Wakubwa Kulishana Sumu

Kilasara

JF-Expert Member
Dec 21, 2008
577
116
Kumeibuka mjadala mkali kuhusu sumu aliotiliwa Mhe. Harrison Mwakyembe; na inaonekana Polisi wetu hawana uwezo wa kukumbuka au kwa maksudi, wanapuuza matukio ya wakubwa kutiliana sumu. Hii ni balaa kwa taifa.

Nakumbuka Waheshimiwa Wabunge wakitimka ukumbini, sio siku nyingi zilizopita, kutokana na sumu iliyomwagiwa katika viti fulani katika Bunge. Sasa inaonekana wakubwa hawaamiani tena. Hivi mtindo huu unatokana na uroho wa madaraka au ni chuki baina ya viongozi?

Kwa nini Polisi wetu hakuchunguza tukio lile lililosababisha Wabunge kutimka toka ukumbini? Na kwanini Manumba, Mkuu wa Upelelezi wa Jinai anataka kufukia fukia uwezekano wa Mwakyembe kutiliwa au kulishwa sumu? Sisi wananchi tunakumbuka Mwakyembe ndiye aliyeongoza KAMATI ya Bunge kuchunguza ufisadi wa Richmond na Dowans; na mtu mwenye akili kidogo tu anaweza kudhani kuna sababu tosha ya mafisadi kumwekea sumu.

Ugua pole Mpendwa Harrison! Mungu akuongoze na kukusaidia katika juhudi zako za kutafuta tiba.
 
Kwenye madaraka huko kuna ulaji wa KUTOSHA sasa wakiona mtu anataka kunyang'anya ulaji wanajitahidi kumnyang'anya yeye roho yake.
 
Back
Top Bottom