Wako wapi Mashujaa wa Uhuru wa Tanganyika?

Wako wapi Mashujaa wa Uhuru wa Tanganyika?

Nawasikitikia sana vijana wanaoendelea kudanganywa na huyu kiumbe aitwae Mohamed Said,

Kwawale wasiojua historia nawaomba msiwe wavivu na kuishia kuzisoma hizi ngano tu,

Tumieni mda wenu vizuri kusaka maandishi mengine ya kujenga uelewa wenu katika historia ya nchini yetu,

Ni ajabu uongo uleule kuendelezwa kwa mlango wa nyuma huku vijana wakiendelea kushangilia bila kujua madhara yake,

Yericko,
Huenda ukapata shida sana katika haya lakini kila nilipokuwa naandika
ikawa nakuja na mambo mapya ambayo hayakuwa hadhir kabla.

Baada ya muda historia hii niliyoandika na ''paper'' nilizowasilisha ndani
na nje ya nchi zimekuwa mashuhuri na kila fursa inapotokea basi hupewa
mwaliko wa kwenda kuzungumza.

Takriban kila mwaka napata mwaliko wa kuzungumza historia hii katika vyuo
mbalimbali.

Kama nilivyokushauri wewe na jamaa zako kuwa njia nzuri ya kupambana na
kitabu changu ni kwa nyie kuandika hiyo historia yenu ya ''kweli'' lakini mkibaki
hapa JF mtaishia humu JF.
 
Au nani leo anamjua Mzee Yusuf Olotu maarufu Yusuf Ngozi wa Moshi na jitihada zake za kuipa TANU ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Kura Tatu mjini Moshi. Au mchango wa Sheikh Yusuf Badi wa Lindi au mchango wa Dk Michael Lugazia, Dk Luciano Tsere, Dk Joseph Mutahangarwa, Dk Vedasto Kyaruzi, Dk Wilbard Mwanjisi na wengineo?

Kumbe haya mambo ya "Mzee" fulani vs "Dk" fulani yalianza kabla hata Mwalimu hajatawala. Lakini bado kuna watu wanalalamika kuwa Nyerere ndiye aliyebeba dini fulani...
 
Yericko,
Huenda ukapata shida sana katika haya lakini kila nilipokuwa naandika
ikawa nakuja na mambo mapya ambayo hayakuwa hadhir kabla.

Baada ya muda historia hii niliyoandika na ''paper'' nilizowasilisha ndani
na nje ya nchi zimekuwa mashuhuri na kila fursa inapotokea basi hupewa
mwaliko wa kwenda kuzungumza.

Takriban kila mwaka napata mwaliko wa kuzungumza historia hii katika vyuo
mbalimbali.

Kama nilivyokushauri wewe na jamaa zako kuwa njia nzuri ya kupambana na
kitabu changu ni kwa nyie kuandika hiyo historia yenu ya ''kweli'' lakini mkibaki
hapa JF mtaishia humu JF.

Wakristo na Waislamu wakichukiana, wakauana, wakatengana, nk kwa sababu ya chuki unazozieneza ndani na nje ya nchi wewe utafaidika nini hasa?
 
Bulesi,
Nakuwekea hapa habari za Edward Mwangosi na Job Lusinde
kama nilivyoandika katika kitabu changu :

The Founding of TANU in Central Province 1955:
[TABLE="width: 660"]
[TR]
[TD]''...Tabora began to participate in active politics in 1945 when the African Association was introduced to the township from Dodoma through the efforts of Edward Mwangosi.

***

Mwangosi's stand was that Makererians were very important to the party as they would provide the required leadership.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]A total of about forty people attended the meeting including the Makererians, among them Job Lusinde, later to become minister, and Amon Nsekela, later to hold important posts in the government including Tanzania’s High Commission to Britain.

Hassan Suleiman and Ali Ponda did not turn up for the meeting.

While they were assembling for the meeting, the officer-in-charge of the Community Center told them that he had received orders from the District Commissioner that the meeting should be cancelled and people dispersed immediately.

