Wako wapi G55?

Setuba Noel

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
426
210
Na wana ushawishi gani kwa hoja hiyo kwa sasa? Hapa nawakumbusha kuhusu hawa wazee, maelezo mafupi kuwahusu, na kwa wale ambao sina habari zao wengine mjazie. Watu wa kuenziwa hawa:
  1. Njelu Kasaka: Huyu alikuwa mbunge wa Lupa mkoani Mbeya. Baada ya sakata lile mzee Ruksa alimpoza kwa kumzawadia unibu waziri. Katik hatua Fulani alikosana na wenye chama chao CCM walipomuengua kwenye kura za maoni, akakasirika akajiunga na CUF. Huko nako hazikuiva, njaa ilipomzidia akarudi "nyumbani" CCM. Msimamo wa CCM ni serikali mbili, kwa hiyo huyu kwenye wapigania Tanganyika keshapotezwa. Ni bahati mbaya sana kwani ndiye aliyekuwa kiongozi wa G55 mwaka ule wa 1993. .
  2. Lumuli Alipili Kasyupa: alikuwa mbunge wa Kyela kule kwa Mwakyembe. Yuko wapi?
  3. William Mpiluka: wa Mufindi, Iringa wakati huo. Yuko wapi? .
  4. Mateo Tluway Qares: alikuwa mbunge wa Babati ambayo wakati huo ilikuwa mkoa wa Arusha. Baadae alipewa uwaziri kwenye serikali iliyofuata ya Mkapa .
  5. Jared Gachocha: alikuwa mbunge wa Ngara. Yuko wapi?
  6. Dr Mganga Titus ole Kipuyo: alikuwa mbunge wa Arumeru Magharibi
  7. Phillip Sanka Marmo: huyu alikuwa mbunge wa Mbulu mkoani Arusha (wakati huo). Alipokuwa anapigania Tanganyika alikuwa ‘benchi', lakini katika serikali za awamu zilizofuata alipewa ulaji mfululizo wa uwaziri na sasa n balozi nchini China. Hana sababu tena ya kudai Tanganyika.
  8. Arcado Ntagazwa: huyu wakati huo alikuwa mbunge wa jimbo la Kibondo, na alikuwa ‘benchi' pia. Kabla ya sakata la kudai Tanganyika alikuwa waziri wa maliasili na utalii katika ile serikali ya mwanzo ya Mzee Ruksa. Baada ya ishu kuzimwa, alipozwa na posts za uwaziri ambazo aliendelea kula nchi hadi walipokuja kumtosa katika awamu ya JK, na kwa hasira akaamua kutimkia CHADEMA. Bado atakuwa anaitaka Tanganyika yake.
  9. Patrick Silvanus Qorro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Karatu (Arusha) ndiye ambaye baadaye alikuja kuwa chanzo cha CCM kupoteza jimbo kwa CHADEMA hadi leo. Wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 1995, marehemu Qorro alichuana na Dr Wilbrod Slaa ambaye ndiyo kwanza alikuwa ametoka kujiuzulu upadri na alikuwa amewekeza sana nguvu zake na mitandao yake katika miradi ya maendeleo Karatu, akitumia ushawishi alioujenga alipokuwa katibu mkuu wa TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki). Wana-CCM walimchagua Dr Slaa awe mgombea, lakini makao makuu wakatengua na kumweka Qorro. Dr Slaa alitimkia CHADEMA ambao walimpa tiketi ya kugombea, jimbo likabakia CHADEMA hadi leo. Mzee Qorro alifariki mapema mwaka huu.
  10. Japhet Sichona: wa Mbozi (Mbeya). Yuko wapi?
  11. Jenerali Twaha Khalfan Ulimwengu: huyu alikuwa mbunge wa Taifa (ndivyo walivyoitwa enzi hizo wale ambao hawakutokea majimboni). Kabla ya hapo aliwahi kuwa mkuu wa wilaya kule Hai, Kilimanjaro. Awamu iliyofuata ya Mzee Mkapa ilimnyanyasa sana huyu Ulimwengu kutokana na tabia yake ya "kushindana na serikali", tena kuna wakati walitangaza kuwa siyo raia na akalazimishwa kuomba upya uraia au kuondoka nchini (nakumbuka sakata lilimhusu pia Mzee Anatoly Amani yule anayegombana na Kagasheki kule Bukoba, na bi Maudline Castico aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM Zanzibar ). Mzee Ulimwengu ameendelea kuwa critical wa serikali lakini sasa hivi anafanya kwa upole si kama wakati ule walipomtishia kumtimua nchini. Bado ana guts za kudai Tanganyika?
  12. Abel K. Mwanga (marehemu): huyu alikuwa mbunge wa Musoma mjini, na pia alikuwa mwandishi mahiri wa vitabu vya kiada vya somo la kiingereza vilivyotumika katika shule za sekondari. Anatajwa pia kuwa ndiye aliyekuwa akimpa aliyekuwa waziri mkuu marehemu Edward Sokoine tuition ya lugha ya kiingereza. Mzee Mwanga alifariki mwaka 2009.
  13. Prof Aaron Eben Japhet Massawe: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, na kabla ya hapo alikuwa akifundisha katika chuo kikuu cha tiba Muhimbili. Ni mtaalamu bingwa wa magonjwa ya ngozi. Kwa sasa ni mstaafu anayetoa huduma za tiba katika hosptali yake binafsi. Ndoto za utanganyika hata kama bado anazo, hana nguvu nazo tena.
  14. Shashu Lugeye: alikuwa mbunge wa Solwa. Yuko wapi?
  15. Sebastian Rweikiza Kinyondo (marehemu): almaarufu "bwana mitemba", alivuta sana kiko huyu jamaa, na alikuwa na sharubu fulani ambazo akiweka mtemba wake mdomoni zilimpa mwonekano wa kipekee sana. Alikuwa mbunge wa Bukoba vijijini. Baada ya sakata lile huyu naye alipozwa kwa kupewa uwaziri wa Kazi ambao alidumu nao hadi kifo chake.
  16. Phares Kashemeza Kabuye (marehemu): Huyu babu alikuwa mbunge wa Biharamulo ambaye alihangaikia sana misimamo yake hadi kifo. Baada ya sakata lile, uchaguzi uliofuata wa 1995 alijiunga na chama cha NCCR Mageuzi enzi hizo kikiwika sana kuliko CHADEMA ya leo, chini ya ‘Mangi' Augustino Lyatonga Mrema na Katibu Mkuu wake Mabere Nyaucho Marando. Ulipotokea mtafaruku wa Marando na Mrema, Mzee Kabuye aliamua kuelekeza utiifu wake kwa Mrema, na akamfuata kwenye TLP yake ambako pia alishinda ubunge dhidi ya jamaa wa CCM aliyeitwa Anatoly Choya ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya mojawapo. Mzee Kabuye alifariki kwa ajali ya basi alipokuwa safarini kufuatilia rufaa ya kesi yake ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na Choya.
  17. Mbwete Polile Hombee: alikuwa mbunge wa Rungwe (Mbeya). Yuko wapi?
  18. Kisyeri Werema Chambiri: alikuwa mbunge wa Tarime. Yuko wapi?
  19. John Byeitima: alikuwa mbunge wa Karagwe. Yuko wapi?
  20. Abdallah Saidi Nakuwa: alikuwa wa Lindi. Yuko wapi?
  21. Dr Ndembwela Ngunangwa: alikuwa mbunge wa Njombe Kusini, mkoani Iringa (wakati huo Anna Makinda alikuwa mkuu wa Mkoa). Yuko wapi?
  22. Mathias Michael Kihaule (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ludewa (mkoa wa Iringa) wakati huo ambapo Horace Kolimba alikuwa Katibu mkuu wa CCM. Interestingly, Mzee Kihaule wakati anapigania Tanganyika alikuwa pia Naibu Spika wa Bunge. Baada ya sakata lile hakupata tena ubunge, CCM ilimtema na kumpa marehemu Horace Kolimba nafasi hiyo, huku Mzee Kihaule akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbarali, nafsi aliyodumu nayo hadi alipostaafu 2004. Mzee Kihaule alifariki mwaka 2012.
