Wakiota mapembe waongezee na mkia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,715
729,888
Hiyo heading ni sehemu ya mashairi ya mwanamuziki Darasa katika wimbo wake uliobamba vilivyo mwishoni mwa mwaka ulioopita.

Napenda bongofleva lakini si mpenzi wa aina ya muziki auimbao Darasa! Ila maneno haya yamenifanya niusikilize kwa makini wimbo ule.

Kuna usemi wa kiswahili usemao kelele za chura hazimzuii tembo kunywa maji...chura hupiga kelele kumtisha tembo asinywe maji kwakuwa wanadhani kwa umbo lake kubwa anaweza kuhamishia maji yote tumboni mwake nao wakakosa cha kunywa wakafa.

Siasa ndio tarumbeta la viongozi na dhima ya chama cha Siasa cha upinzani ni kukosoa pale chama tawala kinapokosea...kwa njia hii chama tawala huwa makini sana...na hii ni haki ya kikatiba popote penye utawala wa sheria.

Sina mapenzi na wamarekani siwafagilii kwenye mambo mengi sana kwa sehemu naweza kusema mimi ni mpinzani wao lakini misimamo yangu hii na ya wengine wote inayofanana na yangu haijamzuia mmarekani kufanya kile anachoamini ni sahihi kwa muktadha wake kwa hili tumeendelea kuwa wanafunzi wasioelimika mbele ya mmarekani.

Juzi hapa walikuwa na uchaguzi na kwa mshangao wa wengi akachaguliwa mtu ambaye hafananii wala haikutegemewa kuwa angechaguliwa kuwa rais wa taifa hilo kubwa ulimwenguni.

Tulizishuhudia hasira za watu kwa kuharibu virus vyao vya thamani na maandamano ya kila wakati mpaka siku ya kuapishwa ambayo nayo maandamano yalikuwa si haba.

Hivi vyote havikuwanyima wafanya maamuni kuendelea na ratiba zao wanajua fika maandamano hayo ni sawa na kelele za chura zisizomzuia tembo kunywa maji sana sana waliwapa waandamanaji uangalizi na ulinzi wa vikosi vya ulinzi na jeshi la polisi.

Rais yuko Ikulu annaendelea kuchapa kazi wanaojisikia kuandamana juani na kuandika mabangoakubwa ya kila aina hawazuiwi tena wanapewa na ulinzi kutokana na kodi wenyewe.

Je, tuna la kujifunza hapa?
 
kuna mahali inafikia nakuwa na mapenzi ya dhati kwa wamarekani na marekani yenyewe sababu kuu ni kuupenda umarekani wao...!!hata raisi waliempata ndio wale conservatives kabisa wa ule umarekani wao kweli kunalakujifunza hapa,maana tunapenda sana umarekani kwa yale tutuonayo yanatufurahisha lakini si kwa yale yanayotuchukiza katika upande ya yanayotuchukiza wanao nekana kukerwa na hayo ni hawa wakubwa katika ofisi zetu za umma..!hawa pendi kusikia demokrasia na uhuru wakutoa maoni,wamejivika gamba linaloitwa uchochezi..!
 
Trump kama Tembo,hao wanao andamana izo kelele zao ndio za chura,hazimzuii yeye kusign executive order zingine!
yapo mengi yakujifunza sana
 
kuna mahali inafikia nakuwa na mapenzi ya dhati kwa wamarekani na marekani yenyewe sababu kuu ni kuupenda umarekani wao...!!hata raisi waliempata ndio wale conservatives kabisa wa ule umarekani wao kweli kunalakujifunza hapa,maana tunapenda sana umarekani kwa yale tutuonayo yanatufurahisha lakini si kwa yale yanayotuchukiza katika upande ya yanayotuchukiza wanao nekana kukerwa na hayo ni hawa wakubwa katika ofisi zetu za umma..!hawa pendi kusikia demokrasia na uhuru wakutoa maoni,wamejivika gamba linaloitwa uchochezi..!

Huwa wanapenda kuanza na hili neno 'we Americans....! au in America....!
 
waandamanaji wa tanzania wengi ni wanywa viroba ivyo ni rahisi wao kufanya uhalifu ndio maana wanazuiwa.
 
wabongo hatuandamani kutaka haki, tunaandamana kutaka fujo
halafu mkizoea kuandamana mtaandamania hata vitu visivyo na maana.
 
Back
Top Bottom