Alexander Kanyamara who was a wealthy African in Dodoma and a personal friend of John Rupia, now TANU Vice-President, called for the postponement of the meeting because of the absence of Hassan Suleiman and Ali Ponda-the TAA top leadership in Dodoma.

Due to this reason and the intimidating order from the DC, the meeting was cancelled without fixing a date for another meeting.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]The following morning Taratibu was arrested by the police and taken to the DC’s office, the present Prime Minister’s office.

Hassan Suleiman was there amicably chatting with the DC, Mr. Smith.

The DC started to interrogate Taratibu by asking him if he spoke English.

Taratibu replied that in the negative.

Speaking in English, Hassan Suleiman told the DC that he was the TANU secretary in Dodoma.

The DC Mr Smith accused Taratibu of forming an illegal organisation and for calling an unauthorized meeting at the Community Center the previous day which was likely to disrupt peace.

Without fear Taratibu replied that he had the mandate to call for a meeting because he was a member of a legally registered political party.

Taratibu fished out his black and green TANU card from his pocket and showed it to the DC. Mr. Smith asked Hassan Suleiman whether he too possessed a TANU card.

Hassan Suleiman had none.

Hassan Suleiman and the DC conversed in English for some time after which he asked both of them to write statements.

After writing his statement Taratibu was allowed to go home.

It is believed that at that time the only TANU members in Dodoma was Taratibu and Alexander Kanyamara who had bought his card in Dar es Salaam.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]When the Makerere graduates, who Mwangosi had put much faith in organizing the party, learned about Taratibu’s ordeal with the DC Mr Smith, they were scared.

They decided to lie low and continue with their academic pursuits at the Kikuyu Secondary School.

Haruna Taratibu and Omari Suleiman now decided to change tactics; they called for a secret meeting at night in the house of Swedi bin Athman.[1]

The meeting decided that Taratibu should go to TANU headquarters in Dar es Salaam and talk to Julius Nyerere himself on the problems facing TANU in Dodoma.

Mahdi Mwinchumu who was TANU member in Dar es Salaam volunteered to accompany Taratibu to the party headquarters since he was known by the leadership there.

Said Musa, another member of the secret committee, also volunteered to accompany Taratibu and Mwinchumu to Dar es Salaam.

On departure day, Job Lusinde went to see the secret delegation off at the railway station.

Lusinde told the delegation that Makererians were in support of all the decisions taken by the secret committee.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Bwana Bulesi,
Ikiwa hujatosheka na habari hizi nifahamishe.

[1] Another version of the founding of TANU in Dodoma is that a meetimg of other patriots was called
in which Seif Waziri Kasembo attended in the house of Salim Omari, who was also present, together
with Fulka Mwinchumu Kinyozi, Swedi Athmani Kagulu, Bakari Omari, Fundi Issa, Mzee Magwila, Manywele
Bushiri, Mzee Ibrahim Sururu Mahusi Selemani, Omari Selemani, Nassoro Mussa, Athmani Nyange and others.
It seems there was rivalry between the two groups because in a paper made available to the author by Seif
Waziri Kasembo it is stated that Haruna Taratibu assumed leadership in Party affairs without the consent of
other patriots. Interesting is the fact that some of the names mentioned by Kasembo appear in both Taratibu
and Suleiman's narration. But the two groups, that of Taratibu and that of Kasembo, came to accommodate
each other because eventually, after office bearers had been elected, Kasembo provided his house as the first
TANU office in Dodoma. Kasembo's father, Waziri Kasembo, was once president of the African Association in
Dodoma.

Tatizo langu na wewe Mohamed ni kwamba you are biased against wakisto na ndio maana hata kwenye hiyo historia ya TANU Dodoma wengi unaowataja na kuhusika na hicho chama ni waislam!! Sasa nikuulize,je huyo Edward Mwangosi alikuwa hana wenzie ambao alishirikiana nao ambao hawakuwa Makerererian au waislam? Katika utafiti wako huko Dododma hukuwahi kusikia majina ya wazee marehemu Mwakasepe, Mwakalinga na Mbowe? Hawa walifanya kazi karibu sana na marehemu Edward Mwangosi lakini nadhani it was not in your scheme of things kuwataja!!
 
mkimaliza haya ya Waislamu vs Wakristu anzeni kabisa na michango ya kikabila katika kupigania Uhuru wa Tanganyika. Sijui kama Tanganyika itaendelea kuwepo,taratibu tumeanza juu kushuka chini!!!
 