  23. Alhaji Mussa Nkhangaa: huyu alikuwa mbunge wa Iramba mkoani Singida. Baadaye katika serikali zilizofuata alipewa nyadhifa za uwaziri (ikiwemo ile ya waziri wa maji), na baadae akawa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
  24. Edward Oyombe Ayila: alikuwa mbunge wa Rorya. Yuko wapi?
  25. Adam Karumbeta: wa Mbeya huyu. Yuko wapi?
  26. Halimeshi Mayonga: alikuwa mbunge wa Kigoma vijijini. Yuko wapi?
  27. Dr John Katunzi: wa Geita. Yuko wapi?
  28. Ismail Ivwata: alikuwa Mbunge wa Manyoni Singida. Yuko wapi?
  29. Tobi Tajiri Mweri: alikuwa mbunge wa Pangani. Yuko wapi?
  30. Aidan Livigha: alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa (Lindi). Yuko wapi?
  31. Tabitha Ijumba Siwale (mama): Huyu alikuwa mbunge wa taifa, na kabla ya hapo aliwahi kuwa waziri katika wizara za elimu na baadaye ardhi. Kwa sasa ni mkurugenzi wa NGO iitwayo WAT (Women Advancement Trust), na pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Efatha Bank (ya nabii Mwingira).
  32. Obel Mwamfupe: wa Mbeya. Yuko wapi?
  33. Othman Ahmed Mpakani: wa Iringa magharibi. Yuko wapi?
  34. Evarist Mwanansao: wa Nkasi. Yuko wapi?
  35. Paschal Degera: wa Kondoa kaskazini. Yuko wapi?
  36. Erasto Losioki: wa Simanjiro. Yuko wapi?
  37. Nassoro Malocho: alikuwa mbunge wa Mtwara. Katika serikali iliyofuata ya Mhe Mkapa, aliteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais, Mipango.
  38. Charles Kagonji: huyu alikuwa mbunge wa Mlalo Lushoto. Alikuwa mwandishi wa habari ikulu enzi za Mwalimu Nyerere. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mzee Kagonji alikasirishwa na uchakachuaji aliofanyiwa na CCM kwenye kura za maoni akaamua kutimkia CHADEMA. Tofauti na wenzie waliotimkia CHADEMA kipindi hicho (akiwemo Hezekiah Wenje aliyekimbia CCM baada ya kuburuzana na Lawrence Masha kule Nyamagana) Mzee Kagonji alishindwa uchaguzi ule.
  39. Venance Francis Ngula: alikuwa mbunge wa Taifa. Katika uchaguzi uliofuata alichaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo Dar na kuteuliwa kuwa naibu waziri wa fedha.
  40. Benedict Kiroya Losurutia (marehemu): alikuwa mbunge wa Kiteto. Alifariki mwaka 2007.
  41. Dr Deogratias Mwita: wa Serengeti.Yuko wapi?
  42. Phineas Nnko: wa Arumeru Mashariki. Yuko wapi?
  43. John Peter Mwanga: alikuwa mbunge wa Moshi mjini na alikuwa miongoni mwa wabunge vijana wakati ule kwani alishinda ubunge akiwa anasubiria graduation yake pale Mzumbe. Ushindi wake mwaka ule wa 1990 dhidi ya Brigedia Muhiddin Kimario (ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani) zaidi ulitokana na kura alizopigiwa na wanafunzi wa sekondari na vyuo ambako ndiko alikowekeza zaidi nguvu kutokana na ushawishi wake kwenye UVCCM (ambao ulikuwa na matawi mashuleni na vyuoni) na MUWATA (Muungano wa wanavyuo Tanzania). Hata hivyo hakufanya lolote katika kipindi chake cha uongozi, kwahiyo alipotea kwenye ramani baada ya kipindi kimoja tu.
  44. Chediel Yohana Mgonja (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Same kwa miaka mingi, na enzi ya Nyerere aliwahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali ikiwemo Elimu. Anakumbukwa pia kwa ile kesi maarufu sana ya uchaguzi Same ya mwaka 1980-1982 ambako alishinda katika mahakama kuu lakini akaja kushindwa katika mahakama ya rufaa na kuvuliwa ubunge. Katika hukumu ya rufaa, aliadhibiwa kutogombea ubunge kwa miaka 10, lakini baadaye adhabu hiyo ilitenguliwa akaruhusiwa kugombea tena 1985 ambako alishinda na kushika vipindi viwili hadi 1995. Mzee Mgonja (ambaye wapare walimpa jina la utani "Kaghembe") alifariki mwaka 2009.
  45. Guntram Amani Itatiro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Ifakara. Baada ya sakata lile la kudai Tanganyika, Mzee Ruksa alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ule utaratibu wa kofia mbili.
  46. Captain (mstaafu) Paschal Kulwa Mabiti: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.
  47. Edith Mallya Munuo (mama): Huyu alikuwa mbunge wa Taifa akiwakilisha umoja wa Wanawake wa CCM (UWT). Katika uchaguzi uliofuata miaka 2 baadaye (1995) CCM ilimtosa, akaamua kujiunga na NCCR Mageuzi na kugombea jimbo la Kawe ambako hata hivyo alishindwa. Aliteuliwa kuingia kama mbunge wa viti maalum kupitia NCCR Mageuzi, na baada ya hapo kwa sababu zisizoeleweka akatangaza kubadilisha jina lake kuwa "Edith Lucina". Hivi yuko wapi siku hizi?
  48. Raphael Shempemba: wa Lushoto. Yuko wapi?
  49. Lt Col (mstaafu) John Mhina: wa Lushoto. Yuko wapi?
  50. Balozi George Maige Nhigula (marehemu): huyu alikuwa Mbunge wa Kwimba, Mwanza. Alikuwa muumini kwelikweli wa utanganyika maana alikuwa miongoni mwa maofisa wa mwanzo wa ubalozi za Tanganyika huru Ulaya miaka ya mwanzo ya uhuru. Alitumikia serikali miaka mingi kwa nyadhifa mbalimbali hadi alipostaafu mwaka 1985 na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Kwimba kwa vipindi viwili. Alistaafu siasa 1995 na kufariki mwaka 2011.
  51. Captain (mstaafu) Theodos James Kasapira (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ulanga magharibi, na kabla ya hapo alishakuwa mkuu wa wilaya mbalimbali. Capt Kasapira alifariki mwaka 2005.
  52. Charles Kinuno: alikuwa mbunge wa Nyanghwale. Yuko wapi?
  53. Christian Fundisha: wa Tabora Kusini. Yuko wapi?
  54. Samuel Ruangisa: alikuwa mbunge wa Bukoba Mjini kwa muda mrefu. Baadae CCM walimtosa kwenye ubunge lakini akabakia kwenye chama na kugombea udiwani na kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba. Mwaka jana Mhe Ruhangisa akiwa diwani wa kata ya Kitendaguro, alikuwa miongoni mwa wale madiwani wanane ambao CCM iliwafukuza uanachama kwa madai ya kumuunga mkono Kagasheki katika ugomvi wake dhidi ya aliyekuwa meya Anatoly Amani.
  55. Dr Maria Josephine Kamm (mama): huyu alikuwa mbunge wa taifa, na alipata umaarufu mkubwa akiwa headmistress wa secondary ya wasichana Weruweru ambayo pia ilikuwa maarufu sana enzi hizo. Kwa sasa Mama Kamm ni mstaafu, na ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Mama Clementina Foundation, asasi inayojishughulisha na elimu kwa wasichana.
 
