Wako wapi Mashujaa wa Uhuru wa Tanganyika?

Wako wapi Mashujaa wa Uhuru wa Tanganyika?

Gurudumu lile lile tunalizungusha tu; histohisia siyo historia. Umewanasa wasiojua historia ya Tanganyika au wale walio wasionauwezo wa kung'amua makosa kadha wa kadha ya kihistoria unayoyafanya katika kuigeuza historia ya kupigania uhuru kuwa ya Waislamu Vs. Wakristu na Wengine...

Kila siku unaambiwa uweke Historia ya Tanganyika ambayo wewe unaijuwa...matokeo yake unajificha chini ya kibao cha Mbuzi kisha unatokeza kichwa tu na kukosoa na kukashifu za wenzio...
 
Nafikiri haijarishi mababuzetu waliipigania uhuru wa nchi hii walikuwa ni wa dini gani au kabila fulani . Kwa maono yako walifanya hivyo kwasababu tu walikuwa waisilamu? I don't think so. Your argument holds no substance. Nivizuri tuwakumbuke na kuwaenzi ipasavyo.
 
Gurudumu lile lile tunalizungusha tu; histohisia siyo historia. Umewanasa wasiojua historia ya Tanganyika au wale walio wasionauwezo wa kung'amua makosa kadha wa kadha ya kihistoria unayoyafanya katika kuigeuza historia ya kupigania uhuru kuwa ya Waislamu Vs. Wakristu na Wengine...
Yaani huyu jamaa sijui yukoje...ameshindwa kabisa kutambua kuwa hizi ngano zake hazina tena mvuto ila kwa watu wale waleee, eti wanafyonza sijui kitu gani vile! Hii age ya internet utamdanganya nani, thubutu! Uzuri ni kwamba hao anaowatembeza akiwanadi, hakuna hata moja aliyewahi kuchaguliwa kwa kura kuongoza hata kamtaa, si Gerezani wala Kipata. Hana tofauti na mtu anayeshinda analowa jasho kwa kuusukuma ukuta na akitoka hapo anajipongeza kwa kufanya kazi kubwa siku nzima huku ukuta bado umesimama pale pale! Kaazi kweli kweli!
Ukisoma hiyo habari hakuna kitu kipya hata kimoja. Niwatanabiashe wakubwa kuwa hizi ni mbinu za kukwepa hoja. Ule uzi wa Islam's role../ unaoendelea Mohamed Said anakabliwa na mambo ya kujibu. Hii ni ku divert attention tu.

1. Imedhihirika kuwa kuna wazee walifanya Matambiko. Kwa mujibu wa dini hilo ni kosa 'shirk'. Kwa mujibu wa Mohamed Said hawa ni sehemu ya wazee walionyima fursa na kusahaulika. Kwa mujibu wa wadau kwanini Mohamed anachagua muda wa makundi? Ametakiwa aeleze wapi makala za wapigania uhuru waliofanya matambiko?
Je si sehemu ya wapigania uhuru?

2. Imebainika kuwa Nyerere alipewa pesa, mboga na makapu ya misaada ya chakula. Kwa mujibu wa wadau, Mohamed ameombwa aeleze nani aalikuwa anamnunulia Nyerere sigareti?

3. Kuna paper mbili za karibuni zinaeleza kuhusu K.Sykes. Moja inasema yeye ni mwanzilishi wa AA, nyingine inasema ni katibu mwanzilishi wa AA. Wadau wanahoji mbona kuna flip flops kila paper inapotoka? Na inakuwaje chama kimeanza na katibu tu! wapi rais wa chama?

4. Kasema waislam walipigania uhuru. Wadau wanauliza ushahidi wa wazee hao kuhusu kauli hiyo upo wapi?
Kuna ushahidi kuwa walipigania uhuru kumkomboa mwafrika.

5. Kasema wazee hawaenziwi. Wadau wakauliza medali zinatoka Mohamed anataka waenziwe kwa kitu gani.

6. Kasema role ya Mshume ni kubwa kuliko ya Kyaruzi Vedastus, wadau wanauliza lini mshume aliongoza chama hata kwa dakika 10 kiasi cha kuwa na CV ya kisiasa kumzidi Dr Kyaruzi?

Wadau wanasubiri majibu, ghafla nyuzi kama ile ikiwa na rangi ya chanikiwiti badala ya hudhurungi inaibuka tena.

Ilitakiwa wewe uje na historia yako unayo ijua ili tulinganishe kati ya wewe moh'd said ni ipi historia ya kweli,punguza kucopy na kupaste.
 