Bulesi,
Unajitisha pasi na sababu.

Watu hawauani kwa kumbukumbu za historia.

Watu huasimiana kwa kudhulumiana.
 
Bulesi
Unajitisha pasi na sababu.

Watu hawauani kwa kumbukumbu za historia.

Watu huasimiana kwa kudhulumiana.

Hizo "kumbukumbu za historia" zenye makengeza (ie kuwatukuza Waislamu tuuuu na kuwaona wengine sio kitu) ni justification ya kufanya fujo, kama Uislamu ulivyo! Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya tu! Hata babu yenu Muhammad ambaye umerithi jina lake alifanya hivyo hivyo akawaua Wayahudi wa Khaybar bila sababu yoyote!
 
Hizo "kumbukumbu za historia" zenye makengeza (ie kuwatukuza Waislamu tuuuu na kuwaona wengine sio kitu) ni justification ya kufanya fujo, kama Uislamu ulivyo! Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya tu! Hata babu yenu Muhammad ambaye umerithi jina lake alifanya hivyo hivyo akawaua Wayahudi wa Khaybar bila sababu yoyote!

hata unachokifanya wewe ni kupandikiza chuki kwa waislam dhidi ya wakristo, muhamad ni mtume wetu sasa unapomfanyia dhihaka tukueleweje?
 
Tatizo langu na wewe Mohamed ni kwamba you are biased against wakisto na ndio maana hata kwenye hiyo historia ya TANU Dodoma wengi unaowataja na kuhusika na hicho chama ni waislam!! Sasa nikuulize,je huyo Edward Mwangosi alikuwa hana wenzie ambao alishirikiana nao ambao hawakuwa Makerererian au waislam? Katika utafiti wako huko Dododma hukuwahi kusikia majina ya wazee marehemu Mwakasepe, Mwakalinga na Mbowe? Hawa walifanya kazi karibu sana na marehemu Edward Mwangosi lakini nadhani it was not in your scheme of things kuwataja!!

Bulesi,
Kwanza ulisema sijamtaja Edward Mwangosi sasa unaniletea majina mengine.
Mwangosi nimekuwekea taarifa zake pamoja na habari za Alexander Kanyamala.

Job Lusinde pia nimekuwekea taarifa zake pamoja na Makererians wengine
ambao baada ya kuona Haruna Taratibu kakamatwa na Waingereza kwa ajili
ya TANU wao kama wasemavyo watoto wa mjini ''wakaingia mitini.''

Hapana neno ikiwa wewe una taarifa za hawa wazalendo akina Mwakasepe,
Mwakalinga
na Mbowe ni vyema ukazileta hapa barzani ili sote tufaidike.

Kwa kweli huwezi kuaandika kiiiila kitu wako wengine utawaacha.

Mimi nilikuwa naandika historia ya TANU na wapashaji wangu habari walikuwa
Mzee Hassan Taufik Suleiman, Haruna Taratibu na Mzee Omar Suleiman.

Na hawa ndiyo walikuwa waasisi wa TANU Central Province.
Ndugu yangu ondoa woga hii ni historia na haya mambo yalitokea kama nilivyoandika.

Hakuna mtu anaechimbwa hapa.
Hiki kitabu sasa kipo mitaani takriban miaka 15 na tunakwenda toleo la tatu In Sha Allah.
 
Sijawahi kuona point za huyu mzee! Kati yake na mimi mmoja ni magumashi
 
Tatizo la mabandiko yako mzee Muddy yanafanana kila siku, hakuna jipya zaidi ya cheap politics
Hata wewe pia umekosea kwenye andiko lako kwani ilitakiwa iwe hivi;
Tatizo la mabandiko yako mzee Muddy yanafanana kila siku, hakuna jipya zaidi ya cheap poliDinis.
Jamaa hawezi kuleta andiko lolote ambalo hawezi kuliunganisha na dini yake..huyu mwanaUamsho matatizo kweli.Mi nasubiri afe ili jina lake nalo liwekwe kwenye hiyo listi anayoililia kila siku..adi tunaanza kuona kinyaa ch UDINI wake ptuu!
 
