kama kampuni kuchapisha hati hata moja ya kielektroniki peke yake kwani kazi yake ya msingi ni kuuza plastic na polycarbonate cards (vitambulisho na kadi za kufungulia milango).
Kutokana na kampuni hii kutokuwa na ujuzi na vifaa vya kutengeneza hati za kusafiria za kielektroniki, imewahi mara moja kwa ubia na kampuni ya DLRS ya nchini Ireland kutengeneza hati ya kielektroniki ya Ireland na sasa wameshirikiana nayo tena kuomba kutengeneza hati ya Tanzania. Hata kwenye mtandao wao imeutangazia ulimwengu ukweli huu.
JAMHURI limebaini kuwa kuna kampuni tatu kubwa na zenye kuaminika duniani zinazofanya kazi ya kuchapisha hati za kielektroniki ambazo ni DeLaRue ya Uingereza, Muhlbaur ya Ujerumani na Gemalto ya Uholanzi.
Kampuni iliyonyimwa kazi inazofanya
Kampuni ya DeLaRue iliyonyimwa zabuni ya kuchapisha hati za kielektroniki kwa gharama ya dola milioni 16 za Marekani kwa miaka minane, inachapisha hati za kielektroniki.
Kwa Bara la Afrika wanachapisha hati za kusafiria za nchi za Angola (e-passport na mifumo), Ghana, Mali (e-passport na mifumo), Swaziland, Lesotho, Botswana (Vitambulisho vya Taifa), Rwanda (Fedha, e-passport na mifumo, vitambulisho vya taifa na huduma za fedha).
Nchi nyingine ni Somalia (fedha na huduma za fedha), Kenya (fedha, e-passport na huduma za fedha), Sudan (stempu za ushuru), Mauritania (e-passport), Cameroon (vitambulisho vya taifa na vya mpigakura) na Guinea Bissau (passport na fedha).
Mchezo ulivyochezwa
Uchunguzi uliofanyika tangu Mei, mwaka jana, umebaini kwamba gharama halisi za mradi ambao umezinduliwa na Rais Magufuli wiki iliyopita hazikutakiwa kuzidi dola milioni 16 za Marekani, karibu Sh bilioni 35.84. Bei ya soko ya kubadili pesa Jumamosi iliyopita ilikuwa Sh 2,240 kwa dola moja ya Marekani.
JAMHURI, limebaini kuwa mchakato wa kumpata mzabuni wa kufanya mradi huo wa Uhamiaji Mtandao, ambao baadaye ungeelekea kwenye kutoa hati ya kusafiria ya kielektroniki (e-passport) ulianza kugubikwa na ‘ushawishi’ wenye harufu ya rushwa ukiwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, na ndipo mabosi wa wizara hiyo walimwomba Rais Magufuli kuingilia kati.
Vyanzo vyetu vimesema miongoni mwa mambo yaliyochangia kuhamishwa kwa zabuni ya kuchapa e-passport kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ni pamoja na Rais Magufuli, kutoridhishwa na mchakato wa zabuni pale wizarani. Sababu nyingine ilikuwa ni kutotaka kufanya zabuni ya wazi maana jambo lenyewe limebeba maslahi mapana ya taifa.
Chanzo chetu cha habari kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kimeliambia JAMHURI kwamba kumekuwepo usiri mkubwa katika mchakato wa kupatikana mzabuni wa kufanya kazi hiyo.
Uchunguzi unaonyesha kuwa kampuni iliyopewa kazi ya kuchapa e-passport haikuwa miongoni mwa kampuni zilizoomba kazi hiyo awali kupitia wizarani hapo, kabla ya kazi hii kuhamishwa Ofisi ya Rais ilikoaminika kuwa wakubwa wataisimamia kwa uadilifu wa hali ya juu.
“Kiutaratibu hapa tulikuwa tumeshafanya [kazi] mpaka kwenye ‘pre-qualification’ lakini utashangaa kwamba makampuni yote ‘reputable’ yameachwa na wamekwenda kumchukua ‘component supplier’. Kuna baadhi ya masharti tuliyaweka kwa wazabuni, lakini nadhani yamekiukwa ama yalikuwa ya hovyo ndiyo maana hayakuzingatiwa kabisa katika kumpata mzabuni.
“Nadhani ni suala la muda tu, kila kitu kitakuwa wazi na wananchi watafahamu namna kodi zao zinavyochezewa… mpaka napata hisia kwamba labda lingeshughulikiwa hapa wizarani kwetu labda mambo yangekuwa tofauti sana,” kimesema chanzo chetu.
Nyendo zinazotiliwa shaka
Uchunguzi wa Gazeti la JAMHURI umebaini kwamba kumekuwepo na nyendo zinazotiliwa shaka, ambazo zimekuwa zikiwahusisha baadhi ya viongozi waandamizi wa Serikali kutoka ndani ya Idara ya Uhamiaji na Ofisi ya Rais.