Ungedai UISLAM kupuuzwa ingekua uhuru uliopiganiwa ungekuwa dhidi ya shetani ili tuipate pepo ningekuelewa, lakini uhuru huu wa tanganyika mtu ajisifie au asifiwe kwa uislam au ukristo wake!!!!! dini ina nini na uhuru wa nyama!!!!!
Hii kiu ya SIFA inatutia ujuha sasa.
 
Tunashukuru sana mzee mohamed said kwa kututoa ukungu, mungu awarehemu wazee wetu mashujaa waliotangulia mbele ya haki
 
Nani anajua mchango wa mzee Lameck Makalanga Bogohe, moja ya watu waliopendekeza jina la TANU, ingawa walikuja kutofautiana na mwalimu baadaye, na kuwekwa kizuizini?

Wanaukumbi,

HISTORIA ya TANU ingelipotea kabisa kama siyo juhudi za makusudi za Profesa John Illife wa Cambridge aliyekuwa mwalimu wa historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika miaka ya katikati ya 1960.

Illife alipogundua tatizo lililokuwapo katika historia ya uhuru wa Tanganyika na hasa historia ya TANU na nafasi ya Julius Nyerere katika kuanzishwa kwake alifanya azma ya kuitafiti na kuiandika. John Illife aliwaagiza wanafunzi wake kutafiti na kuandika maisha ya wazalendo waliofanya mambo ya kutukuka katika sehemu zao. Zoezi hili lilipokamilika palipatikana historia za wazalendo wengi na kazi hii ikazaa kitabu “Modern Tanzanians” ambacho Iliffe alikihariri na yeye mwenyewe akiwa mmoja wa watu waliochangia uandishi akaandika maisha ya Martin Kayamba.

Kitabu hiki kina habari za maisha ya Watanganyika 12 ambao waliishi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini wakati wa utawala wa Wajerumani hadi kufika kwa Waingereza. Katika kitabu hiki kitu kimoja kinachojitokeza dhahiri ni kuwa wazalendo wote walioshiriki katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika walikuwa Waislam. (Kleist Sykes, Ali Ponda na Hassan Suleiman) wao maisha yao yalijikita katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza wakati wenziwao Wakristo Canon Kolumba Msigala, Pastor Yohane Nyagava na Bishop Jeremiah Kissula) historia ya maisha yao ilikuwa katika nyanja za utumishi wa kanisa.

Hali hii imeendelea hadi ilipofika wakati wa kuasisiwa kwa TANU. Katika ukweli huu ndipo palipo tatizo la wanahistoria kuiogopa historia ya kweli ya TANU kwa kuwa harakati zilichukua mkondo mkali wa Waislam kupinga ukoloni kwa dhati. Kwa ajili hii basi historia nzima ya kudai uhuru imejaa majina ya Waislam. Hili ni moja ya sababu inayofanya historia hii iwe nyeti, iogopewe na isitafitiwe na kuandikwa inavyopaswa. Hili ni tatizo la kwanza.

Tatizo la pili ni watafiti kwa hofu au kwa kutaka kujipendekeza kwa Mwalimu Julius Nyerere kupuuza michango ya wale waliokuwa katika harakati za kupambana na ukoloni ama kabla ya Nyerere au walikuwa pamoja nae. Watafiti hawa pamoja na hata wanasiasa ndani ya TANU kwa wakati ule wakawa wanashindana katika kumjazia sifa Mwalimu Nyerere kuwa kwa hakika kabla yake hapakuwa na harakati zozote za kutaka kuikomboa Tanganyika. Hali hii iliendelea kwa kipindi kirefu hadi kwa mara ya kwanza mmoja kati ya waasisi wa TANU, marehemu Joseph Kasella Bantu alipoandika kueleza mchango wake katika kuunda TANU.

Katika makala ile Kasella Bantu alijigamba kwa kusema kuwa yeye ndiye aliyeitisha mkutano mkuu wa mwaka 1954(New African March 1985). Kassela Bantu ikawa hapa kama vile kafungua sanduku la Pandora kwa kuwa palitokea watu wakampinga kuwa hakusema kweli yote katika nukta ile. Mwandishi wa makala hii akiwa mmojawapo alimpinga Kassela Bantu (New African May 1985) kwa kusema kuwa kama ipo haja ya kutoa sifa kwa mtu mmoja mmoja basi sifa ile alistahili zaidi marehemu Abdulwahid Sykes. Mchango wa familia ya Sykes katika kuiasisi African Association na baadae TANU umejipembua vyema na unafahamika. Huu ndio ukweli wa historia ya TANU na mambo yalivyokuwa kati ya mwaka 1929 ilipoasisiwa African Association (AA) hadi 1954 TANU ilipozaliwa, iwe wanahistoria wanatambua au vinginevyo.