KWA TAARIFA YAKO tANZANIA HAINA SHUJAA WA UHURU. shujaa wa uhuru anapatikana katika vita vya uhuru na sio wapiga domo kama hao wooote anao wataja askofu Mohamedi saidi. Askofu Mohamedi saidi yeye anataka kuionesha kuwa wasiolamu ndio walioikomboa Tanganyika na sio wakristo.

Kwa kufanya hivyo Askofu Mohamedi saidi aangalie sana kuwa anpotosha umma na kuigawa nchi katika misingi ya kidini. Mashujaa wa uhuru wapo Israel tuu na hakuna kwingine.
 
KWA TAARIFA YAKO tANZANIA HAINA SHUJAA WA UHURU. shujaa wa uhuru anapatikana katika vita vya uhuru na sio wapiga domo kama hao wooote anao wataja askofu Mohamedi saidi. Askofu Mohamedi saidi yeye anataka kuionesha kuwa wasiolamu ndio walioikomboa Tanganyika na sio wakristo.

Kwa kufanya hivyo Askofu Mohamedi saidi aangalie sana kuwa anpotosha umma na kuigawa nchi katika misingi ya kidini. Mashujaa wa uhuru wapo Israel tuu na hakuna kwingine.

Hapo kwenye BOLD unamkusudia Mtume Paulo sio tehe tehe tehe!

Nyie wachungwaji mna khasara kubwa!

Au ni ile picha ya yule mzungu ulonunua pale stationary na kuiweka nyumbani kwako ndio inakutia uchizi?! tehe tehe tehe!
 
Hizo "kumbukumbu za historia" zenye makengeza (ie kuwatukuza Waislamu tuuuu na kuwaona wengine sio kitu) ni justification ya kufanya fujo, kama Uislamu ulivyo! Ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya tu! Hata babu yenu Muhammad ambaye umerithi jina lake alifanya hivyo hivyo akawaua Wayahudi wa Khaybar bila sababu yoyote!
Wakati Mtume salalahu alayhi wasallam anahamia Madinah kulikuwa hakuna Mayahudi Khybar (Khobar) !ila kulikuwa na makabila matatu ya Kiyahudi Madina kabla hata ya kuja Mtume.

Mayahudi walihamia Madina baada ya kusoma katika vitabu vyao kuwa kutatokea Mtume wa mwisho na ataishi Madina.

Walipofika Madina walikuta Waarabu kuwa ni Mapagani (ila wachache sana) wasiojua chochote kuhusu Mwenyezi Mungu hivyo walikuwa wakiwatambia na kuwaambia kuwa subirini Mtume wa mwisho aje, nyote mtatufuata.

Alipokuja Mtume walimuona na ishara zote zilizoandikwa katika vitabu vyao ila tatizo kwao ni kuwa Mtume alikuwa ni Mwarabu na si kutoka katika kizazi cha Wana wa Israel kama walivyokuwa wakitaka hivyo wakakataa kumfuata Mtume kwa sababu ya Uarabu wake.

Ikumbukwe kuwa makabila ya Kiyahudi yaliyoluwepo Madinah ni Banu Nadir, Banu Quraydhah na Banu Qaynuqah, wengine walikuwa wakikubali kuwa kweli Mtume ni wa haki na ametoka kwa Mwenyezi Mungu ila ni kwa Waarabu tu na si kwa Mayahudi na ulimwengu mzima (mpaka leo hii bado kuna sect ya Kiyahudi inabeba itikadi hii).

Wakati Mtume SAW anaanzisha nchi ya kwanza ya Kiislamu Madinah hakumfukuza yoyote yule ambaye hakuwa Muislamu! wote waliokuwepo Madinah wakati wa kuanzishwa taifa la Kiislamu walifanywa kuwa ni raia wa nchi wakiwemo Mayahudi.

Ni pale Mayahudi walipokuja kuisaliti nchi yao wenyewe Madinah (hebu isaliti nchi yako uone utakavyofanywa) ndipo walipotolewa nchini na kupelekwa Khaybar.