Setuba Noel
ipangilie basi hiyo post ili isomeke vizuri. Kuna nondo nzuri hapo.
 
Last edited by a moderator:
Na wana ushawishi gani kwa hoja hiyo kwa sasa? Hapa nawakumbusha kuhusu hawa wazee, maelezo mafupi kuwahusu, na kwa wale ambao sina habari zao wengine mjazie. Watu wa kuenziwa hawa:
  1. Njelu Kasaka: Huyu alikuwa mbunge wa Lupa mkoani Mbeya. Baada ya sakata lile mzee Ruksa alimpoza kwa kumzawadia unibu waziri. Katik hatua Fulani alikosana na wenye chama chao CCM walipomuengua kwenye kura za maoni, akakasirika akajiunga na CUF. Huko nako hazikuiva, njaa ilipomzidia akarudi “nyumbani” CCM. Msimamo wa CCM ni serikali mbili, kwa hiyo huyu kwenye wapigania Tanganyika keshapotezwa. Ni bahati mbaya sana kwani ndiye aliyekuwa kiongozi wa G55 mwaka ule wa 1993. .
  2. Lumuli Alipili Kasyupa: alikuwa mbunge wa Kyela kule kwa Mwakyembe. Yuko wapi?
  3. William Mpiluka: wa Mufindi, Iringa wakati huo. Yuko wapi? .
  4. Mateo Tluway Qares: alikuwa mbunge wa Babati ambayo wakati huo ilikuwa mkoa wa Arusha. Baadae alipewa uwaziri kwenye serikali iliyofuata ya Mkapa .
  5. Jared Gachocha: alikuwa mbunge wa Ngara. Yuko wapi?
  6. Dr Mganga Titus ole Kipuyo: alikuwa mbunge wa Arumeru Magharibi
  7. Phillip Sanka Marmo: huyu alikuwa mbunge wa Mbulu mkoani Arusha (wakati huo). Alipokuwa anapigania Tanganyika alikuwa ‘benchi’, lakini katika serikali za awamu zilizofuata alipewa ulaji mfululizo wa uwaziri na sasa n balozi nchini China. Hana sababu tena ya kudai Tanganyika.
  8. Arcado Ntagazwa: huyu wakati huo alikuwa mbunge wa jimbo la Kibondo, na alikuwa ‘benchi’ pia. Kabla ya sakata la kudai Tanganyika alikuwa waziri wa maliasili na utalii katika ile serikali ya mwanzo ya Mzee Ruksa. Baada ya ishu kuzimwa, alipozwa na posts za uwaziri ambazo aliendelea kula nchi hadi walipokuja kumtosa katika awamu ya JK, na kwa hasira akaamua kutimkia CHADEMA. Bado atakuwa anaitaka Tanganyika yake.
  9. Patrick Silvanus Qorro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Karatu (Arusha) ndiye ambaye baadaye alikuja kuwa chanzo cha CCM kupoteza jimbo kwa CHADEMA hadi leo. Wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 1995, marehemu Qorro alichuana na Dr Wilbrod Slaa ambaye ndiyo kwanza alikuwa ametoka kujiuzulu upadri na alikuwa amewekeza sana nguvu zake na mitandao yake katika miradi ya maendeleo Karatu, akitumia ushawishi alioujenga alipokuwa katibu mkuu wa TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki). Wana-CCM walimchagua Dr Slaa awe mgombea, lakini makao makuu wakatengua na kumweka Qorro. Dr Slaa alitimkia CHADEMA ambao walimpa tiketi ya kugombea, jimbo likabakia CHADEMA hadi leo. Mzee Qorro alifariki mapema mwaka huu.
  10. Japhet Sichona: wa Mbozi (Mbeya). Yuko wapi?
  11. Jenerali Twaha Khalfan Ulimwengu: huyu alikuwa mbunge wa Taifa (ndivyo walivyoitwa enzi hizo wale ambao hawakutokea majimboni). Kabla ya hapo aliwahi kuwa mkuu wa wilaya kule Hai, Kilimanjaro. Awamu iliyofuata ya Mzee Mkapa ilimnyanyasa sana huyu Ulimwengu kutokana na tabia yake ya “kushindana na serikali”, tena kuna wakati walitangaza kuwa siyo raia na akalazimishwa kuomba upya uraia au kuondoka nchini (nakumbuka sakata lilimhusu pia Mzee Anatoly Amani yule anayegombana na Kagasheki kule Bukoba, na bi Maudline Castico aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM Zanzibar ). Mzee Ulimwengu ameendelea kuwa critical wa serikali lakini sasa hivi anafanya kwa upole si kama wakati ule walipomtishia kumtimua nchini. Bado ana guts za kudai Tanganyika?
  12. Abel K. Mwanga (marehemu): huyu alikuwa mbunge wa Musoma mjini, na pia alikuwa mwandishi mahiri wa vitabu vya kiada vya somo la kiingereza vilivyotumika katika shule za sekondari. Anatajwa pia kuwa ndiye aliyekuwa akimpa aliyekuwa waziri mkuu marehemu Edward Sokoine tuition ya lugha ya kiingereza. Mzee Mwanga alifariki mwaka 2009.
  13. Prof Aaron Eben Japhet Massawe: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, na kabla ya hapo alikuwa akifundisha katika chuo kikuu cha tiba Muhimbili. Ni mtaalamu bingwa wa magonjwa ya ngozi. Kwa sasa ni mstaafu anayetoa huduma za tiba katika hosptali yake binafsi. Ndoto za utanganyika hata kama bado anazo, hana nguvu nazo tena.
  14. Shashu Lugeye: alikuwa mbunge wa Solwa. Yuko wapi?
  15. Sebastian Rweikiza Kinyondo (marehemu): almaarufu “bwana mitemba”, alivuta sana kiko huyu jamaa, na alikuwa na sharubu fulani ambazo akiweka mtemba wake mdomoni zilimpa mwonekano wa kipekee sana. Alikuwa mbunge wa Bukoba vijijini. Baada ya sakata lile huyu naye alipozwa kwa kupewa uwaziri wa Kazi ambao alidumu nao hadi kifo chake.
  16. Phares Kashemeza Kabuye (marehemu): Huyu babu alikuwa mbunge wa Biharamulo ambaye alihangaikia sana misimamo yake hadi kifo. Baada ya sakata lile, uchaguzi uliofuata wa 1995 alijiunga na chama cha NCCR Mageuzi enzi hizo kikiwika sana kuliko CHADEMA ya leo, chini ya ‘Mangi’ Augustino Lyatonga Mrema na Katibu Mkuu wake Mabere Nyaucho Marando. Ulipotokea mtafaruku wa Marando na Mrema, Mzee Kabuye aliamua kuelekeza utiifu wake kwa Mrema, na akamfuata kwenye TLP yake ambako pia alishinda ubunge dhidi ya jamaa wa CCM aliyeitwa Anatoly Choya ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya mojawapo. Mzee Kabuye alifariki kwa ajali ya basi alipokuwa safarini kufuatilia rufaa ya kesi yake ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na Choya.
  17. Mbwete Polile Hombee: alikuwa mbunge wa Rungwe (Mbeya). Yuko wapi?
  18. Kisyeri Werema Chambiri: alikuwa mbunge wa Tarime. Yuko wapi?
  19. John Byeitima: alikuwa mbunge wa Karagwe. Yuko wapi?
  20. Abdallah Saidi Nakuwa: alikuwa wa Lindi. Yuko wapi?
  21. Dr Ndembwela Ngunangwa: alikuwa mbunge wa Njombe Kusini, mkoani Iringa (wakati huo Anna Makinda alikuwa mkuu wa Mkoa). Yuko wapi?
  22. Mathias Michael Kihaule (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ludewa (mkoa wa Iringa) wakati huo ambapo Horace Kolimba alikuwa Katibu mkuu wa CCM. Interestingly, Mzee Kihaule wakati anapigania Tanganyika alikuwa pia Naibu Spika wa Bunge. Baada ya sakata lile hakupata tena ubunge, CCM ilimtema na kumpa marehemu Horace Kolimba nafasi hiyo, huku Mzee Kihaule akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbarali, nafsi aliyodumu nayo hadi alipostaafu 2004. Mzee Kihaule alifariki mwaka 2012.