Sasa kwa kujua au kutojua Mwalimu Nyerere ambae maisha yake yote hakupenda kuizungumzia historia ya TANU au habari za wazalendo waliokuwapo katika siasa kabla yake, katika kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Busara mjini Tabora Mwalimu Nyerere alitoa hotuba kuhusu umuhimu wa kuwatambua wazalendo walioijenga TANU kati ya mwaka 1954 - 1958. Sababu ya kusema maneno hayo lilikuwa swali aliloulizwa katika mkutano wa hadhara na Mzee Ramadhani Singo mmoja wa wanachama shupavu wa TANU Tabora. Singo alimkabili Mwalimu Nyerere na kumuuliza ‘Mwalimu mbona umetusahau wenzako?’ Swali lile liligusa hisia za Mwalimu na ile hadhira iliyokuwapo pale. Ndiyo katika kujibu swali lile Mwalimu Nyerere akawaadhimisha mashujaa walioingia TANU zile siku za mwanzo.

Kikundi kile cha wapigania uhuru wa TANU waliokuwa pale mkutanoni mbele ya Mwalimu takriban wote walikuwa wazee katika kanzu mbovu na nguo zilizochakaa. Katika hali ile hawakutoa picha iliyompendeza yeyote. Mwalimu Nyerere akiwa hakika katahayari kwa kuwaona wapigania uhuru wenzake walivyokuwa taabani aliona ipo haja kwa wakati na saa ile kuwaadhimisha. Ndipo aliposema waasisi wa TANU waheshimiwe. Sasa basi kwa Mwalimu Nyerere tokeo kama hili lilikuwa la pili kumtokea. Hali kama ile ilimtokea Kizota alipokutana na Dossa Aziz.

Mwaka 1987 katika Mkutano maarufu wa Kizota ndipo Nyerere alikutana na Dossa Aziz uso kwa uso baada ya miaka mingi kupita. Dossa mfadhili mkubwa wa Mwalimu na TANU alikuwa kachoka kwa shida. Dossa sasa alikuwa masikini na hali yake haikuweza kujificha. Kila aliyemjua Dossa na enzi zake alishtushwa na hali yake. Inasemekana hata nguo za kuvaa kuja katika mkutano wa Kizota ilibidi anunuliwe na rafiki yake mpenzi toka utotoni waliosoma darasa moja hapo Shule ya Kichwele (sasa Shule ya Uhuru) Balozi Abbas Sykes. Dossa aliweka mfuko wake wazi kwa Nyerere na TANU katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Kadi yake ya TANU ni namba 4. Dossa ndiye aliipa TANU gari yake ya kwanza – Land Rover ambayo ndiyo iliyomtembeza Nyerere nchi nzima wakati wa kuitangaza TANU kwa wananchi.

Waliomjua Dossa na ukarimu wake walilia kwa kwikwi wakati wa mazishi yake. Waliona uchungu kwa kuwa Dossa hakuwa mtu wa kupanga foleni kungoja tiba Hospitali ya Tumbi. Hali ya Dossa ilimgusa sana Mwalimu Nyerere na haikupita muda Mwalimu alimnunulia Dossa gari imsaidie.

Turudi kwa Baba wa Taifa. Sasa kwa mara ya pili katika kipindi kisichozidi mwaka hali kama ile ya Dossa aliyoiona Kizota alikuwa anaiona tena kwa wazee wa Tabora – wapigania uhuru wa Tanganyika waliochoka na kupigwa sawasawa na ufukara. Ilikuwa lazima Mwalimu aseme kitu kuhusu hawa wazalendo aliowasahau au waliosahauliwa na historia na wakati. Mwalimu kwa kuwatukuza waasisi wale alisema kuwa siku za mwanzo za TANU zilikuwa ngumu na chama lazima kiwaheshimu wale wanachama wa mwanzo. Kwa kauli ile Mwalimu Nyerere akawa kanifungulia mimi njia ya kupita kwa kuunga mkono maneno yake. Nikaandika makala ambayo kwa mara ya kwanza nikasema kuwa historia ya TANU haiwezi kukamilika bila kutaja mchango wa Waislam na bila ya kumtaja Abdulwahid na Ally Sykes, Saadani Abdu Kandoro, John Rupia na Dossa Aziz (In Praise of Ancestors: Africa Events March/April 1988).