Walikuwepo Khaybar wakati wote wa maisha ya Mtume,Khalifa wa kwanza Abubakri mpaka wakati wa Khalifa wa pili Umar aliyekuja kuwaondosha na kuelekea Iraq.
 
The originator of the thread has the benefit of being close to the mashujaa wa harakati za Uhuru wa Tanganyika the major shortcoming though is his inclination towards one religion which passionately contends as being the vanguard of the Uhuru struggle but later on was systematically relegated to a novice and it's leaders persecuted!

If I may ask, Nyerere came to Dar in 1952( as the very first educated man and with inclination to modern /Westminister politics) why then was he carried shoulder high by the "John. Okello"of Then Tanganyika?

MS seem to place so much faith and sweat on money (financial resources) sacrificed by Mzee Dossa, Rupia etc but he is conviiently forgetting that money by itself is a non starter. Kama fwezais everything, Akins papa msoffe wangelikuwa meta ani. MS it takes two to tango! After all Mwalimu is not here to respond to your......
 
Hapa historia haikuwa jumuishi hata kidogo
 
Wanaukumbi,

HISTORIA ya TANU ingelipotea kabisa kama siyo juhudi za makusudi za Profesa John Illife wa Cambridge aliyekuwa mwalimu wa historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ya katikati ya 1960.

Illife alipogundua tatizo lililokuwapo katika historia ya uhuru wa Tanganyika na hasa historia ya TANU na nafasi ya Julius Nyerere katika kuanzishwa kwake alifanya azma ya kuitafiti na kuiandika. John Illife aliwaagiza wanafunzi wake kutafiti na kuandika maisha ya wazalendo waliofanya mambo ya kutukuka katika sehemu zao. Zoezi hili lilipokamilika palipatikana historia za wazalendo wengi na kazi hii ikazaa kitabu Modern Tanzanians ambacho Iliffe alikihariri na yeye mwenyewe akiwa mmoja wa watu waliochangia uandishi akaandika maisha ya Martin Kayamba.

Kitabu hiki kina habari za maisha ya Watanganyika 12 ambao waliishi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini wakati wa utawala wa Wajerumani hadi kufika kwa Waingereza. Katika kitabu hiki kitu kimoja kinachojitokeza dhahiri ni kuwa wazalendo wote walioshiriki katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika walikuwa Waislam. (Kleist Sykes, Ali Ponda na Hassan Suleiman) wao maisha yao yalijikita katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza wakati wenziwao Wakristo Canon Kolumba Msigala, Pastor Yohane Nyagava na Bishop Jeremiah Kissula) historia ya maisha yao ilikuwa katika nyanja za utumishi wa kanisa.

Hali hii imeendelea hadi ilipofika wakati wa kuasisiwa kwa TANU. Katika ukweli huu ndipo palipo tatizo la wanahistoria kuiogopa historia ya kweli ya TANU kwa kuwa harakati zilichukua mkondo mkali wa Waislam kupinga ukoloni kwa dhati. Kwa ajili hii basi historia nzima ya kudai uhuru imejaa majina ya Waislam. Hili ni moja ya sababu inayofanya historia hii iwe nyeti, iogopewe na isitafitiwe na kuandikwa inavyopaswa. Hili ni tatizo la kwanza.

Tatizo la pili ni watafiti kwa hofu au kwa kutaka kujipendekeza kwa Mwalimu Julius Nyerere kupuuza michango ya wale waliokuwa katika harakati za kupambana na ukoloni ama kabla ya Nyerere au walikuwa pamoja nae. Watafiti hawa pamoja na hata wanasiasa ndani ya TANU kwa wakati ule wakawa wanashindana katika kumjazia sifa Mwalimu Nyerere kuwa kwa hakika kabla yake hapakuwa na harakati zozote za kutaka kuikomboa Tanganyika. Hali hii iliendelea kwa kipindi kirefu hadi kwa mara ya kwanza mmoja kati ya waasisi wa TANU, marehemu Joseph Kasella Bantu alipoandika kueleza mchango wake katika kuunda TANU.