  23. Alhaji Mussa Nkhangaa: huyu alikuwa mbunge wa Iramba mkoani Singida. Baadaye katika serikali zilizofuata alipewa nyadhifa za uwaziri (ikiwemo ile ya waziri wa maji), na baadae akawa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
  24. Edward Oyombe Ayila: alikuwa mbunge wa Rorya. Yuko wapi?
  25. Adam Karumbeta: wa Mbeya huyu. Yuko wapi?
  26. Halimeshi Mayonga: alikuwa mbunge wa Kigoma vijijini. Yuko wapi?
  27. Dr John Katunzi: wa Geita. Yuko wapi?
  28. Ismail Ivwata: alikuwa Mbunge wa Manyoni Singida. Yuko wapi?
  29. Tobi Tajiri Mweri: alikuwa mbunge wa Pangani. Yuko wapi?
  30. Aidan Livigha: alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa (Lindi). Yuko wapi?
  31. Tabitha Ijumba Siwale (mama): Huyu alikuwa mbunge wa taifa, na kabla ya hapo aliwahi kuwa waziri katika wizara za elimu na baadaye ardhi. Kwa sasa ni mkurugenzi wa NGO iitwayo WAT (Women Advancement Trust), na pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Efatha Bank (ya nabii Mwingira).
  32. Obel Mwamfupe: wa Mbeya. Yuko wapi?
  33. Othman Ahmed Mpakani: wa Iringa magharibi. Yuko wapi?
  34. Evarist Mwanansao: wa Nkasi. Yuko wapi?
  35. Paschal Degera: wa Kondoa kaskazini. Yuko wapi?
  36. Erasto Losioki: wa Simanjiro. Yuko wapi?
  37. Nassoro Malocho: alikuwa mbunge wa Mtwara. Katika serikali iliyofuata ya Mhe Mkapa, aliteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais, Mipango.
  38. Charles Kagonji: huyu alikuwa mbunge wa Mlalo Lushoto. Alikuwa mwandishi wa habari ikulu enzi za Mwalimu Nyerere. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mzee Kagonji alikasirishwa na uchakachuaji aliofanyiwa na CCM kwenye kura za maoni akaamua kutimkia CHADEMA. Tofauti na wenzie waliotimkia CHADEMA kipindi hicho (akiwemo Hezekiah Wenje aliyekimbia CCM baada ya kuburuzana na Lawrence Masha kule Nyamagana) Mzee Kagonji alishindwa uchaguzi ule.
  39. Venance Francis Ngula: alikuwa mbunge wa Taifa. Katika uchaguzi uliofuata alichaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo Dar na kuteuliwa kuwa naibu waziri wa fedha.
  40. Benedict Kiroya Losurutia (marehemu): alikuwa mbunge wa Kiteto. Alifariki mwaka 2007.
  41. Dr Deogratias Mwita: wa Serengeti.Yuko wapi?
  42. Phineas Nnko: wa Arumeru Mashariki. Yuko wapi?
  43. John Peter Mwanga: alikuwa mbunge wa Moshi mjini na alikuwa miongoni mwa wabunge vijana wakati ule kwani alishinda ubunge akiwa anasubiria graduation yake pale Mzumbe. Ushindi wake mwaka ule wa 1990 dhidi ya Brigedia Muhiddin Kimario (ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani) zaidi ulitokana na kura alizopigiwa na wanafunzi wa sekondari na vyuo ambako ndiko alikowekeza zaidi nguvu kutokana na ushawishi wake kwenye UVCCM (ambao ulikuwa na matawi mashuleni na vyuoni) na MUWATA (Muungano wa wanavyuo Tanzania). Hata hivyo hakufanya lolote katika kipindi chake cha uongozi, kwahiyo alipotea kwenye ramani baada ya kipindi kimoja tu.
  44. Chediel Yohana Mgonja (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Same kwa miaka mingi, na enzi ya Nyerere aliwahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali ikiwemo Elimu. Anakumbukwa pia kwa ile kesi maarufu sana ya uchaguzi Same ya mwaka 1980-1982 ambako alishinda katika mahakama kuu lakini akaja kushindwa katika mahakama ya rufaa na kuvuliwa ubunge. Katika hukumu ya rufaa, aliadhibiwa kutogombea ubunge kwa miaka 10, lakini baadaye adhabu hiyo ilitenguliwa akaruhusiwa kugombea tena 1985 ambako alishinda na kushika vipindi viwili hadi 1995. Mzee Mgonja (ambaye wapare walimpa jina la utani “Kaghembe”) alifariki mwaka 2009.
  45. Guntram Amani Itatiro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Ifakara. Baada ya sakata lile la kudai Tanganyika, Mzee Ruksa alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ule utaratibu wa kofia mbili.
  46. Captain (mstaafu) Paschal Kulwa Mabiti: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.
  47. Edith Mallya Munuo (mama): Huyu alikuwa mbunge wa Taifa akiwakilisha umoja wa Wanawake wa CCM (UWT). Katika uchaguzi uliofuata miaka 2 baadaye (1995) CCM ilimtosa, akaamua kujiunga na NCCR Mageuzi na kugombea jimbo la Kawe ambako hata hivyo alishindwa. Aliteuliwa kuingia kama mbunge wa viti maalum kupitia NCCR Mageuzi, na baada ya hapo kwa sababu zisizoeleweka akatangaza kubadilisha jina lake kuwa “Edith Lucina”. Hivi yuko wapi siku hizi?
  48. Raphael Shempemba: wa Lushoto. Yuko wapi?
  49. Lt Col (mstaafu) John Mhina: wa Lushoto. Yuko wapi?
  50. Balozi George Maige Nhigula (marehemu): huyu alikuwa Mbunge wa Kwimba, Mwanza. Alikuwa muumini kwelikweli wa utanganyika maana alikuwa miongoni mwa maofisa wa mwanzo wa ubalozi za Tanganyika huru Ulaya miaka ya mwanzo ya uhuru. Alitumikia serikali miaka mingi kwa nyadhifa mbalimbali hadi alipostaafu mwaka 1985 na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Kwimba kwa vipindi viwili. Alistaafu siasa 1995 na kufariki mwaka 2011.
  51. Captain (mstaafu) Theodos James Kasapira (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ulanga magharibi, na kabla ya hapo alishakuwa mkuu wa wilaya mbalimbali. Capt Kasapira alifariki mwaka 2005.
  52. Charles Kinuno: alikuwa mbunge wa Nyanghwale. Yuko wapi?
  53. Christian Fundisha: wa Tabora Kusini. Yuko wapi?
  54. Samuel Ruangisa: alikuwa mbunge wa Bukoba Mjini kwa muda mrefu. Baadae CCM walimtosa kwenye ubunge lakini akabakia kwenye chama na kugombea udiwani na kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba. Mwaka jana Mhe Ruhangisa akiwa diwani wa kata ya Kitendaguro, alikuwa miongoni mwa wale madiwani wanane ambao CCM iliwafukuza uanachama kwa madai ya kumuunga mkono Kagasheki katika ugomvi wake dhidi ya aliyekuwa meya Anatoly Amani.
  55. Dr Maria Josephine Kamm (mama): huyu alikuwa mbunge wa taifa, na alipata umaarufu mkubwa akiwa headmistress wa secondary ya wasichana Weruweru ambayo pia ilikuwa maarufu sana enzi hizo. Kwa sasa Mama Kamm ni mstaafu, na ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Mama Clementina Foundation, asasi inayojishughulisha na elimu kwa wasichana.