Mwalimu alichukua uongozi wa TAA toka kwa Abdulwahid Sykes. Uchaguzi huu una kisa kirefu cha kusisimua wakati mwalimu wa shule asiyejulikana Julius Nyerere kutoka Musoma alipomuangusha kwa kura chache sana ndani ya Ukumbi wa Arnatouglou Abdulwahid Sykes, kijana maarufu wa mjini na mtoto wa mmoja wa waasisi wa African Association ambaye baba yake, Kleist Sykes alifanya mengi katika maendeleo ya Waafrika kati ya vita kuu mbili za dunia. Inasikitisha sana kuona kuwa kipande hiki cha kupokezana uongozi kati ya marehemu Abdulwahid Sykes na Nyerere ni katika historia inayofanywa nyeti.

Wanasiasa wetu na hata Nyerere mwenyewe katika umri wake wote wa siasa aliijenga fikra yake vyema kiasi kuwa alifanikiwa kufuta katika ubongo wake ni vipi alikuja kupata uongozi wa TAA. Katika maisha yake yote hakupata hata siku moja kutamka majina ya wazalendo wenzake aliokuwa nao kati ya mwaka 1953 hadi 1961 Tanganyika ilipojikomboa.

Katika kupuuza historia ya siasa kabla ya kuja kwa Mwalimu Nyerere viongozi wetu imewalazimu kubadilisha msamiati. TAA chama ambacho kilidumu kwa miongo miwili kikipigania haki ya Mwafrika kikawa baada ya kuundwa TANU kinakejeliwa na wanasiasa wapya na watafiti wa historia ya uhuru wa Tanganyika. Ikawa kila inapotajwa TAA ile sura yake ya chama cha siasa huvuliwa kikaitwa ‘chama cha starehe.’ Kwa maana ya kuwa TAA haikuwa lolote hadi Nyerere alipofika na wasemavyo wenyewe kuanzisha TANU.

Kwa mantiki hii ikawa lazima ilazimishwe kuwa TANU iliasisiwa na Mwalimu Nyerere peke yake bila ya msaada wa yeyote. Huu ndio ukawa mwelekeo hata wa Mwalimu Nyerere. Historia yote ya nyuma hadi kufikia mwaka 1954 ilipoundwa TANU ikazikwa na ikawa kama vile ni usaliti kuwataja wazalendo wengine waliokuwa katika siasa kabla ya Mwalimu Nyerere.

Leo hii wangapi wanajua kuwa siku ya mwisho walipokubaliana kuunda TANU mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAA New Street kwenye chumba kidogo kilichukuwa na samani duni? Ndani ya chumba kile walikuwapo wanakamati ya ndani ya TAA - Abdulwahid, Ally, Dossa, Mzee Rupia na Nyerere. Baadhi yao katika chumba kile walikuwa wamepindua masanduku ya bia na kuyakalia kwa kuwa viti vilikuwa havitoshi. Vyumba katika ofisi ile ya TAA vilikuwa vimepangishwa Muhindi aliyekuwa akifanya kazi ya kufua nguo (dobi).

Hiyo ndiyo siku walipokubaliana kuwa hapana sababu tena ya kusubiri. Wakati wa kupiga mbiu ya mgambo kuanzishwa TANU umefika. Baada ya uamuzi huu kufanyika Dar es Salaam, mjini Tabora Salum Abdallah na wazalendo wengine mmojawapo akiwa marehemu Abubakar Mwilima, George Magembe na wengine walikutana kwa siri kupanga mipango ya kumsafirisha Germano Pacha aliyekuwa katibu wa TAA Western Province kuja Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa kuanzishwa kwa TANU Julai 7 1954.

Salum Abdallah hatajiki popote katika historia ya TANU lakini ana kisa cha kusisimua katika maisha yake ya siasa kuanzia mwaka 1947 hadi alipowekwa kizuizini mwaka 1964 akiwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway Africa Union (TRAU). Salum Abdallah amekufa akiwa ameacha nyuma hazina kubwa ya kumbukumbu ya harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Vipi leo tuambiwe bila hata ya chembe ya aibu ati African Association iliyokuja kubadilishwa jina na kuitwa Tanganyika African Association kilikuwa chama cha starehe?

Historia ya TANU yenyewe inakataa hili achilia mbali historia ya mzalendo mmoja mmoja na michango yao katika kudai uhuru. Kumbukumbu hizi zina uwezo wa kumsisimua mtafiti yeyote. Inasikitisha na kutia hofu kuwa nyaraka nyingi za TANU na nyingine zinazomuhusu Mwalimu Nyerere na uhuru wa Tanganyika kumbukumbu ambazo ni muhimu kwa historia ya nchi hii ziko mikononi mwa watu binafsi na nyingine hazitopatikana kabisa.