Katika makala ile Kasella Bantu alijigamba kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyeitisha mkutano mkuu wa mwaka 1954(New African March 1985). Kassela Bantu ikawa hapa kama vile kafungua sanduku la Pandora kwa kuwa palitokea watu wakampinga kuwa hakusema kweli yote katika nukta ile. Mwandishi wa makala hii akiwa mmojawapo alimpinga Kassela Bantu (New African May 1985) kwa kusema kuwa kama ipo haja ya kutoa sifa kwa mtu mmoja mmoja basi sifa ile alistahili zaidi marehemu Abdulwahid Sykes. Mchango wa familia ya Sykes katika kuiasisi African Association na baadae TANU umejipembua vyema na unafahamika. Huu ndio ukweli wa historia ya TANU na mambo yalivyokuwa kati ya mwaka 1929 ilipoasisiwa African Association (AA) hadi 1954 TANU ilipozaliwa, iwe wanahistoria wanatambua au vinginevyo.

Sasa kwa kujua au kutojua Mwalimu Nyerere ambae maisha yake yote hakupenda kuizungumzia historia ya TANU au habari za wazalendo waliokuwapo katika siasa kabla yake, katika kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Busara mjini Tabora Mwalimu Nyerere alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa kuwatambua wazalendo walioijenga TANU kati ya mwaka 1954 - 1958. Sababu ya kusema maneno hayo lilikuwa swali aliloulizwa katika mkutano wa hadhara na Mzee Ramadhani Singo mmoja wa wanachama shupavu wa TANU Tabora. Singo alimkabili Mwalimu Nyerere na kumuuliza Mwalimu mbona umetusahau wenzako? Swali lile liligusa hisia za Mwalimu na ile hadhira iliyokuwapo pale. Ndiyo katika kujibu swali lile Mwalimu Nyerere akawaadhimisha mashujaa walioingia TANU zile siku za mwanzo.

Kikundi kile cha wapigania uhuru wa TANU waliokuwa pale mkutanoni mbele ya Mwalimu takriban wote walikuwa wazee katika kanzu mbovu na nguo zilizochakaa. Katika hali ile hawakutoa picha iliyompendeza yeyote. Mwalimu Nyerere akiwa hakika katahayari kwa kuwaona wapigania uhuru wenzake walivyokuwa taabani aliona ipo haja kwa wakati na saa ile kuwaadhimisha. Ndipo aliposema waasisi wa TANU waheshimiwe. Sasa basi kwa Mwalimu Nyerere tokeo kama hili lilikuwa la pili kumtokea. Hali kama ile ilimtokea Kizota alipokutana na Dossa Aziz.

Mwaka 1987 katika Mkutano maarufu wa Kizota ndipo Nyerere alikutana na Dossa Aziz uso kwa uso baada ya miaka mingi kupita. Dossa mfadhili mkubwa wa Mwalimu na TANU alikuwa kachoka kwa shida. Dossa sasa alikuwa masikini na hali yake haikuweza kujificha. Kila aliyemjua Dossa na enzi zake alishtushwa na hali yake. Inasemekana hata nguo za kuvaa kuja katika mkutano wa Kizota ilibidi anunuliwe na rafiki yake mpenzi toka utotoni waliosoma darasa moja hapo Shule ya Kichwele (sasa Shule ya Uhuru) Balozi Abbas Sykes. Dossa aliweka mfuko wake wazi kwa Nyerere na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Kadi yake ya TANU ni namba 4. Dossa ndiye aliipa TANU gari yake ya kwanza Land Rover ambayo ndiyo iliyomtembeza Nyerere nchi nzima wakati wa kuitangaza TANU kwa wananchi.

Waliomjua Dossa na ukarimu wake walilia kwa kwikwi wakati wa mazishi yake. Waliona uchungu kwa kuwa Dossa hakuwa mtu wa kupanga foleni kungoja tiba Hospitali ya Tumbi. Hali ya Dossa ilimgusa sana Mwalimu Nyerere na haikupita muda Mwalimu alimnunulia Dossa gari imsaidie.