Ahsante!
 
Kila ninapowasoma hawa wazee na jinsi walivyothubutu kuiweka mbele hoja yao WAZIWAZI, nashangaa ni kwanini watetezi wa Tanganyika wa leo wanaogopa kupiga kura ya wazi katika bunge la katiba? Kwa sasa hivi adui mkubwa wa kupatikana kwa Tanganyika ni unafiki. Wapo wabunge ambao vipembeni wanashabikia Tanganyika, wakiwa ndani ya jengo lenye kikao cha maamuzi wanaufyata, wanaogopa kuonesha msimamo huu waziwazi! Ndio kizazi cha opportunists tulichonacho, wachumia tumbo!
 
Na wana ushawishi gani kwa hoja hiyo kwa sasa? Hapa nawakumbusha kuhusu hawa wazee, maelezo mafupi kuwahusu, na kwa wale ambao sina habari zao wengine mjazie. Watu wa kuenziwa hawa:
  1. Njelu Kasaka: Huyu alikuwa mbunge wa Lupa mkoani Mbeya. Baada ya sakata lile mzee Ruksa alimpoza kwa kumzawadia unibu waziri. Katik hatua Fulani alikosana na wenye chama chao CCM walipomuengua kwenye kura za maoni, akakasirika akajiunga na CUF. Huko nako hazikuiva, njaa ilipomzidia akarudi “nyumbani” CCM. Msimamo wa CCM ni serikali mbili, kwa hiyo huyu kwenye wapigania Tanganyika keshapotezwa. Ni bahati mbaya sana kwani ndiye aliyekuwa kiongozi wa G55 mwaka ule wa 1993. .
  2. Lumuli Alipili Kasyupa: alikuwa mbunge wa Kyela kule kwa Mwakyembe. Yuko wapi?
  3. William Mpiluka: wa Mufindi, Iringa wakati huo. Yuko wapi? . Marehemu kwa sasa
  4. Mateo Tluway Qares: alikuwa mbunge wa Babati ambayo wakati huo ilikuwa mkoa wa Arusha. Baadae alipewa uwaziri kwenye serikali iliyofuata ya Mkapa .
  5. Jared Gachocha: alikuwa mbunge wa Ngara. Yuko wapi?
  6. Dr Mganga Titus ole Kipuyo: alikuwa mbunge wa Arumeru Magharibi
  7. Phillip Sanka Marmo: huyu alikuwa mbunge wa Mbulu mkoani Arusha (wakati huo). Alipokuwa anapigania Tanganyika alikuwa ‘benchi’, lakini katika serikali za awamu zilizofuata alipewa ulaji mfululizo wa uwaziri na sasa n balozi nchini China. Hana sababu tena ya kudai Tanganyika.
  8. Arcado Ntagazwa: huyu wakati huo alikuwa mbunge wa jimbo la Kibondo, na alikuwa ‘benchi’ pia. Kabla ya sakata la kudai Tanganyika alikuwa waziri wa maliasili na utalii katika ile serikali ya mwanzo ya Mzee Ruksa. Baada ya ishu kuzimwa, alipozwa na posts za uwaziri ambazo aliendelea kula nchi hadi walipokuja kumtosa katika awamu ya JK, na kwa hasira akaamua kutimkia CHADEMA. Bado atakuwa anaitaka Tanganyika yake.
  9. Patrick Silvanus Qorro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Karatu (Arusha) ndiye ambaye baadaye alikuja kuwa chanzo cha CCM kupoteza jimbo kwa CHADEMA hadi leo. Wakati wa kura za maoni ndani ya CCM mwaka 1995, marehemu Qorro alichuana na Dr Wilbrod Slaa ambaye ndiyo kwanza alikuwa ametoka kujiuzulu upadri na alikuwa amewekeza sana nguvu zake na mitandao yake katika miradi ya maendeleo Karatu, akitumia ushawishi alioujenga alipokuwa katibu mkuu wa TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki). Wana-CCM walimchagua Dr Slaa awe mgombea, lakini makao makuu wakatengua na kumweka Qorro. Dr Slaa alitimkia CHADEMA ambao walimpa tiketi ya kugombea, jimbo likabakia CHADEMA hadi leo. Mzee Qorro alifariki mapema mwaka huu.
  10. Japhet Sichona: wa Mbozi (Mbeya). Yuko wapi?
  11. Jenerali Twaha Khalfan Ulimwengu: huyu alikuwa mbunge wa Taifa (ndivyo walivyoitwa enzi hizo wale ambao hawakutokea majimboni). Kabla ya hapo aliwahi kuwa mkuu wa wilaya kule Hai, Kilimanjaro. Awamu iliyofuata ya Mzee Mkapa ilimnyanyasa sana huyu Ulimwengu kutokana na tabia yake ya “kushindana na serikali”, tena kuna wakati walitangaza kuwa siyo raia na akalazimishwa kuomba upya uraia au kuondoka nchini (nakumbuka sakata lilimhusu pia Mzee Anatoly Amani yule anayegombana na Kagasheki kule Bukoba, na bi Maudline Castico aliyekuwa katibu mwenezi wa CCM Zanzibar ). Mzee Ulimwengu ameendelea kuwa critical wa serikali lakini sasa hivi anafanya kwa upole si kama wakati ule walipomtishia kumtimua nchini. Bado ana guts za kudai Tanganyika?
  12. Abel K. Mwanga (marehemu): huyu alikuwa mbunge wa Musoma mjini, na pia alikuwa mwandishi mahiri wa vitabu vya kiada vya somo la kiingereza vilivyotumika katika shule za sekondari. Anatajwa pia kuwa ndiye aliyekuwa akimpa aliyekuwa waziri mkuu marehemu Edward Sokoine tuition ya lugha ya kiingereza. Mzee Mwanga alifariki mwaka 2009.