Mathalan wangapi leo wanajua habari za Erika Fiah au Ramadhani Mashado Plantan. Hawa ndio wazalendo wa mwanzo kufungua magazeti yaliyokuwa sauti ya Waafrika. Fiah alikuwa mmoja wa wanasiasa wa mwanzo kabisa wa mrengo wa kushoto na kalamu yake katika gazeti lake Kwetu alilolianzisha mwaka 1937 ilikuwa ikitema cheche kali dhidi ya ukoloni.

Nani anajua kuwa gazeti la kwanza kumpa Mwalimu sauti na kueneza sera za TANU lilikuwa Zuhra mhariri akiwa Plantan? Makala za Fiah katika gazeti lake la Kwetu ingawa zimeandikwa zaidi ya nusu karne sasa bado zina msisimko kwa msomaji kama vile kaziandika jana.

Au nani leo anamjua Mzee Yusuf Olotu maarufu Yusuf Ngozi wa Moshi na jitihada zake za kuipa TANU ushindi wa kishindo katika Uchaguzi wa Kura Tatu mjini Moshi. Au mchango wa Sheikh Yusuf Badi wa Lindi au mchango wa Dk Michael Lugazia, Dk Luciano Tsere, Dk Joseph Mutahangarwa, Dk Vedasto Kyaruzi, Dk Wilbard Mwanjisi na wengineo?

Kwa kuhitimisha, haya niliyoandika ni mifano michache tu katika dondoo za historia ya nchi yetu. Naamini wapo wazalendo wengi huko mikoani ambao kwa njia moja au nyingine wamefanya mengi katika historia ya uhuru wa Tanganyika. Kizazi kilichopo sasa kina wajibu mkubwa wa kutafiti habari zao, kuzihifadhi na kuwapa heshima wanayostahili.

Alipokufa Dossa Aziz ilipofika wakati wa CCM kutoa rambirambi zao hawakujua waseme nini kwa kuwa viongozi waliokuwapo hakuna hata mmoja aliyekuwa anajua mchango gani Dossa alitoa kwa Nyerere na TANU na kwa bahati mbaya sana Mwalimu Nyerere hakuhudhuria mazishi yale.

Juma Volter Mwapachu katika tanzia aliyomwandikia Dossa, ‘Dossa Aziz a Fallen Hero’ (The African 12 May 1998) alimlaumu Mwalimu kwa kukaa kimya kuhusu wapigania uhuru wenzake kiasi kuwa hakuna chochote kinachojulikana kuhusu mchango wao.

Hali hii ilijitokeza pia katika mazishi ya Mzee Paul Bomani hakuelezwa kama ilivyostahili. Kwanini tuogope kuieleza historia vilivyo?
 
Gurudumu lile lile tunalizungusha tu; histohisia siyo historia. Umewanasa wasiojua historia ya Tanganyika au wale walio wasionauwezo wa kung'amua makosa kadha wa kadha ya kihistoria unayoyafanya katika kuigeuza historia ya kupigania uhuru kuwa ya Waislamu Vs. Wakristu na Wengine...

Nakubaliana na wewe huyu jamaa unfortunately hata katika familia yake kuna wakristo lakini he is always biased against wakristo pengine kwasasbabu za kifamilia yake!!! Anapozungumzia wapigania Uhuru wa Tanganyika kwa mfano kutoka mkoa wa Dododma anamzungumzia sana Ali Ponda lakini hazungumzii mchango wa watu kama Edward Mwangosi!!! Waulize wazee wa Dodoma kama wakina Job Lusinde wakueleze mchango wa huyu mzee katika harakati za kugombea uhuru.
 
Hata kwenye Msiba wa Sokoine hakwenda na hakuwa na shughuli yoyote.
Sanasana akaagiza jeneza lipelekwe Ikulu kisha lifunuliwe na amuage then waende kumzika...

kadhalika kwa Kambona na Abdulwahed Sykes...

Je woote hao alikuwa bussy?
Ubussy huo ni ubussy gani?
Mbona nchi ilikuwa inaporomoka mikononi kwake kila uchwao?

Kuhudhulia mazishi sio ishara ya kugushwa sana na msiba husika; watu wengi wanahudhulia mazishi kwa kutaka publicity na unafiki!!! Nyerere alionesha mapenzi kwa rafiki zake wakati wa uhai wao na sio baada ya kufa; na ndio maana hawa watoto wa Mwapachu , Sykes na wakina Bomani aliwapa vyeo kwa sababu ya michango ya wazazi wao ingawa wengine wao leo wanadhani wamefika hapo walipo kwa juhudi zao pekee!!!
 
Nafikiri mdingi kashindwa kufanya analysis na kujua kama hizi porojo zake jamii inazisikiliza au lah...