Turudi kwa Baba wa Taifa. Sasa kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwaka hali kama ile ya Dossa aliyoiona Kizota alikuwa anaiona tena kwa wazee wa Tabora wapigania uhuru wa Tanganyika waliochoka na kupigwa sawasawa na ufukara. Ilikuwa lazima Mwalimu aseme kitu kuhusu hawa wazalendo aliowasahau au waliosahauliwa na historia na wakati. Mwalimu kwa kuwatukuza waasisi wale alisema kuwa siku za mwanzo za TANU zilikuwa ngumu na chama lazima kiwaheshimu wale wanachama wa mwanzo. Kwa kauli ile Mwalimu Nyerere akawa kanifungulia mimi njia ya kupita kwa kuunga mkono maneno yake. Nikaandika makala ambayo kwa mara ya kwanza nikasema kuwa historia ya TANU haiwezi kukamilika bila kutaja mchango wa Waislam na bila ya kumtaja Abdulwahid na Ally Sykes, Saadani Abdu Kandoro, John Rupia na Dossa Aziz (In Praise of Ancestors: Africa Events March/April 1988).

Mwalimu alichukua uongozi wa TAA toka kwa Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huu una kisa kirefu cha kusisimua wakati mwalimu wa shule asiyejulikana Julius Nyerere kutoka Musoma alipomuangusha kwa kura chache sana ndani ya Ukumbi wa Arnatouglou Abdulwahid Sykes, kijana maarufu wa mjini na mtoto wa mmoja wa waasisi wa African Association ambaye baba yake, Kleist Sykes alifanya mengi katika maendeleo ya Waafrika kati ya vita kuu mbili za dunia. Inasikitisha sana kuona kuwa kipande hiki cha kupokezana uongozi kati ya marehemu Abdulwahid Sykes na Nyerere ni katika historia inayofanywa nyeti.

Wanasiasa wetu na hata Nyerere mwenyewe katika umri wake wote wa siasa aliijenga fikra yake vyema kiasi kuwa alifanikiwa kufuta katika ubongo wake ni vipi alikuja kupata uongozi wa TAA. Katika maisha yake yote hakupata hata siku moja kutamka majina ya wazalendo wenzake aliokuwa nao kati ya mwaka 1953 hadi 1961 Tanganyika ilipojikomboa.

Katika kupuuza historia ya siasa kabla ya kuja kwa Mwalimu Nyerere viongozi wetu imewalazimu kubadilisha msamiati. TAA chama ambacho kilidumu kwa miongo miwili kikipigania haki ya Mwafrika kikawa baada ya kuundwa TANU kinakejeliwa na wanasiasa wapya na watafiti wa historia ya uhuru wa Tanganyika. Ikawa kila inapotajwa TAA ile sura yake ya chama cha siasa huvuliwa kikaitwa chama cha starehe. Kwa maana ya kuwa TAA haikuwa lolote hadi Nyerere alipofika na wasemavyo wenyewe kuanzisha TANU.

Kwa mantiki hii ikawa lazima ilazimishwe kuwa TANU iliasisiwa na Mwalimu Nyerere peke yake bila ya msaada wa yeyote. Huu ndio ukawa mwelekeo hata wa Mwalimu Nyerere. Historia yote ya nyuma hadi kufikia mwaka 1954 ilipoundwa TANU ikazikwa na ikawa kama vile ni usaliti kuwataja wazalendo wengine waliokuwa katika siasa kabla ya Mwalimu Nyerere.

Leo hii wangapi wanajua kuwa siku ya mwisho walipokubaliana kuunda TANU mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAA New Street kwenye chumba kidogo kilichukuwa na samani duni? Ndani ya chumba kile walikuwapo wanakamati ya ndani ya TAA - Abdulwahid, Ally, Dossa, Mzee Rupia na Nyerere. Baadhi yao katika chumba kile walikuwa wamepindua masanduku ya bia na kuyakalia kwa kuwa viti vilikuwa havitoshi. Vyumba katika ofisi ile ya TAA vilikuwa vimepangishwa Muhindi aliyekuwa akifanya kazi ya kufua nguo (dobi).