  13. Prof Aaron Eben Japhet Massawe: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, na kabla ya hapo alikuwa akifundisha katika chuo kikuu cha tiba Muhimbili. Ni mtaalamu bingwa wa magonjwa ya ngozi. Kwa sasa ni mstaafu anayetoa huduma za tiba katika hosptali yake binafsi. Ndoto za utanganyika hata kama bado anazo, hana nguvu nazo tena.
  14. Shashu Lugeye: alikuwa mbunge wa Solwa. Yuko wapi?
  15. Sebastian Rweikiza Kinyondo (marehemu): almaarufu “bwana mitemba”, alivuta sana kiko huyu jamaa, na alikuwa na sharubu fulani ambazo akiweka mtemba wake mdomoni zilimpa mwonekano wa kipekee sana. Alikuwa mbunge wa Bukoba vijijini. Baada ya sakata lile huyu naye alipozwa kwa kupewa uwaziri wa Kazi ambao alidumu nao hadi kifo chake.
  16. Phares Kashemeza Kabuye (marehemu): Huyu babu alikuwa mbunge wa Biharamulo ambaye alihangaikia sana misimamo yake hadi kifo. Baada ya sakata lile, uchaguzi uliofuata wa 1995 alijiunga na chama cha NCCR Mageuzi enzi hizo kikiwika sana kuliko CHADEMA ya leo, chini ya ‘Mangi’ Augustino Lyatonga Mrema na Katibu Mkuu wake Mabere Nyaucho Marando. Ulipotokea mtafaruku wa Marando na Mrema, Mzee Kabuye aliamua kuelekeza utiifu wake kwa Mrema, na akamfuata kwenye TLP yake ambako pia alishinda ubunge dhidi ya jamaa wa CCM aliyeitwa Anatoly Choya ambaye kwa sasa ni mkuu wa wilaya mojawapo. Mzee Kabuye alifariki kwa ajali ya basi alipokuwa safarini kufuatilia rufaa ya kesi yake ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa na Choya.
  17. Mbwete Polile Hombee: alikuwa mbunge wa Rungwe (Mbeya). Yuko wapi?
  18. Kisyeri Werema Chambiri: alikuwa mbunge wa Tarime. Yuko wapi? si yule mguge wa Babati??
  19. John Byeitima: alikuwa mbunge wa Karagwe. Yuko wapi?
  20. Abdallah Saidi Nakuwa: alikuwa wa Lindi. Yuko wapi?
  21. Dr Ndembwela Ngunangwa: alikuwa mbunge wa Njombe Kusini, mkoani Iringa (wakati huo Anna Makinda alikuwa mkuu wa Mkoa). Yuko wapi?
  22. Mathias Michael Kihaule (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ludewa (mkoa wa Iringa) wakati huo ambapo Horace Kolimba alikuwa Katibu mkuu wa CCM. Interestingly, Mzee Kihaule wakati anapigania Tanganyika alikuwa pia Naibu Spika wa Bunge. Baada ya sakata lile hakupata tena ubunge, CCM ilimtema na kumpa marehemu Horace Kolimba nafasi hiyo, huku Mzee Kihaule akiteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbarali, nafsi aliyodumu nayo hadi alipostaafu 2004. Mzee Kihaule alifariki mwaka 2012.
  23. Alhaji Mussa Nkhangaa: huyu alikuwa mbunge wa Iramba mkoani Singida. Baadaye katika serikali zilizofuata alipewa nyadhifa za uwaziri (ikiwemo ile ya waziri wa maji), na baadae akawa mkuu wa mkoa wa Dodoma.
  24. Edward Oyombe Ayila: alikuwa mbunge wa Rorya. Yuko wapi?
  25. Adam Karumbeta: wa Mbeya huyu. Yuko wapi?
  26. Halimeshi Mayonga: alikuwa mbunge wa Kigoma vijijini. Yuko wapi?
  27. Dr John Katunzi: wa Geita. Yuko wapi? Marehemu kwa sasa
  28. Ismail Ivwata: alikuwa Mbunge wa Manyoni Singida. Yuko wapi?
  29. Tobi Tajiri Mweri: alikuwa mbunge wa Pangani. Yuko wapi?
  30. Aidan Livigha: alikuwa mbunge wa jimbo la Ruangwa (Lindi). Yuko wapi?
  31. Tabitha Ijumba Siwale (mama): Huyu alikuwa mbunge wa taifa, na kabla ya hapo aliwahi kuwa waziri katika wizara za elimu na baadaye ardhi. Kwa sasa ni mkurugenzi wa NGO iitwayo WAT (Women Advancement Trust), na pia ni mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Efatha Bank (ya nabii Mwingira).
  32. Obel Mwamfupe: wa Mbeya. Yuko wapi?
  33. Othman Ahmed Mpakani: wa Iringa magharibi. Yuko wapi?
  34. Evarist Mwanansao: wa Nkasi. Yuko wapi?
  35. Paschal Degera: wa Kondoa kaskazini. Yuko wapi?
  36. Erasto Losioki: wa Simanjiro. Yuko wapi?
  37. Nassoro Malocho: alikuwa mbunge wa Mtwara. Katika serikali iliyofuata ya Mhe Mkapa, aliteuliwa kuwa waziri wa ofisi ya rais, Mipango.
  38. Charles Kagonji: huyu alikuwa mbunge wa Mlalo Lushoto. Alikuwa mwandishi wa habari ikulu enzi za Mwalimu Nyerere. Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Mzee Kagonji alikasirishwa na uchakachuaji aliofanyiwa na CCM kwenye kura za maoni akaamua kutimkia CHADEMA. Tofauti na wenzie waliotimkia CHADEMA kipindi hicho (akiwemo Hezekiah Wenje aliyekimbia CCM baada ya kuburuzana na Lawrence Masha kule Nyamagana) Mzee Kagonji alishindwa uchaguzi ule.