Ila always kelele za chura huwa hazimzuii ng'ombe kunywa maji....

Hizi si porojo ni historia ya kweli yaliyo jiri na wasomaji wapo wengi wewe ukiwa mmojawapo, sioni tatizo lolote ,au una mengine ya kuhoji zaidi ya hili?
 
Asante ndugu Mohd Said kwa kweli ni burudani kujua taifa letu la Tanganyika lilitoka wapi.

Ni muda muafaka kuifufua Tanganyika yetu.
 
Gurudumu lile lile tunalizungusha tu; histohisia siyo historia. Umewanasa wasiojua historia ya Tanganyika au wale walio wasionauwezo wa kung'amua makosa kadha wa kadha ya kihistoria unayoyafanya katika kuigeuza historia ya kupigania uhuru kuwa ya Waislamu Vs. Wakristu na Wengine...

Yaani mpaka kichefuu chefu!
Watu wa aina kama hii ya Mohamed Said hawana tofauti na Al-Shabab.Kila kitu ni dini na ni vigumu kwao kuelewa na hawatapata kuwa na uelewa mpaka kiama chake maana kuna chuki ndani yake!

Mohamed said hao unaowaita wapigania uhuru wa Tanganyika (Waisilamu) labda usema walikuwa wanataka uhuru wa Bandari Salama -Dar Es Salaamu maana sijapata kusikia pakizungumzwa watu hao kuizunguaka Tanganyika katika harakati ya kudai Uhuru zaidi ya porojo za hapa Bandari Salama.

Lakini mbaya zaidi umewasahau Wazee wa Tanganyika kwa ujumla wao walistahili hicho unachozungumzia yaani kutambuliwa kila moja kwa nafasi yake toka vita ya Maji Maji na si hii porojo za watu 12 na tena bila haya unawaita waisilamu.

Tafuta watu wa aina au wenye Imani ya Al-shabab labda watakuelewa!(Shetani kwa kwenda Mbele)

Kitabu hiki kina habari za maisha ya Watanganyika 12 ambao waliishi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini wakati wa utawala wa Wajerumani hadi kufika kwa Waingereza. Katika kitabu hiki kitu kimoja kinachojitokeza dhahiri ni kuwa wazalendo wote walioshiriki katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika walikuwa Waislam. (Kleist Sykes, Ali Ponda na Hassan Suleiman) wao maisha yao yalijikita katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza wakati wenziwao Wakristo Canon Kolumba Msigala, Pastor Yohane Nyagava na Bishop Jeremiah Kissula) historia ya maisha yao ilikuwa katika nyanja za utumishi wa kanisa.
 
Yaani mpaka kichefuu chefu!
Watu wa aina kama hii ya Mohamed Said hawana tofauti na Al-Shabab.Kila kitu ni dini na ni vigumu kwao kuelewa na hawatapata kuwa na uelewa mpaka kiama chake maana kuna chuki ndani yake!

Mohamed said hao unaowaita wapigania uhuru wa Tanganyika (Waisilamu) labda usema walikuwa wanataka uhuru wa Bandari Salama -Dar Es Salaamu maana sijapata kusikia pakizungumzwa watu hao kuizunguaka Tanganyika katika harakati ya kudai Uhuru zaidi ya porojo za hapa Bandari Salama.

Lakini mbaya zaidi umewasahau Wazee wa Tanganyika kwa ujumla wao walistahili hicho unachozungumzia yaani kutambuliwa kila moja kwa nafasi yake toka vita ya Maji Maji na si hii porojo za watu 12 na tena bila haya unawaita waisilamu.

Tafuta watu wa aina au wenye Imani ya Al-shabab labda watakuelewa!(Shetani kwa kwenda Mbele)

Huyu hapo chini ni mimi nikikifanyia uchambuzi kitabu cha John Iliffe nikijiuliza mbona katika
siasa siwaoni Wakristo?

Watu hawa waliishi katika Tanganyika ya mwanzo wa karne ya ishirini.

Ulikuwa ndiyo mzao wa akina Kleist Sykes, Ali Juma Ponda, Hassan Taufik Suleiman na wengineo...
Vipi wewe haihangaishi ubongo wako?
Au uanaona ni sawa tu?

Kitabu hiki kina habari za maisha ya Watanganyika 12 ambao waliishi miaka ya mwanzo ya karne ya ishirini wakati wa utawala wa Wajerumani hadi kufika kwa Waingereza. Katika kitabu hiki kitu kimoja kinachojitokeza dhahiri ni kuwa wazalendo wote walioshiriki katika kutafuta Uhuru wa Tanganyika walikuwa Waislam. (Kleist Sykes, Ali Ponda na Hassan Suleiman) wao maisha yao yalijikita katika siasa za ukombozi wa Tanganyika kutoka ukoloni wa Waingereza wakati wenziwao Wakristo Canon Kolumba Msigala, Pastor Yohane Nyagava na Bishop Jeremiah Kissula) historia ya maisha yao ilikuwa katika nyanja za utumishi wa kanisa.
 