JAMHURI limebaini kuwa Novemba 27, mwaka jana viongozi watano kutoka Uhamiaji, walifanya mkutano wa siri katika chumba binafsi Na. 303 cha Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kati ya saa 08:30 alasiri hadi 11:00 jioni, wakiwa na mmoja wa mawakala wa kampuni ya HID Global iliyoshinda zabuni na kupewa kazi ya kuchapisha e-passport kwa kasi ya kutisha.
Kitendo hicho cha kujifungia chumbani watu zaidi ya watano, kinaleta maswali mengi, pengine hata kuikumbusha nchi machungu ya mmoja wa waliowahi kuwa mawaziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi kwenda kusaini mkataba wa kuchimba dhahabu ya Buzwagi katika chumba cha Hotel ya Churchill nchini Uingereza mwaka 2007.
Desturi za taifa zinaliona jambo hilo lina ukakasi, hasa ikizingatiwa kwamba kama ni mkutano halali usiokuwa na hila wala mawaa ndani yake, kwanini ukafanyike chumbani wakati kumbi za mikutano kwenye hoteli na ofisi za Serikali zipo.
Taarifa zinaonesha chumba hicho kilikuwa kimekodiwa na raia wa Kenya, Henry Mkuzi, ambaye naye alishiriki kikao hicho kwa muda wa saa tatu.
“Ndugu mwandishi nadhani hapo hata kama ni mtoto mdogo mwenye ufahamu mdogo anaweza kunusa harufu isiyopendeza,” kimesema chanzo chetu.
JAMHURI limezungumza na Mkuzi akiwa nchini Kenya, ambaye ameng’aka kwa nini aulizwe swali hilo, akihoji kuna kosa gani yeye kufanya mkutano na watu alioingia nao mkataba, na akataka asipigiwe simu tena.
“Kwani kuna shida gani mimi kukutana na watu ambao tuna mkataba nao hotelini? Mimi sitakiwi kuzungumza na wewe hilo, tafadhali fuata utaratibu sahihi wa kuzungumza na HID,” amesema na ameongeza kuwa JAMHURI likipenda likawaulize watu wa Uhamiaji juu ya suala hili.
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (CHADEMA), wiki iliyopita alimtaja aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dk. Modestus Kipilimba kuwa alisaini mkataba wa hovyo ulioongeza gharama ya kupata hati za kielektroniki.
Amesema Mkurugenzi huyo amekiuka maelekezo ya Rais Magufuli ya kupata mzabuni mwenye bei nafuu na hivyo amelitia taifa hasara ya mabilioni ya fedha.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, amejibu hoja hiyo bungeni kwa kusema: “Naomba niwaambie kwamba mwanzoni upembuzi uliokuwa unafanyika kabla Serikali haijaingia kati, ukubwa wa mradi ni uleule na fedha zilizotakiwa kutumika ni takribani dola za Marekani milioni 192.
“Kwa maana hiyo kama ambavyo nimesema tangu mwanzo, na ninamjua babu yangu [mtani wake] Mheshimiwa Heche, tangu akiwa kule Bavicha [Baraza la Vijana Chadema] haka ka wimbo ka ufisadi kalikuwa kananoga sana. Kama kuna mtu anadhani nasema uongo atasubiri sana,” amesema Dk. Nchemba.
Jitihada za kumpata Dk. Kipilimba, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa, hazikuzaa matunda, ila Gazeti la Tanzania Daima Toleo Na. 4718 la Februari 3, 2018, Jumamosi, limemkariri akisema:
“Nilipelekwa NIDA Februari 25, nikaondoka pale Agosti 24. Kwa miezi sita niliyokuwa pale kwanza ofisi haikuwa na fedha. Sikuwahi kununua wala kuagiza chochote…sijasaini mkataba wowote ndani ya NIDA. Lakini nimenyamaza. Nimeshangaa sana, vitu vingi wamepindua.
“I said nothing (sikusema chochote), wakati mwingine nilikuwa natoa hela yangu mfukoni kununua stationeries. Siku niliyoondoka mimi, kesho yake hela zikaingia kutoka kwa donors [wafadhili] na Serikali Kuu.
“Mimi nimerekebisha tu, hasa tatizo la ikama. Kama mtakumbuka kulikuwa na mashine 150 lakini watu wa kufanya kazi walikuwa 840. Nikaona hata tukifanya shift tatu wanaohitajika ni watu 450 tu, nikapunguza.
“Kingine nilichofanya ni ku-introduce [kuanzisha], kitambulisho chenye signature (saini). To be honest (kuwa mkweli) ofisi haikuwa na fedha. Sikununua chochote, maana sikuwa na hela,” amesisitiza Dk. Kipilimba.
Kuhusu e-passport, Dk. Kipilimba amesema madai ya mbunge Heche yamelenga eneo moja, hakubainisha kwamba kilichozinduliwa ni e-immigration.
“Eti kile kitabu peke yake ndiyo ameona azungumzie. Kuna e-boarder, e permit, e-passport, e-visa, yaani ndugu zangu hao bwana, nyie ndio mnaojuana nao vizuri,” amesema.
Rais Magufuli anena
Wiki iliyopita, Rais Magufuli alizindua mfumo wa Uhamiaji Mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali.
Uzinduzi wa mfumo huo ulifanyika katika Ofisi Kuu ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Seif Ali Iddi, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa.
