Wako wapi wanunuzi wa madini?

Wako wapi wanunuzi wa madini?

Mkuu GAZETI,

Naomba tuwasiliane na ingawa kwa sasa sina mtu anayetaka kununua. Tatizo kubwa kwa Tanzania ni kuwa watu wanataka uwalipe hela wakati mzigo hujauona. Kama utakuwa na mzigo mkubwa na upo tayari kuupeleka Dubai au Switzland ambako wanapima (kwa Almasi) au kuisafisha dhahabu na hapo mnauziana kwa bei ya Pure Gold basi wewe tuwasiliane na ntajaribu kukuulizia wanunuzi.

Kuna jamaa wengi wametapeliwa pesa zao na jamaa mmoja kutoka hapa Poland aliibiwa hela zake Bongo na aliporudi akapata ugonjwa wa moyo na alishajifia siku nyingi. Hivyo uaminifu ndiyo huwa tatizo kubwa hasa kwa wale wanaotaka kuuza madini nje ya nchi. Ila kama una COPPER yaani Shaba basi tuwasiliane kwani hiyo inahitajika sana kwa sasa.

Kama kuna mtu ana Aluminium hasa wale walioko Mzumbiji basi tuwasiliane haraka sana.

Angalizo tu kidogo: Hakuna malipo yoyote yatatolewa hadi mnunuzi awe na uhakika wa mzigo na mzigo akabidhiwe Agent wa kuusafirisha. Inashangaza mtu anauza tani 1,000 ya Copper ila hana fedha za kuuchukua mzigo kutoka hapo kwake na kuupeleka Bandarini na anatataka malipo kidogo ya kuanzia kazi. Mtu kama huyu huwa hata sina hamu ya kuendelea kuwasiliana naye. Mzigo ukishahakikishwa ni wa uhakika, katika Neutral point au kampuni yenye kupima na kuchukua mzigo, basi malipo yatafanyika hapo hapo na si kabla.

Mkuu, kuhusu Copper mi nafahamu mashamba makubwa mno ya copper, tatizo ni mtaji wa kufanya uchimbaji! hakuna makampuni huko ambao wangependa kuwekeza kwa ubia, kama mtu ana vitalu vyake na anataka mwekezaji afanye naye ubia.
 
Mimi niliyapata Msumbiji, tena ni hukuhuku mpakani na TZ si mbali sana
kutoka Mweda hadi huko tena huko sikwenda kwa lengo la madini nilipeleka
Laptop.

Hongera Mkuu, Msumbiji kuna Gemstone nyingi sana we ulipata Dhahabu na Almasi?, ulienda maeneo gani Mkuu, Mtepweshi? btw, vipi biashara ya laptops bado unapeleka?..biashara ya laptops na compters kwa ujumla imekaaje huko?
 
Sawa Mkuu,

Ntaulizia ingawa kwa Tanzania kuna shida kidogo kuwa Wingi wa Copper katika mawe upo chini kidogo kulinganisha na Wacongo au Zambia na hivyo wawekezaji wanaona heri waende Congo na hasa Lubumbashi. Hivyo ninavyoandika, jamaa wanashughulikia safari ya kwenda Lubumbashi kuonana na Gavana wa Mji huo Mama Maria.

Anyway, kama ntapata jamaa walio tayari basi ntakujulisha. Ila wengi ni wafanya biashara ambao hawataki kuwekeza kwenye migodi na kuwapata hao ni ngumu sana kwa sababu wanakuwa ni watu wenye viwanda na matajiri wa kutisha ambao wao wanaongea na Nchi na siyo mtu binafsi. Hapa nikiwa na maana ni Rais wa nchi anakuja kuwaona wakawekeze sehemu au Waziri na si mtu binafsi.
Mkuu, kuhusu Copper mi nafahamu mashamba makubwa mno ya copper, tatizo ni mtaji wa kufanya uchimbaji! hakuna makampuni huko ambao wangependa kuwekeza kwa ubia, kama mtu ana vitalu vyake na anataka mwekezaji afanye naye ubia.
 
Sawa Mkuu,

Ntaulizia ingawa kwa Tanzania kuna shida kidogo kuwa Wingi wa Copper katika mawe upo chini kidogo kulinganisha na Wacongo au Zambia na hivyo wawekezaji wanaona heri waende Congo na hasa Lubumbashi. Hivyo ninavyoandika, jamaa wanashughulikia safari ya kwenda Lubumbashi kuonana na Gavana wa Mji huo Mama Maria.

Anyway, kama ntapata jamaa walio tayari basi ntakujulisha. Ila wengi ni wafanya biashara ambao hawataki kuwekeza kwenye migodi na kuwapata hao ni ngumu sana kwa sababu wanakuwa ni watu wenye viwanda na matajiri wa kutisha ambao wao wanaongea na Nchi na siyo mtu binafsi. Hapa nikiwa na maana ni Rais wa nchi anakuja kuwaona wakawekeze sehemu au Waziri na si mtu binafsi.

Heshima kwako Mkuu!
 
Mkuu, kuhusu Copper mi nafahamu mashamba makubwa mno ya copper, tatizo ni mtaji wa kufanya uchimbaji! hakuna makampuni huko ambao wangependa kuwekeza kwa ubia, kama mtu ana vitalu vyake na anataka mwekezaji afanye naye ubia.
Mkuu
Hayo mashamba makubwa ya copper yako wapi kwa hapa Tanzania?
 
uzi ni wakitambo kidogo ila nlitaka kufahamu kitu jamani..nna vpande vya ruby na red garnet ukubwa kama punje za mtama au mchele ..naweza uza wapi??
 
Wadau nahitaji kujua Mercury in rangi gani hasa maana najua kwa kusoma kwa makaratasi na story ,kuna ya kiwandani na jiwe sasa je yakiwandani ikoje na soko lake likoje kwa gram
 
Wadau nahitaji kufahamu mercury ya kiwandani ikoje na ya kwenye mwamba ikoje
 
Back
Top Bottom