Nakubaliana na wewe huyu jamaa unfortunately hata katika familia yake kuna wakristo lakini he is always biased against wakristo pengine kwasasbabu za kifamilia yake!!! Anapozungumzia wapigania Uhuru wa Tanganyika kwa mfano kutoka mkoa wa Dododma anamzungumzia sana Ali Ponda lakini hazungumzii mchango wa watu kama Edward Mwangosi!!! Waulize wazee wa Dodoma kama wakina Job Lusinde wakueleze mchango wa huyu mzee katika harakati za kugombea uhuru.

Bulesi,
Nakuwekea hapa habari za Edward Mwangosi na Job Lusinde
kama nilivyoandika katika kitabu changu :

The Founding of TANU in Central Province 1955:
[TABLE="width: 660"]
[TR]
[TD]''...Tabora began to participate in active politics in 1945 when the African Association was introduced to the township from Dodoma through the efforts of Edward Mwangosi.

***

Mwangosi's stand was that Makererians were very important to the party as they would provide the required leadership.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]A total of about forty people attended the meeting including the Makererians, among them Job Lusinde, later to become minister, and Amon Nsekela, later to hold important posts in the government including Tanzania's High Commission to Britain.

Hassan Suleiman and Ali Ponda did not turn up for the meeting.

While they were assembling for the meeting, the officer-in-charge of the Community Center told them that he had received orders from the District Commissioner that the meeting should be cancelled and people dispersed immediately.

Alexander Kanyamara who was a wealthy African in Dodoma and a personal friend of John Rupia, now TANU Vice-President, called for the postponement of the meeting because of the absence of Hassan Suleiman and Ali Ponda-the TAA top leadership in Dodoma.

Due to this reason and the intimidating order from the DC, the meeting was cancelled without fixing a date for another meeting.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]The following morning Taratibu was arrested by the police and taken to the DC's office, the present Prime Minister's office.

Hassan Suleiman was there amicably chatting with the DC, Mr. Smith.

The DC started to interrogate Taratibu by asking him if he spoke English.

Taratibu replied that in the negative.

Speaking in English, Hassan Suleiman told the DC that he was the TANU secretary in Dodoma.

The DC Mr Smith accused Taratibu of forming an illegal organisation and for calling an unauthorized meeting at the Community Center the previous day which was likely to disrupt peace.

Without fear Taratibu replied that he had the mandate to call for a meeting because he was a member of a legally registered political party.

Taratibu fished out his black and green TANU card from his pocket and showed it to the DC. Mr. Smith asked Hassan Suleiman whether he too possessed a TANU card.

Hassan Suleiman had none.

Hassan Suleiman and the DC conversed in English for some time after which he asked both of them to write statements.

After writing his statement Taratibu was allowed to go home.

It is believed that at that time the only TANU members in Dodoma was Taratibu and Alexander Kanyamara who had bought his card in Dar es Salaam.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]When the Makerere graduates, who Mwangosi had put much faith in organizing the party, learned about Taratibu's ordeal with the DC Mr Smith, they were scared.

They decided to lie low and continue with their academic pursuits at the Kikuyu Secondary School.

Haruna Taratibu and Omari Suleiman now decided to change tactics; they called for a secret meeting at night in the house of Swedi bin Athman.[1]

The meeting decided that Taratibu should go to TANU headquarters in Dar es Salaam and talk to Julius Nyerere himself on the problems facing TANU in Dodoma.

Mahdi Mwinchumu who was TANU member in Dar es Salaam volunteered to accompany Taratibu to the party headquarters since he was known by the leadership there.

Said Musa, another member of the secret committee, also volunteered to accompany Taratibu and Mwinchumu to Dar es Salaam.

On departure day, Job Lusinde went to see the secret delegation off at the railway station.

Lusinde told the delegation that Makererians were in support of all the decisions taken by the secret committee.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Bwana Bulesi,
Ikiwa hujatosheka na habari hizi nifahamishe.