Hiyo ndiyo siku walipokubaliana kuwa hapana sababu tena ya kusubiri. Wakati wa kupiga mbiu ya mgambo kuanzishwa TANU umefika. Baada ya uamuzi huu kufanyika Dar es Salaam, mjini Tabora Salum Abdallah na wazalendo wengine mmojawapo akiwa marehemu Abubakar Mwilima, George Magembe na wengine walikutana kwa siri kupanga mipango ya kumsafirisha Germano Pacha aliyekuwa katibu wa TAA Western Province kuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kuanzishwa kwa TANU Julai 7 1954.

Salum Abdallah hatajiki popote katika historia ya TANU lakini ana kisa cha kusisimua katika maisha yake ya siasa kuanzia mwaka 1947 hadi alipowekwa kizuizini mwaka 1964 akiwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway Africa Union (TRAU). Salum Abdallah amekufa akiwa ameacha nyuma hazina kubwa ya kumbukumbu ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Vipi leo tuambiwe bila hata ya chembe ya aibu ati African Association iliyokuja kubadilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association kilikuwa chama cha starehe?

Historia ya TANU yenyewe inakataa hili achilia mbali historia ya mzalendo mmoja mmoja na michango yao katika kudai uhuru. Kumbukumbu hizi zina uwezo wa kumsisimua mtafiti yeyote. Inasikitisha na kutia hofu kuwa nyaraka nyingi za TANU na nyingine zinazomuhusu Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa historia ya nchi hii ziko mikononi mwa watu binafsi na nyingine hazitopatikana kabisa.

Mathalan wangapi leo wanajua habari za Erika Fiah au Ramadhani Mashado Plantan. Hawa ndio wazalendo wa mwanzo kufungua magazeti yaliyokuwa sauti ya Waafrika. Fiah alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa wa mrengo wa kushoto na kalamu yake katika gazeti lake Kwetu alilolianzisha mwaka 1937 ilikuwa ikitema cheche kali dhidi ya ukoloni.

Nani anajua kuwa gazeti la kwanza kumpa Mwalimu sauti na kueneza sera za TANU lilikuwa Zuhra mhariri akiwa Plantan? Makala za Fiah katika gazeti lake la Kwetu ingawa zimeandikwa zaidi ya nusu karne sasa bado zina msisimko kwa msomaji kama vile kaziandika jana.

Au nani leo anamjua Mzee Yusuf Olotu maarufu Yusuf Ngozi wa Moshi na jitihada zake za kuipa TANU ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Kura Tatu mjini Moshi. Au mchango wa Sheikh Yusuf Badi wa Lindi au mchango wa Dk Michael Lugazia, Dk Luciano Tsere, Dk Joseph Mutahangarwa, Dk Vedasto Kyaruzi, Dk Wilbard Mwanjisi na wengineo?

Kwa kuhitimisha, haya niliyoandika ni mifano michache tu katika dondoo za historia ya nchi yetu. Naamini wapo wazalendo wengi huko mikoani ambao kwa njia moja au nyingine wamefanya mengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Kizazi kilichopo sasa kina wajibu mkubwa wa kutafiti habari zao, kuzihifadhi na kuwapa heshima wanayostahili.

Alipokufa Dossa Aziz ilipofika wakati wa CCM kutoa rambirambi zao hawakujua waseme nini kwa kuwa viongozi waliokuwapo hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua mchango gani Dossa alitoa kwa Nyerere na TANU na kwa bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere hakuhudhuria mazishi yale.

Juma Volter Mwapachu katika tanzia aliyomwandikia Dossa, Dossa Aziz a Fallen Hero (The African 12 May 1998) alimlaumu Mwalimu kwa kukaa kimya kuhusu wapigania uhuru wenzake kiasi kuwa hakuna chochote kinachojulikana kuhusu mchango wao.

Hali hii ilijitokeza pia katika mazishi ya Mzee Paul Bomani hakuelezwa kama ilivyostahili. Kwanini tuogope kuieleza historia vilivyo?
Mmoja yupo gerezani lwa kesi mchongo,wengine waliwakimbiza vijizee chakavu,mwishowe vikaamua kutupa tutaulo twao na kukimbilia vichakani kwa kusitiriwa na wanamitutu!
 
Back
Top Bottom