  39. Venance Francis Ngula: alikuwa mbunge wa Taifa. Katika uchaguzi uliofuata alichaguliwa kuwa mbunge wa Ubungo Dar na kuteuliwa kuwa naibu waziri wa fedha.
  40. Benedict Kiroya Losurutia (marehemu): alikuwa mbunge wa Kiteto. Alifariki mwaka 2007.
  41. Dr Deogratias Mwita: wa Serengeti.Yuko wapi?
  42. Phineas Nnko: wa Arumeru Mashariki. Yuko wapi?
  43. John Peter Mwanga: alikuwa mbunge wa Moshi mjini na alikuwa miongoni mwa wabunge vijana wakati ule kwani alishinda ubunge akiwa anasubiria graduation yake pale Mzumbe. Ushindi wake mwaka ule wa 1990 dhidi ya Brigedia Muhiddin Kimario (ambaye alikuwa waziri wa mambo ya ndani) zaidi ulitokana na kura alizopigiwa na wanafunzi wa sekondari na vyuo ambako ndiko alikowekeza zaidi nguvu kutokana na ushawishi wake kwenye UVCCM (ambao ulikuwa na matawi mashuleni na vyuoni) na MUWATA (Muungano wa wanavyuo Tanzania). Hata hivyo hakufanya lolote katika kipindi chake cha uongozi, kwahiyo alipotea kwenye ramani baada ya kipindi kimoja tu.
  44. Chediel Yohana Mgonja (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Same kwa miaka mingi, na enzi ya Nyerere aliwahi kuwa waziri wa wizara mbalimbali ikiwemo Elimu. Anakumbukwa pia kwa ile kesi maarufu sana ya uchaguzi Same ya mwaka 1980-1982 ambako alishinda katika mahakama kuu lakini akaja kushindwa katika mahakama ya rufaa na kuvuliwa ubunge. Katika hukumu ya rufaa, aliadhibiwa kutogombea ubunge kwa miaka 10, lakini baadaye adhabu hiyo ilitenguliwa akaruhusiwa kugombea tena 1985 ambako alishinda na kushika vipindi viwili hadi 1995. Mzee Mgonja (ambaye wapare walimpa jina la utani “Kaghembe”) alifariki mwaka 2009.
  45. Guntram Amani Itatiro (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Ifakara. Baada ya sakata lile la kudai Tanganyika, Mzee Ruksa alimteua kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro kwa ule utaratibu wa kofia mbili.
  46. Captain (mstaafu) Paschal Kulwa Mabiti: huyu alikuwa mbunge wa jimbo la Mwanza. Kwa sasa ni mkuu wa mkoa wa Simiyu.
  47. Edith Mallya Munuo (mama): Huyu alikuwa mbunge wa Taifa akiwakilisha umoja wa Wanawake wa CCM (UWT). Katika uchaguzi uliofuata miaka 2 baadaye (1995) CCM ilimtosa, akaamua kujiunga na NCCR Mageuzi na kugombea jimbo la Kawe ambako hata hivyo alishindwa. Aliteuliwa kuingia kama mbunge wa viti maalum kupitia NCCR Mageuzi, na baada ya hapo kwa sababu zisizoeleweka akatangaza kubadilisha jina lake kuwa “Edith Lucina”. Hivi yuko wapi siku hizi?
  48. Raphael Shempemba: wa Lushoto. Yuko wapi?
  49. Lt Col (mstaafu) John Mhina: wa Lushoto. Yuko wapi?
  50. Balozi George Maige Nhigula (marehemu): huyu alikuwa Mbunge wa Kwimba, Mwanza. Alikuwa muumini kwelikweli wa utanganyika maana alikuwa miongoni mwa maofisa wa mwanzo wa ubalozi za Tanganyika huru Ulaya miaka ya mwanzo ya uhuru. Alitumikia serikali miaka mingi kwa nyadhifa mbalimbali hadi alipostaafu mwaka 1985 na kuchaguliwa kuwa mbunge wa Kwimba kwa vipindi viwili. Alistaafu siasa 1995 na kufariki mwaka 2011.
  51. Captain (mstaafu) Theodos James Kasapira (marehemu): Huyu alikuwa mbunge wa Ulanga magharibi, na kabla ya hapo alishakuwa mkuu wa wilaya mbalimbali. Capt Kasapira alifariki mwaka 2005.
  52. Charles Kinuno: alikuwa mbunge wa Nyanghwale. Yuko wapi?
  53. Christian Fundisha: wa Tabora Kusini. Yuko wapi?
  54. Samuel Ruangisa: alikuwa mbunge wa Bukoba Mjini kwa muda mrefu. Baadae CCM walimtosa kwenye ubunge lakini akabakia kwenye chama na kugombea udiwani na kuchaguliwa kuwa Meya wa Manispaa ya Bukoba. Mwaka jana Mhe Ruhangisa akiwa diwani wa kata ya Kitendaguro, alikuwa miongoni mwa wale madiwani wanane ambao CCM iliwafukuza uanachama kwa madai ya kumuunga mkono Kagasheki katika ugomvi wake dhidi ya aliyekuwa meya Anatoly Amani.
  55. Dr Maria Josephine Kamm (mama): huyu alikuwa mbunge wa taifa, na alipata umaarufu mkubwa akiwa headmistress wa secondary ya wasichana Weruweru ambayo pia ilikuwa maarufu sana enzi hizo. Kwa sasa Mama Kamm ni mstaafu, na ni mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji wa Mama Clementina Foundation, asasi inayojishughulisha na elimu kwa wasichana.