Wengine ni Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Zubeir Ali Maulid; Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson; Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Dk. Ali Hassan Mwinyi na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
Kabla ya kuzindua mfumo wa Uhamiaji Mtandao, Rais Magufuli alikagua teknolojia iliyotumika katika mfumo huo ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa alama za vidole na baadaye kupatiwa pasipoti mpya ya kielektronikia (e-Passport) ambayo pia ilianza kutolewa siku hiyo hiyo.
Pasipoti mpya za kielektroniki pia zimetolewa kwa viongozi wengine wakuu wa Serikali, Bunge na Mahakama waliohudhuria uzinduzi huo.
Rais Magufuli akampongeza Dk. Nchemba na Idara ya Uhamiaji kwa kufanikisha mradi wa kuweka mfumo wa Uhamiaji Mtandao na kuanza kutoa hati mpya ya kielektroniki kwa gharama nafuu ya ya dola milioni 57 (Sh bilioni 127.2) ikilinganishwa na makadirio yaliyowekwa awali ya Sh bilioni 400.
“Hapa tumeokoa fedha nyingi za Watanzania, kuna watu walikuwa wamejiandaa kutupiga na kuchukua hizo Sh bilioni 400, lakini tukatumia vyombo vyetu mbalimbali, tukafanya uchunguzi na tumefanikiwa kutekeleza mradi huu kwa gharama nafuu,” alisema Rais Magufuli.
Rais Magufuli akaahidi kutoa Sh bilioni 10 kwa ajili ya kujenga ofisi ya makao makuu ya Idara ya Uhamiaji mjini Dodoma.
“Kamishna Jenerali Dk. Anna Makakala na timu yako mnafanya kazi nzuri, ndio maana nimewanunulia nyumba 103 kwa ajili ya wafanyakazi kule Dodoma na leo nitawapa fedha nyingine Sh bilioni 10 mkajenge ofisi nzuri ya makao makuu. Nyinyi endeleeni kuchapa kazi, endeleeni kukamata wahamiaji haramu na endeleeni kukusanya mapato vizuri,” alisema Rais Magufuli.
Mapema, akitoa taarifa ya mfumo wa Uhamiaji Mtandao, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Makakala alisema mfumo huo ni muunganiko wa mifumo mbalimbali ambayo imesanifiwa kufanya kazi kwa pamoja, kutoa taarifa kwa watumiaji na wadau wa huduma za kiuhamiaji.
Alisema kupitia mfumo huo Idara ya Uhamiaji inatarajia kutoa pasipoti za kielektroniki (e-Passport), viza za kielektroniki (e-Visa), vibali vya ukaazi vya kielektroniki (e-Permit) na udhibiti wa mipaka wa kielektroniki (e-Border Management) kwa awamu nne hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu; pamoja na kutoa pasipoti ya kielektroniki ya Afrika Mashariki – ya Tanzania.
Chanzo: Jamhuri

- Mshindi wa zabuni anapaswa kuwa amewahi kuchapisha au yuko katika mchakato wa kuchapisha kama mkandarasi mkuu katika miradi mitano ya hati za kielektroniki. Katika miradi hiyo, anapaswa kuwa aliwahi kuchapisha hati za kusafiria milioni 1 au zaidi kwa kila mkataba kwa mwaka, ambayo mzabuni amekuwa mkandarasi mkuu.
- Kipaumbele kinatolewa kwa mkandarasi anayeonyesha katika zabuni yake kuwa ataweka masuala mengi ya kiusalama katika hati ya kusafiria husika kuliko makandarasi wenzake.
- Mkandarasi anapaswa kuthibitisha kwa kutoa rejea angalau 10 za kazi za hati za kusafiria alizowahi kuzifanya, zikiwa na mfumo wa taarifa za siri katika ukurasa wa taarifa. Kati ya hati hizo 10, tano ya hati hizo [za nchi mbalimbali] zinapaswa kuwa za kielektroniki.
- Mkandarasi anapaswa kuthibitisha kwa kutoa rejea inayoonyesha uwezo wake kuwa alipata kuyatengenezea mataifa yapatayo matano hati za kieleketroniki na kuyahamisha kutoka mfumo wa hati tulionao sasa.
- Mkandarasi anapaswa kuonyesha uzoefu wa kurithi mkataba wa kuchapisha hati za kielektroniki katikati ya mradi unaoendelea na akaumalizia kwa ufanisi mkubwa.
- Mkandarasi anapaswa kuthibitisha kuwa amewahi kutoa suluhisho la hati za kielektroniki zinazojumuisha kutia saini ya kieleketroniki.
- Mkandarasi anapaswa kuwa na rejea tatu za nchi alikochapisha hati za kielektroniki zenye viwango na ubora wa kimataifa.
- Mkandarasi anapaswa kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa za miaka mitano zenye kuonyesha kuwa mzunguko wa biashara yake unafikia dola milioni 100 za Marekani kwa mwaka, na;.
- Mkandarasi anapaswa kuonyesha ufahamu juu ya mfumo wa hati za kusafiria za kielektroniki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.