Hay wanajamvi wenzangu
Mnaendeleaje na pilika pilika za maandalizi ya sikukuu ya Pasaka, na mambo mengine
kiujumla, mwenzenu niko fiti naendelea vyema na shughuli zangu za kunipatia kipato cha kula
Awali ya yote nimeonelea leo niongee au nizungumzie tabia chafu ya baadhi ya WANAUME
ambao wamekuwa kero kila kona. Kitu ambacho nataka nikisema leo jamani wandugu tena
naomba marafiki zangu wanaume wa humu jf mmu msinielewe vibaya kwa hoja hii. ni kuhusu
UCHAFU WA BAADHI YA WANAUME ambao umekuwa kero kwetu hasa jamii nzima, lakini sio wote
ambao ni wachafu au wananuka, bali wako baadhi ambao wanajiendekeza kwa unukaji, na wengine
wanadiriki kuvaa nguo wiki nzima, wao hawaoni kuwa ni chafu bali ule UVIVU uliowatawala ndani
yao wanashindwa hata kufua jamani. na wengine inapita siku tatu hawaogi, ukisema wanasema
kuwa wao ni wanatashati, heee! jamani utanashati gani huo?
Sasa mtu kama huyo anayejifanya eyeye ni mtanashati hebu mfanye naye kazi sehemu moja
kwenye meza moja huku Airconditioner iwe imewashwa utakimbia mahali hapo kwani huo uharufu
unaotoka hapo utasema kuwa PANYA AMEFIA WAPI TUMTAFUTE, kumbe sio panya ni yeye ananuka
vibaya, mbaya zaidi wengine wanashindwa hata kunyoa sehemu zile ...............................
(sizitaji kwa usalama zaidi) kwani harufu ya huko si mchezo wengine ukipishana nao wananuka vinywa utafikiri wajapiga mswaki mwaka mzima jamani we acha, mm Lady sitaki kuongeza chumvi hapo
ila nasema vijana, makaka zetu na mababa zetu jamani acheni tabia hiyo ya uchafu ni hatari kwa afya
zenu na afya za familia zenu jamani. Labda niwashauri wanawake wenzangu kama mkiona wanaume zenu ni wachafu wasemeni msiwaogope kwani hao wamekuwa simba mpaka muwaogope, sema nao kwa nguvu zote, na kama hawajirekebishi basi chukua uamuzi wa kuwakimbia maana ni hatari kwa afya zenu.
Onyo: Akina makaka, mababa, vijana wetu acheni tabia ya uchafu kwa uvivu wenu wa kutokujipenda
ninyi ni viongozi wa familia mnataka watoto wajifunze wapi huo uchafu wenu?
NASEMA JAMANI ACHENI TABIA YA UCHAFU NADHANI MESSAGE SEND