[1] Another version of the founding of TANU in Dodoma is that a meetimg of other patriots was called
in which Seif Waziri Kasembo attended in the house of Salim Omari, who was also present, together
with Fulka Mwinchumu Kinyozi, Swedi Athmani Kagulu, Bakari Omari, Fundi Issa, Mzee Magwila, Manywele
Bushiri, Mzee Ibrahim Sururu Mahusi Selemani, Omari Selemani, Nassoro Mussa, Athmani Nyange and others.
It seems there was rivalry between the two groups because in a paper made available to the author by Seif
Waziri Kasembo it is stated that Haruna Taratibu assumed leadership in Party affairs without the consent of
other patriots. Interesting is the fact that some of the names mentioned by Kasembo appear in both Taratibu
and Suleiman's narration. But the two groups, that of Taratibu and that of Kasembo, came to accommodate
each other because eventually, after office bearers had been elected, Kasembo provided his house as the first
TANU office in Dodoma. Kasembo's father, Waziri Kasembo, was once president of the African Association in
Dodoma.
 
Ukisoma hiyo habari hakuna kitu kipya hata kimoja. Niwatanabiashe wakubwa kuwa hizi ni mbinu za kukwepa hoja. Ule uzi wa Islam's role../ unaoendelea Mohamed Said anakabliwa na mambo ya kujibu. Hii ni ku divert attention tu.

1. Imedhihirika kuwa kuna wazee walifanya Matambiko. Kwa mujibu wa dini hilo ni kosa 'shirk'. Kwa mujibu wa Mohamed Said hawa ni sehemu ya wazee walionyima fursa na kusahaulika. Kwa mujibu wa wadau kwanini Mohamed anachagua muda wa makundi? Ametakiwa aeleze wapi makala za wapigania uhuru waliofanya matambiko?
Je si sehemu ya wapigania uhuru?

2. Imebainika kuwa Nyerere alipewa pesa, mboga na makapu ya misaada ya chakula. Kwa mujibu wa wadau, Mohamed ameombwa aeleze nani aalikuwa anamnunulia Nyerere sigareti?

3. Kuna paper mbili za karibuni zinaeleza kuhusu K.Sykes. Moja inasema yeye ni mwanzilishi wa AA, nyingine inasema ni katibu mwanzilishi wa AA. Wadau wanahoji mbona kuna flip flops kila paper inapotoka? Na inakuwaje chama kimeanza na katibu tu! wapi rais wa chama?

4. Kasema waislam walipigania uhuru. Wadau wanauliza ushahidi wa wazee hao kuhusu kauli hiyo upo wapi?
Kuna ushahidi kuwa walipigania uhuru kumkomboa mwafrika.

5. Kasema wazee hawaenziwi. Wadau wakauliza medali zinatoka Mohamed anataka waenziwe kwa kitu gani.

6. Kasema role ya Mshume ni kubwa kuliko ya Kyaruzi Vedastus, wadau wanauliza lini mshume aliongoza chama hata kwa dakika 10 kiasi cha kuwa na CV ya kisiasa kumzidi Dr Kyaruzi?

Wadau wanasubiri majibu, ghafla nyuzi kama ile ikiwa na rangi ya chanikiwiti badala ya hudhurungi inaibuka tena.

Nguruvi,
Hivi haijakupitikia kuwa mimi naburudika hapa JF?

Hebu panga vyema maswali nikujibu.

Unachanganya mambo mengi na ukifanya hivyo mnakasha
unakorogeka.
 
Nyerere ataendaje kwenye msiba wa soko4 wakati yeye ndio alimnaniliu!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nawasikitikia sana vijana wanaoendelea kudanganywa na huyu kiumbe aitwae Mohamed Said,

Kwawale wasiojua historia nawaomba msiwe wavivu na kuishia kuzisoma hizi ngano tu,

Tumieni mda wenu vizuri kusaka maandishi mengine ya kujenga uelewa wenu katika historia ya nchini yetu,

Ni ajabu uongo uleule kuendelezwa kwa mlango wa nyuma huku vijana wakiendelea kushangilia bila kujua madhara yake,
 
Kila siku unaambiwa uweke Historia ya Tanganyika ambayo wewe unaijuwa...matokeo yake unajificha chini ya kibao cha Mbuzi kisha unatokeza kichwa tu na kukosoa na kukashifu za wenzio...
Ni haki ya msomi yeyote kukosoa kazi ya mtu mwingine bila kujali kama yeye ameandika kazi yoyote au la!
 
Ilitakiwa wewe uje na historia yako unayo ijua ili tulinganishe kati ya wewe moh'd said ni ipi historia ya kweli,punguza kucopy na kupaste.
Kama hamzijui kanuni za kisomi kwanini mnajichomeka? Kwanini msikae pembeni mkawa watazamaji tu! Msiwe mnajitahidi kumtetea mzee wenu kwa hoja dhaifu kama hizi kwani mnazidi kumzamisha kwenye matope.
 
Back
Top Bottom