Bolded
 
Mytake: Hata hawa wanaopigiana kelele bungeni tutawasahau na hatutajua walipo after few years. Usipoweka legacy ya kueleweka tutakusahau tu.
 
Mkuu Setuba Noel kudos hii ndo JF home of Great Thinkers sio hawa watoto wavamizi wanaharibu heshima ya jukwaa
 
Last edited by a moderator:
Asante sana kwa kuleta rekodi hiyo.

Sijajua msukumo wao wakati ule ulikuwa ni nini kwa vile bado kulikuwa na matumani ya kufikia lengo la kuwa na serikali moja. Inawezekana walishayaona mapema mambo haya ambayo tunayaona leo kuwa serikali ya Muungano ilikuw inapotzea nguvu huko Zanzaibar na vile vile wazanzibar walikuwa wakishika madaraka ndani ya serikali ya Muungano kushughulika na mambo ya Tanganyika ambayo hayakuwa ya muungano.
 
Sahihisho dogo wakati Mzee Ngunangwa akiwa mbunge Mama Makinda alikuwa waziri wa wanawake na watoto! Ila umetoa nondo safi!
 
Wengi wamefariki pia. Mbunge Byeitma wa Karagwe alishafariki, Mzee Nassoro wa Mtwara naye alishafariki
 
Back
Top Bottom